Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,455
- 32,981
Guasa...Shukran in advance ndugu
Hata sijui tukushukuru vipi.
Ahsante sana kaka.
Guasa...Shukran in advance ndugu
Mkuu hiyo Avatar yako nadhani ni... Ambiere.. KiviereWashindadhe...!!
njoo huku napata1 Barid
waiter mletee Mshana jr![]()
![]()
Makumazahn ninayo maneno ya kusema lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyonge kama hawa maneno yangu ni baina ya mimi na wewe ila nitasema hayaAlikuwa kibaraka wa wazungu according to simulizi...
[HASHTAG]#Musaliti[/HASHTAG]
Dah itakuwa powa sana mkuu, nirushie na inbox aisee..
Many thanks mkuu...Hiki hapa kwa faida ya wote mkuu.
Umsolopaganz ndo limetulia zaidi.MAKUMAZAN bonge moja la a.k.a nalitumia kitaa
Tuliwahi kukisoma shule za msingi miaka ya 70s. Baadae kilikuja kupigwa marufuku na serikali,kwa maelezo kwamba kilikuwa kinadhalilisha utu wa muafrika. Miongoni mwa vitabu vilivyopigwa marufuku wakati huo ni pamoja na 'Revolution in Zanzibar' cha Field Marshal John Okello na kile cha 'Jando na unyago'.Legendary wa kizulu alikuwa noma sana story zake ni tamu ila zinatisha na zimejaa ukatili
Hongera...kwa mtirirko huu unajua mengi aisee......sie miaka hiyo ndiyo kwanza wazazi wanazaliwa.Mshana Jr,
Umenipeleka mbali sana kaka.
Ngoja nami nikupeleke Scotland Milimani kuna sehemu nadhani
wanaita Castle huko ni Edinburgh.
Hii ni sehemu maarufu kwa watalii.
Basi siku moja nimetoka Glasgow nimekuja Edinburgh kisha nikapandisha
mlimani kwenye ''castles,'' nanyoosha miguu.
Nikakuta ''pub,'' au nyumba sina hakika khasa maana miaka mingi imekwenda.
Nje kuna kibao kuwa Rider Haggard alikuwa akikaa hapa na kuandika vitabu
vyake.
Roho ikanindunda.
Huyu Rider Haggard ndiye mwandishi wa ''Allan Quatermain,'' ambamo ndani
ya kitabu hiki utamkuta huyo Umslopogaas.
Ninazo picha nikizipata nitazileta jamvini tustaladhi sote.
Kitabu hiki kilikuwa maarufu sana kwa sisi tuliokuwa shule katika miaka ya 1960.
Pamoja na kitabu hiki kulikuwa na kingine Machimbo ya Mfalme Suleiman.
Ukikishika hukiweki chini.
Siku hizo serikali ikitoa vitabu vya kusoma bure kwa shule.
Siku nyingine niko Paris nanyoosha miguu.
Nikakuta mtaa unaitwa, ''Alexandre Dumas,'' au ''Victor Hugo.''
Hawa pia walikuwa waandishi maarufu sana katika wakati wao.
Victor Hugo ndiye mwandishi wa ''The Hunchback of Notre Dame'' na Alexandre
Dumas aliandika, ''The Count of Monte Cristo.''
Nikasimama kuzubaa na kibao kile kwa muda.
Mwili unanisisimka kwani najua raha niliyokuwa nikipata utotoni katika vitabu hivi.
![]()
Mwandishi na James Brennan nyumbani kwangu Magomeni Mapipa, Dar es Salaam 2010
Siku nyingine niko kwenye gari ya rafiki yangu James Brennan tunatoka Iowa ananileta
Chicago nipande ndege kwenda New York.
Tukafika Mississippi River.
Akawa ananieleza kuwa huu mto unaitwa Mississippi.
Nikamwambia, ''Jim hebu pumzisha pumzi zako mimi mto huu nyumbani kwangu.''
Mmarekani kashtuka hajanifahamu vyema.
Nikamwambia, ''Jim, mimi nilikuwa na rafiki zangu hapa - Tom Sawyer na Huckleberry
Finn.''
Jim akacheka sana huku anatingishwa kichwa.
''Mohamed you never cease to amaze me!''
Hawa Tom Sawyer na Huckleberry Finn ni ''characters'' katika kitabu cha Mark Twain.
Mmarekani kashangaa kuwa huyu Mswahili kawajuaje hawa watu?
Mshana Jr,
Ahsante sana kwa kunitia katika ''Time Machine,'' na kunirudisha nyuma nikawa mtoto tena
wa miaka 12.
Tupo wengi kumbe.Hata mimi
Guasa...Makumazahn ninayo maneno ya kusema lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyonge kama hawa maneno yangu ni baina ya mimi na wewe ila nitasema haya
Mwanamke mzuri alinihaini mautini akalifunika jina langu kwa aibu ndio mke wangu mwenyewe mwanamwali mwenye uso kama mwezi hata hivyo niliepuka kutoka katika mikono ya waliokuja kuniua nilipiga mapigo matatu kwa inkosikazi hili hakika baba yangu utalikumbuka moja upande wa kuume moja upande wa kushoto moja mbele toka nyumbani kwangu baba yangu nilikimbia na wale matarishi wa mauti walinifuata na kama ujuavyo ingawa ni mzee lakini miguu yangu ni mwepesi kwenda mbele kama paa na wala hakuna awezae kunishika niishapo toka ubavuni pake nilikimbia na wale matarishi walinifuata na sauti zao zilikuwa kama mbwa wanaowinda nikampita yule alie nihaini kisimani kama kivuli cha mauti kisha nikapiga pigo moja tahamaki kichwa chake kikatumbukia kisimani nami nisisimae nikazidi kukimbia mpaka nilipo kutana na safari ya mwindaji yule mweupe ambae amekwisha fariki nami nimekuja na watu wake hapa!
Sikuchukua kitu chochote pamoja nami ila shoka langu la vita ambalo kwa nguvu zake nilitawala watu wangu wametwaa ng'ombe zangu wamechukua wake zangu ila kwa shoka hili hili nitakata njia nifike penye ustawi nimesema aaaa