princess ariana
JF-Expert Member
- Aug 19, 2016
- 9,652
- 19,264
bulichekaTehtehtehteh...nimecheka sana, inaelekea vijana wa zamani mnakumbuka Enzi zenu....Hivi hebu niambie lile kabila la Wagagagigikoko lilikuwa linasimuliwa katika kitabu gani vile??
bulichekaTehtehtehteh...nimecheka sana, inaelekea vijana wa zamani mnakumbuka Enzi zenu....Hivi hebu niambie lile kabila la Wagagagigikoko lilikuwa linasimuliwa katika kitabu gani vile??
Upo sahihi kabisa ndiyo viliitwa hivyo na mara nyingi watu hupata simulizi za mdomo kuliko kuvisoma vitabu vyenyewe vimekuwa adimu sana mimi mzee wangu hiki kitabu cha Allan quartermein alikuwa nacho kipya kabisa so nimekisomea nyumbani ingawa kuna baradhuli mmoja alikuja kukikwepua baadae ila kilikuwa na msisimko hata kuwapa watu ujasiri wa bandia na kujifanya wenyewe nao kama yule mzee mzulu nakumbuka alipomwambia makumazahn "makumazahn nakufa lakini kifo hiki kimetabiriwa na watu wa zamani saa yetu imefika ewe muindaji mzee na ije! tumeishi si haba lakini ningependa kuona vita vingine kama vile vya jana wanizike kwa desturi za kikwetu makumazahn wauelekeze uso wangu kuelekea nchi ya uzulu.Hekaya za Abunuasi.
Hata mimimie ndiyo kwanza naona hapa.
View attachment 403987na shoka lake la inkos-kaaz
(Umsolopagazi na inkosikazi)[/QUO
Mshana Jr,View attachment 403987na shoka lake la inkos-kaaz
(Umsolopagazi na inkosikazi)
Sorais...Malkia Solaisi
Tufanyie ihsani muungwana kwa kuzidi kutushushia khabari hizi maana wengine tumezipata baadhi tu na vingine kama hivi tunazidi kutanua ufahamu wetu Shukran sana sheik mohamed.Mshana Jr,
Umenipeleka mbali sana kaka.
Ngoja nami nikupeleke Scotland Milimani kuna sehemu nadhani
wanaita Castle huko ni Edinburgh.
Hii ni sehemu maarufu kwa watalii.
Basi siku moja nimetoka Glasgow nimekuja Edinburgh kisha nikapandisha
mlimani kwenye ''castles,'' nanyoosha miguu.
Nikakuta ''pub,'' au nyumba sina hakika khasa maana miaka mingi imekwenda.
Nje kuna kibao kuwa Rider Haggard alikuwa akikaa hapa na kuandika vitabu
vyake.
Roho ikanindunda.
Huyu Rider Haggard ndiye mwandishi wa ''Allan Quatermain,'' ambamo ndani
ya kitabu hiki utamkuta huyo Umslopogaas.
Ninazo picha nikizipata nitazileta jamvini tustaladhi sote.
Kitabu hiki kilikuwa maarufu sana kwa sisi tuliokuwa shule katika miaka ya 1960.
Pamoja na kitabu hiki kulikuwa na kingine Machimbo ya Mfalme Suleiman.
Ukikishika hukiweki chini.
Siku hizo serikali ikitoa vitabu vya kusoma bure kwa shule.
Siku nyingine niko Paris nanyoosha miguu.
Nikakuta mtaa unaitwa, ''Alexandre Dumas,'' au ''Victor Hugo.''
Huyu pia alikuwa mwandishi maarufu sana katika wakati wake.
Victor Hugo ndiye mwandishi wa ''The Hunchback of Notre Dame'' na Alexandre
Dumas aliandika, ''The Count of Monte Cristo.''
Nikasimama kuzubaa na kibao kile kwa muda.
Mwili unanisisimka kwani najua raha niliyokuwa nikipata utotoni katika vitabu hivi.
![]()
Mwandishi na James Brennan Magomeni Mapipa, Dar es Salaam 2010
Siku nyingine niko kwenye gari ya rafiki yangu James Brennan tunatoka Iowa ananileta
Chicago nipande ndege kwenda New York.
Tukafika Mississippi River.
Akawa ananieleza kuwa huu mto unaitwa Mississippi.
Nikamwambia, ''Jim hebu pumzisha pumzi zako mimi mto huu nyumbani kwangu.''
Mmarekani kashtuka hajanifahamu vyema.
Nikamwambia, ''Jim, mimi nilikuwa na rafiki zangu hapa - Tom Sawyer na Huckleberry
Finn.''
Jim akacheka sana huku anatingishwa kichwa.
''Mohamed you never cease to amaze me!''
Hawa Tom Sawyer na Huckleberry Finn ni ''characters'' katika kitabu cha Mark Twain.
Mmarekani kashangaa kuwa huyu Mswahili kawajuaje hawa watu?
Mshana Jr,
Ahsante sana kwa kunitia katika ''Time Machine,'' na kunirudisha nyuma nikawa mtoto tena
wa miaka 12.
Someni kwa furaha; sterling alikuwa Bulicheka na mkewe Lizabeti, upande wa pili kulikuwa na Mfalme Huhihuhi ambaye alipigwa na Bulicheka.Tehtehtehteh...nimecheka sana, inaelekea vijana wa zamani mnakumbuka Enzi zenu....Hivi hebu niambie lile kabila la Wagagagigikoko lilikuwa linasimuliwa katika kitabu gani vile??
Hiki kizazi kinawaza miziki ya kufokafoka na Bongo flavour tu; siku hizi wamekuja na Singeli, yaani wanaimba na kuzunguka tu kama wamepandwa na mashetani.Mwanamakumazan alievuka maji ya shingo bila mbupu kulowa hahaaa heshima kwako kk mshana jr kwa kunikumbusha hii mambo zmn tulifaidi sn tofauti na hiki kizazi cha shigongo
Asante mkuu,huyu mzulu hakika alikuwa na matambo kweli kweli.Upo sahihi kabisa ndiyo viliitwa hivyo na mara nyingi watu hupata simulizi za mdomo kuliko kuvisoma vitabu vyenyewe vimekuwa adimu sana mimi mzee wangu hiki kitabu cha Allan quartermein alikuwa nacho kipya kabisa so nimekisomea nyumbani ingawa kuna baradhuli mmoja alikuja kukikwepua baadae ila kilikuwa na msisimko hata kuwapa watu ujasiri wa bandia na kujifanya wenyewe nao kama yule mzee mzulu nakumbuka alipomwambia makumazahn "makumazahn nakufa lakini kifo hiki kimetabiriwa na watu wa zamani saa yetu imefika ewe muindaji mzee na ije! tumeishi si haba lakini ningependa kuona vita vingine kama vile vya jana wanizike kwa desturi za kikwetu makumazahn wauelekeze uso wangu kuelekea nchi ya uzulu.
Ndipo alipozitelemka ngazi yule mtu mkubwa kisha likatokea tukio la ajabu yule kala mtu wa zuvendi nae akatelemka ndipo umslopogaaz akasema na wewe unakuja? karibu shujaa mimi napenda kuona watu wanakufa kishujaa Aaah tu tayari tunainoa midomo yetu kama tai! Mikuki yetu inang'aa katika miali ya jua! Nani anataka kuja kumsabahi inkosikazi ambaye matunda ya kumbusu kwake ni kifo! Mimi gota gota!mimi umslopogaaz mwenye shoka! Mshindi asiye shindika mimi mkuu wa kikosi cha nkomabakozi mimi mwana wa makedama! wa damu ya chaka mimi nawaita kama kulungu aitwavyo njooni!
kitabu adhim hichi kaka,nilikisoma nikiwa nakua nacho kilikua cha bibi yangu kipenzi,umenikumbusha mbali sana mshanaView attachment 403987na shoka lake la inkos-kaaz
(Umsolopagazi na inkosikazi)
Guasa,Tufanyie ihsani muungwana kwa kuzidi kutushushia khabari hizi maana wengine tumezipata baadhi tu na vingine kama hivi tunazidi kutanua ufahamu wetu Shukran sana sheik mohamed.
What a great memory thanks so much for sharing! Pls usisahau pichaMshana Jr,
Umenipeleka mbali sana kaka.
Ngoja nami nikupeleke Scotland Milimani kuna sehemu nadhani
wanaita Castle huko ni Edinburgh.
Hii ni sehemu maarufu kwa watalii.
Basi siku moja nimetoka Glasgow nimekuja Edinburgh kisha nikapandisha
mlimani kwenye ''castles,'' nanyoosha miguu.
Nikakuta ''pub,'' au nyumba sina hakika khasa maana miaka mingi imekwenda.
Nje kuna kibao kuwa Rider Haggard alikuwa akikaa hapa na kuandika vitabu
vyake.
Roho ikanindunda.
Huyu Rider Haggard ndiye mwandishi wa ''Allan Quatermain,'' ambamo ndani
ya kitabu hiki utamkuta huyo Umslopogaas.
Ninazo picha nikizipata nitazileta jamvini tustaladhi sote.
Kitabu hiki kilikuwa maarufu sana kwa sisi tuliokuwa shule katika miaka ya 1960.
Pamoja na kitabu hiki kulikuwa na kingine Machimbo ya Mfalme Suleiman.
Ukikishika hukiweki chini.
Siku hizo serikali ikitoa vitabu vya kusoma bure kwa shule.
Siku nyingine niko Paris nanyoosha miguu.
Nikakuta mtaa unaitwa, ''Alexandre Dumas,'' au ''Victor Hugo.''
Hawa pia walikuwa waandishi maarufu sana katika wakati wao.
Victor Hugo ndiye mwandishi wa ''The Hunchback of Notre Dame'' na Alexandre
Dumas aliandika, ''The Count of Monte Cristo.''
Nikasimama kuzubaa na kibao kile kwa muda.
Mwili unanisisimka kwani najua raha niliyokuwa nikipata utotoni katika vitabu hivi.
![]()
Mwandishi na James Brennan nyumbani kwangu Magomeni Mapipa, Dar es Salaam 2010
Siku nyingine niko kwenye gari ya rafiki yangu James Brennan tunatoka Iowa ananileta
Chicago nipande ndege kwenda New York.
Tukafika Mississippi River.
Akawa ananieleza kuwa huu mto unaitwa Mississippi.
Nikamwambia, ''Jim hebu pumzisha pumzi zako mimi mto huu nyumbani kwangu.''
Mmarekani kashtuka hajanifahamu vyema.
Nikamwambia, ''Jim, mimi nilikuwa na rafiki zangu hapa - Tom Sawyer na Huckleberry
Finn.''
Jim akacheka sana huku anatingishwa kichwa.
''Mohamed you never cease to amaze me!''
Hawa Tom Sawyer na Huckleberry Finn ni ''characters'' katika kitabu cha Mark Twain.
Mmarekani kashangaa kuwa huyu Mswahili kawajuaje hawa watu?
Mshana Jr,
Ahsante sana kwa kunitia katika ''Time Machine,'' na kunirudisha nyuma nikawa mtoto tena
wa miaka 12.
Huu mkwara alikuwa anampiga yule mkuu wa wajivuni wa sehemu ya. ...amboni ambae alikuja pale kwa bwana makenzie na kapu lililokuwa na maua pia barua aliyo andika flossie yule bint wa makenzie "tarishi wa kwanza tulie mtuma hakuongea akionyesha kichwa cha yule mjakazi wa bwana makenzie alie kwenda na flossie.Dah mkuu mshana jr umenikumbusha masimulizi ya hivi vitabu vya Sir Haggard,Naweza sema huyu mzulu Msolopagazi ni moja kati ya binadamu wa Riwayani wenye mikwala ya hatari .....moja kati ya majigambo yake alipokutana na wajivuni "Mimi msolopogaas,mwana wa inkosikazi,mjukuu wa makumazan,nyanya wa khumabakoz, wa damu ya Chaka, wa kabila la Wazulu, mkuu wa jeshi la Nkomabakosi, kama wengi wengine walivyofanya; nawe utajiinamisha mbele ya Inkosikazi kama walivyofanya wengi wengine. Ndiyo, cheka, cheka! Usiku wa kesho
fisi watakuwa wanacheka na huku wanavunja na kuzitafuna mbavu zako."...Huyu mtu hataree sana mkuu,asante kwa hizi kumbukumbu kiongozi.
Vyama Vingi,Someni kwa furaha; sterling alikuwa Bulicheka na mkewe Lizabeti, upande wa pili kulikuwa na Mfalme Huhihuhi ambaye alipigwa na Bulicheka.
Vv
Mshana Jr,What a great memory thanks so much for sharing! Pls usisahau picha
Mshana,Am sure nilishawahi kukutana nawe lakini sijui ni wapi
Guasa...Huu mkwara alikuwa anampiga yule mkuu wa wajivuni wa sehemu ya. ...amboni ambae alikuja pale kwa bwana makenzie na kapu lililokuwa na maua pia barua aliyo andika flossie yule bint wa makenzie "tarishi wa kwanza tulie mtuma hakuongea akionyesha kichwa cha yule mjakazi wa bwana makenzie alie kwenda na flossie.
Baada ya kutoa maelezo na kugeuka nyuma ili aondoke ndipo akakuta yule mzee mzulu kasimama nyuma yake akamwambia pisha upesi ile kauli ikaonekana kumkera yule mzulu na kumpelekea uso wake mkali na kumwambia waniona? Yule mjivuni akajibu nakuona kitwana! kisha umslopogaaz akalipeleka shoka lake na kwamwambia yaliona hili? yule mjivuni akajibu la nini? Umslopogaaz akasema "wewe mjivuni mbwa mkamata watoto wa kike kwa mchezo huu nitavitapanya viungo vyako katika majani tukipambanishwa wawili nitakuonyesha mambo cheka cheka lakini usiku wa kesho fisi watakuwa wakicheka huku wakizitafuna mbavu zako.