Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Mzee Mohamed Said, nimeipitia.
Sasa maalimu kakusahau weye na kunisema mimi kuwa nina ghasia waqt wewe ndio unamchokoza na kumtoa huko aliko ila yote kheri tuendelee kumtafuta afungue kichwa aende penye kina kirefu cha bahari alete samaki wazuri Shukran nyingi kwako ndugu
 
Kuna baadhi ya vitu huwakutanisha watu kiroho hii post ni kimojawapo! najiona mimi wa wakati huo nikisoma hivi vitabu mstari kwa mstari
Swadakta swahiba wangu mada imewafikirisha wenye mada na pia wenye kupenda vitu vya kale hisia zinarudi nyuma na kukumbuka mbali
 
Sasa maalimu kakusahau weye na kunisema mimi kuwa nina ghasia waqt wewe ndio unamchokoza na kumtoa huko aliko ila yote kheri tuendelee kumtafuta afungue kichwa aende penye kina kirefu cha bahari alete samaki wazuri Shukran nyingi kwako ndugu
Guasa! Huyu mzee ana vitu kichwani balaa.
Bila kumsahau mzuvendi mshana jr. Ukiwachokoza hawa watu utapata vitu vingi sana.
 
Nasubiri maalim Mohamed anipe kisa cha Marehemu Kolimba na mwl nyerere. Bifu lao lilivyokuwa.
 
Nenda samora bookshop ya Tph,pale nilikuta had Adili na nduguze,merchant of Venice
 
Nimepita huko maalimu ingawa si mara ya kwanza kupita ila leo umakinika wangu umeongezeka zaidi na zaidi ila uchokozi huu au ghasia hii ipogolo ndo kaianzisha.
Guasa...
Ahsante sana kaka nyote mna kesi ya kujibu...

Miaka kama 30 iliyopita wakati naanza utafiti huu kwa kweli kila
hatua nilikuwa nakutana na mambo yaliyonistaajabisha sana.

Leo wapo watu na wao wanapigwa na butwaa nikiwahadithia haya
na kuna wengine wanaghadhibika na kunitukana hadi kufikia kunitisha.

hapa mimi hustaajabu upya na kujiuliza, ''Kwani kuna nini hapa?''
 
Swadakta maneno yako tufunge buti pamoja sana ndugu yangu
Guasa...
Mtatupasua vichwa hebu tuhurumieni.
Umri tu kaka kuwa tumetangulia kwa hiyo njia tumeanza kuijua sie.

Leo mimi mwanafunzi kwa wanangu katika IT ingawa mimi ndiyo mtu
wa kwanza kuwasikisha key board.
 
Guasa...
Mtatupasua vichwa hebu tuhurumieni.
Umri tu kaka kuwa tumetangulia kwa hiyo njia tumeanza kuijua sie.

Leo mimi mwanafunzi kwa wangu katika IT ingawa mimi ndiyo mtu
wa kwanza kuwasikisha key board.
Huruma kwa hili haipo maalimu sababu mtaondoka na hazina zenu watu wa jana hutufundisha somo la kesho simaanishi punda afe mzigo ufike ila kutokana na global warming vyanzo vya maji vingi hupotea basi kijua ndio hiki wacha tuuanike tusije utwanga mbichi.
 
Huruma kwa hili haipo maalimu sababu mtaondoka na hazina zenu watu wa jana hudundisha somo la kesho simaanishi punda afe mzigo ufike ila kutokana na global warming vyanzo vya maji vingi hupotea basi kijua ndio hiki wacha tuuanike tusije utwanga mbichi.
Guasa...
Ukiutwanga mbichi unadoda...
Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua...

Wazungu nao wana yao, ''Make hay while the sun is shining...''
 
Guasa...
Ukiutwanga mbichi unadoda...
Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua...

Wazungu nao wana yao, ''Make hay while the sun is shining...''
Swadakta ndo maana twataka umwage vitu watu wachukue bila ghasia na uchokozi huwezi kumbuka.
 
Guasa...
Ukiutwanga mbichi unadoda...
Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua...

Wazungu nao wana yao, ''Make hay while the sun is shining...''
Umesema kama mwanamume inkubu ya nini kuogopa? yule mtoto wa kike kasema watakula na kufanya karamu na iwe karamu yao ya mazikoni! Yule mbwa ninae tumaini kumuumbua kutakapo pambazuka amesema hatuwezi kuwashambulia sababu tu wachache! bwana mkubwa makenzie ana watu ishirini na kuna watu watano wako makumazahn kisha kuna watu weupe watano wanatosha kabisa tazama vita vitapiganwa hivi wakati mwangaza unaanza kuangazia pembe za ng'ombe si kabla wala baada (makumazahn wewe ni mzee na mwerevu wa mambo ya vita!
Unalijua lile boma waliloweka kambi niliiona asubuhi! Akachora chini hapa kuna mlango mkubwa umezibwa kwa miiba inkubu mimi na yule mkazi mwenye kifua kipana ni mtu jasiri tutasimama hapo na mashoka yetu.
Bougwan na watu wake kumi waende penye mlango mdogo wamuue yule mlinzi anaeshika zamu bila kufanya sauti kisha watu wengine waliobaki wagawanywe kwa makumazahn na bwana mkubwa kisha utakapo fanya sauti ya mlio wa ng'ombe wewe makumazahn basi waanze kushambulia lakini wakimuangalia yule mtoto wa kike basi kwa milio ya bunduki ya makumazahn na kwa makelele ya sauti ya juu ya ukuta ya watu wa bougwan basi wajivuni wale kwa pombe nyingi walizo kunywa na kwa hamaki ya kuamshwa usingizini watajikusanya na kuelekea lango la miiba basi hapo watatukuta na inkubu hilo ndio shauri langu makumazahn kama nawe una shauri jema liseme.
Basi hapo nikawaambia maneno mengine wasio yaelewa kisha wote tukakubaliana na mbinu za yule mzulu nikamtania aah mzee simba unajua jinsi ya kuvizia na jinsi ya kuuma unajua pahala pa kushika na mahala pa kushika akajibu ndio makumazahn vita vitakuwa vyema.
 
Mwaga vitu kaka mwaga...

Umenirudisha 1963 Kinondoni Primary School...na mie mkutubu
wa darasa na ''time keeper'' mgonga kengele.

Bibi yangu Mwantum biti Rajabu alikuwa ana kibiashara chake
pale shule akiuza maharage kipimo kikombe cha kahawa.

Hela yake mwenyewe kaifunga kwenye upande wa khanga.

Likibaki rojo lile ni la waume zake mimi na rafiki zangu tunakwenda
kusafisha sufuria.

Hatukusikia kipindupindu wala nini...
Hapo nyumba juu kuti chini tope.

Iko siku nilipata hamu ya kwenda kuangalia shule yangu.
Siku nzima sikuwa na raha najiuliza kulitokea nini?

Maua tuliyokuwanayo pale shule hakuna...

Madarasa hayana milango wala madirisha, makabati tuliyokuwa tunawekea
vitabu hivi vya Msloopogas maktaba ya darasa hakuna hata hilo kabati...

Nimebakia nimeduwaa...
Yarabi nini kimetokea?

Na hii wala haikuwa shule ya matajiri.
Tukisoma sisi watoto wa watu wa kawaida kabisa.

Kulikuwa na timu kali ya kabumbu, net ball, riadha tukiongoza mkoa wa Dar
Salaam.

1966 darasa zima limepasi kwenda sekondari.

Nikamkumbuka Mr. Romenesko mwalimu Peace Corps mwalimu wetu wa
Kiingereza aliyetufunza kucheza base ball na mwalimu wa riadha...
 
Back
Top Bottom