Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,305
Duh! Kisa kilianzia pale lamu baada ya kuongea na bwana balozi ndie aliwapa maelezo ya kwenda kuonana na bwana makenzie aishie mwishoni mwa mto tana akawaamibia inabidi muwe na wapagazi wa kuwabebea vitu vyenu nje ya mji kuna wakazi walikuja na bwana wao alie kuwa amekwenda kuupanda mlima kilimanjaro lakini wakati wa kurudi akapata maradhi ya homa na kufariki nendeni mkawaone .Guasa...
Mwaga vitu...
Naisubiri ile ya ''kubonga.''
We mtu hatari sana kaka.
Hizi hazina za kale ndugu yangu.
Kwanza hilo neno mslopoganz nilisikia kwenye wimbo wa profesa jay basii na sikuwah kulifatilia ,,nilijua ni jina tuu kumbe kuna kitabu chakeTupo wengi kumbe.
Late 80'stells us your age!!!
Mie hata sijawahi lisikia.....Kwanza hilo neno mslopoganz nilisikia kwenye wimbo wa profesa jay basii na sikuwah kulifatilia ,,nilijua ni jina tuu kumbe kuna kitabu chake
Legendary wa kizulu alikuwa noma sana story zake ni tamu ila zinatisha na zimejaa ukatili
basi nami ngoja nianze kutafuta swaga.Ooopsie wanafanana.
Basi nieshaanza kulifanyia kazi...subiria mrejesho kupitia kipakato chako!!!
Sikumbuki jina lake ndugu na kuvipata siku hizi ni kazi sana
Elfu Ulela Lela km sikosei
Hivi Agon alikuwa kwenye hiki kitabu au ni kile cha Mashimo ya Mfalme Suleiman?
Nafikiri huyo alikuwa kwenye kitabu cha Mashimo ya Mfalme Suleiman lakini mtunzi wa vitabu hivyo viwili alikuwa ni mmoja - Mwingereza huyo alikuwa kichwa kweli kweli, si rahisi kuamini kama adithi hizo niza kutunga!
Yote tisa, lakini binafsi naona Alan Quaterman ilikuwa kibiko zaidi, yaani tukiwa shule ya msingi unaona usiku unakawai unatanani kuche haraka uende kusoma Msolopogasi na Bwana Good na lodi yake!!
Kitabu hicho kilitafusiliwa kutoka lugha ya kingereza, Kiswahili chake kilikuwa kizuri sana, sasa sijui kwa nini Wizara ya Elimu ilikifuta badala yake wakatunga vitabu vya kusifia vijiji vya ujamaa, watendaji wakuu wa vijiji na maduka ya ushirika - ajabu kweli kweli!!! Serikali yetu ilijitumbukiza kichwa kichwa ku-copy idealogy za Warusi na Wachina za kusifia viongozi na kulaani everything Western, mpaka vitabu vya kufundisha kingereza vilivyo tungwa kwa ajili ya shule za East Africa navyo wakavipiga marufuku - wakatunga vya kwao wakiwa na lengo ka kuvuna pesa - vitabu vyenyewe ukivisoma ni sawa sawa na hakuna kabisa, alafu tunashangaa kwa nini watoto wetu kingereza kinawapiga chenga.