Wanene kuongezewa marupurupu

Wanene kuongezewa marupurupu

Hakuna kashfa hapa! nimeeleza maisha aliyokulia zitto ndio sababu ya kufanya uovu wake.

BI Sent 50.

tuwekee picha ya harusi ya wazazi wake zitto. hilo litadhibitisha uongo wangu.

Malezi kwa watoto ni muhimu sana. ukiyakosa unaweza kuwa kauzu ukubwani.

Sasa kama ni hivyo ndugu yangui Mswahili kwani kumsakama Zitto na si malezi? Kwani kumkashifu na kumsakama hadi mzazi wake kana kwamba alikosea kumzaa Zitto?

Wataka kutuambia kuwa malezi yako yalikuwa perfect? Kama ni hivyo basi usitumie 'kivuli' (Mswahili) come with your full detaila- jina lako na mahali unapotoka uone ili uwape Wana JF na wakujuao nafasi ya kujadili kuhusu background yako na wazazi wako. Nadhani hutafanya na wakianza kuwajadili wazazi wako utajisikia vibaya sana maana hawakufanya kosa kukuzaa na kukulea pia udhaifu wao have nothing to do with udhaifu wako.

Simtetei Zitto hapa ingawa ni mdogo wangu lakini bado issue ya hii thread bado haihusiani na suala la Zitto bali mustakabali wa Taifa.
 
Kitila,

Tatizo kubwa hapa halikuwa Zitto bali hao waliojaribu kutumia nguvu zote kumkingia asijibu maswali. Hilo lingefanikiwa ingelikuwa failure kubwa sana ya JF.

JF sio Mwanakijiji, badala yake ni members wote kuanzia wanaosoma tu mpaka wale wanaochangia kwa kuandika.

Binafsi nilishutushwa sana na baadhi ya kauli za watu hasa Mwanakijiji kuhusu
kwamba haya ni mambo binafsi wakati huko nyuma mambo hayo hayo ya nguoni yanajadiliwa hapa tena na watu hao hao.

Mimi siilaumu CHADEMA maana kuna wana Chadema mliamua kutokukaa kimya na mkasema, kwa aina moja ama nyingine mlisaidia kuondoa hii perception ya
kwamba CHADEMA wanapendelewa hapa JF. I hope huko chini chini hutaonja joto la jiwe la chama.

Mzee ES, usijali itabidi tuendelee kulinda heshima ya JF kwa kuhakisha hakuna mwanachama au chama ambacho kina nguvu kuliko JF.

I hope kuna siku Mwanakijiji atapata courage ya kumfunga paka kengele na kumhoji rafiki yake Zitto juu ya hiyo scandal kama anavyowahoji viongozi wengine. Kama atakatiwa simu pia ni mategemeo yangu atatuambia wana JF.
 
Acha kuhalalisha wizi.. hapa alieibiwa ni Mohammed Mpakanjia kwa maana amechukuliwa chake bila ya ridhaa yake.


Myopic view of sexual relationships kudhani kuwa mwanamme ndiye anayemmiliki mwanamke tu not otherwise.
 
My only plea is that our criticism should always be evidence-based, objective, constructive and not eroding others' dignity as people and human beings!

Mkubwa nakuelewa sana. Kwa binadamu wengi, "the Other" is an object, hata kama ni binadamu. Tunasahau kwamba what you look at the mirror is also "the Other".

Tutaendelea kuambiana ukweli na kuonyeshana njia pale unafiki unapokuwa dhahiri.



Big points,

Nilivyoona hapa ni kwamba watu walikuwa na jazba na Zitto binafsi kiasi kuwa asiyekubaliana na approach au maneno yao alionekana anafanya hivyo kulinda CHADEMA au ana double standard, kama kwamba sis wote hapa ni wanachama wa CHADEMA. Binafsi nimepingana na hawa jamaa siyo kwa sababu natetea uzinzi wa Zitto wala kuuona hauna maana, nilichopinga ni jinsi walivyofanya mashambulizi na kutaka tukubaliane nao bila kutupa evidence zaidi ya tunavyofahamu, wakidai kuwa Zitto ni mzinzi mkubwa na mwizi, lazima aje hapa ajibu maswali. Kwanza kabisa, nilionya kuwa hata kama ni kweli kuwa Zitto alimbeba yule mama, bado anaweza asikubali kutokana na fedheha ya jambo lenyewe, hiyo ni tabia ya binadamu mpaka umuonyeshe ushahidi (kumbuka Clinton-Monica). Kwa hiyo, baada Zitto kujibu kuwa hakuhusika, walitakiwa wamuulize kwa kutumia ushahidi uliopo lakini badala yake wao wakawa explosive na kupoteza control. Binafsi niliwauliza sana jamaa hawa huko nyuma kama wana ushahidi kuonyesha kuwa aliyosema Zitto si kweli. Mswahili akatoa sababu za kimazingira kuhoji ukweli wake; nikamwambia kuwa sababu za kimazingira hizo ndizo alizotakiwa kuziweka hapa zijadiliwe kuliko maneno aliyoleta. Mzee ES akasema yeye ana ushahidi kamili wa kuonyesha kuwa kweli yule Zitto alizini na Amina, nikamwambia kuwa angetoa ushahid huo hapa kama alivyofanya kwenye skendo nyingine tungemunga mkono lakini hadi sasa bado hajautoa; nilirudia ile thread ya Zitto/Amina kwenye vibweka na kusoma posts zote sikuona ushahidi wowte mpya zaidi ya tunavyofahamu. Wengine walikuwa wakishambulia bila kuwa na punje ya ushahidi wowote bali kwa kutumia blanket tu kuwa mbona viongozi wengine hushambuliwa wakifanya makosa, kwa nini Zitto asishambuliwe.

Maishani yangu nimejifunza kuwa katika mambo ya jamii kila mtu ana mtazamo wake, hii ni tofauti na sayansi ambako kila swali lina jibu moja tu. Kwa hiyo ushahidi unatakiwa sana katika mambo ya kijamii, na hata hivyo kila mtu bado anaweza kuwa na tafsiri tofauti ya ushahidi huo. Ndiyo maana mahakama kuu nyingi duniani zinakuwa na majaji ama watatu, au watano, au saba au tisa n.k. kwa kufuata msululu huo wakielewa kuwa majaji wengine watakuwa na tafsiri tofauti na ushahdi utakaotolewa. Kwa hiyo ni muhimu sana kutumia hoja ili kuwavuta wale wanaopinga mtazamo wako.

In any case, hata mimi nilikatishwa tamaa sana na watu wanaotumia nguvu na matusi kuendeleza mawazo yao badala ya kutumia hoja kuelemisha wengine, na kudhani kuwa wao ndio wanajua zaidi ya wengine wakati wote. Kama wao walivyokuwa katishwa tamaa na jinsi nilivyowapinga binafsi, ndivyo na mimi nilivyokuwa tamaa na jinsi wanavotoa mawazo yao bila kuyapima.
 
Sijaona swali la kusema tuunge mkono! na hakuna mahakama ya dini, kabila wala nchi inayoweza simamisha madai kama haya kwa dhana!.. ati imani za Uchawi wa kina Nchimbi ambaye tumemzoea kila Uchaguzi wa CCM.
Binafsi nawaona wale wanaotaka kulipeleka swala hili kuwa personal ndio wenye matatizo maanake wanatumia uvumi kuendesha shughuli zao. Kibaya zaidi ni kwamba WAMETUMWA sii bure maanake haiwezekani Zitto azungumziwe maisha yake, familia yake na kadhalika hali Amina mtuhumiwa mwingine ni Malaika!..
je, sio huyu huyu MwanaKijiji aliyeanzisha kampeni ya kumwachia Amina Chifupa Huru?... mbona sikuona maswali mengi wakati Ule ila leo inapofika kwa Zitto - Mwanakijiji ni...
Hii mada haina mpango kabisa uchawi mtupu!
Dr. Nchimbi got what he wanted! na anafanikiwa kila siku kwani wadanganyika tupo wengi.
 
je, sio huyu huyu MwanaKijiji aliyeanzisha kampeni ya kumwachia Amina Chifupa Huru?... mbona sikuona maswali mengi wakati Ule ila leo inapofika kwa Zitto - Mwanakijiji ni...
.


Kama alivyosema mwenyewe mwanakijiji tatizo letu moja ni short attention span, kwa hiyo tunasahau mapema. Mwanakijiji of all the people amekuwa devils advocate, yeye hujitahidi kusimama katika haki na ukweli mara nyingi kuliko wengi wetu hapa. Of course, yeye ni binadamu na amefanya makosa hapa na pale, lakini hili la kuhusu Zitto sio sehemu ya makosa aliyowahi kuyafanya.

Nilichogundua katika hii forum, pamoja na mambo mengine, kuna watu wapo kwa ajili ya kukatisha tamaa what wanaojaribu kuwa-advance a good course. Mwanakijiji amejaribu kuibuka na initiative nyingi sana mojawapo ikiwa swala la Ukraine. Sasa kuna watu hapa JF wameshindwa kuchangia kwa sababu ya ukata au kutoamini hiyo course au roho mbaya na wivu, wameamua kumuangukia mwanakjiji pasipo na sababu zozote. Kama mtu huwezi kuchangia kwa sababu yeyote ile acha na kaa kimya, wapo watakaoguswa na haiwezekani wote tuguswe na tatizo kwa namna inayolingana. Kama mtu huwezi kucngia, huna sababu za kuhalalisha kushindwa kuchangia kwako kwa kuwazushia watu mambo ambayo hayana maana.

Ushauri kwa Mwanakijiji: najua kuna baadhi ya posts katika siku mbili zilizopita zitakuwa zimekukwaza as a human being na kukufanya ujiulize maswali mengi. Naomba nikutie moyo kuwa njia ya kuleta mabadiliko na kutetea wanyonge haijawahi kuwa rahisi. Kwa hiyo don't be disappointed, keep up the struggle, in the process you will make some enemies, but many friends and well wishers. Change has and will never be (een) easy! God bless you abundantly!
 
hahahh... Mswahili wangapi hapa tunapenda ngono? Kama wewe hupendi ni matatizo yako kaka na inaweza kutoa jibu kwanini umemshupalia Zitto, mama yake n.k Nimefuatilia unavyoandika katika mada mbalimbalii. Jambo moja nimegundua ni kuwa hakuna sentensi au hoja utakayosema bila kumtaja mwanakjj. Imefikia mahali kuna mtu kauliza kama kuna beef kati yenu na hata wengine wamefikia mahali pa kufikiria huenda mmezidiana kete. Hata hivyo kwa jinsi unavyoandika mimi nafikiri ni zaidi ya hivyo. Haiwezekani hata kidogo kutaja jina la mwanamme mwenzio kila mara hadi kufikia kutuambia juu ya ugovi wake bila kuwa na sababu kubwa ya msingi.

Nikifuata Freudian psychology, yote inahusiana na frustrations za ngono.

Hivyo nilichotaka kumuuliza ndugu yetu Mswahili, inakuwaje umfikirie mwanamme mwenzio kiasi hicho? Inawezekana kuwa una "manly crush" na huwezi kusikia raha ya roho hadi utaje jina lake? Binafsi sina tatizo na hilo kwani nawajua baadhi ya watu wa pwani walivyo. Sasa kaka kama umempenda au unataka akurudishie penzi ni bora muambiane maana mtu hakujibu, wala kukuacknowledge kila unapomtaja, na wewe huridhiki kila sentensi ni "mwanakijiji hiki, mwanakijiji kile".

Kama kaka tumeshakupoteza kwa "timu ile" basi sawa tunaomba uje clean angalau tujue. Hivyo naomba ndugu Mswahili uje utuambie imekuwaje umtaje taje mwanamme mwenzio hivyo na kwa kila jambo. Mara hukosi kusikiliza radio yake, mara tulimmiss kwa wiki tatu, mara hivi na vile. Sijui mara ya mwisho mwanakijiji kukujibu hapa ilikuwa lini.

Kwa ufupi, kama mnatakana au kama unataka akutake napendekeza mambo hayo myafanye chemba. Mimi pia ni msikilizaji mwaminifu wa karedio kake, lakini wakati ule anaumwa hakusema lolote kuhusu "kukatwa" kwake, kwa vile wewe unajua hilo lote, kwa vyovyote kuna vitu vinaendelea baina yenu nyinyi wawili. So, tafute chumba myamalize.

Na kaka Mwanakjj, kama anataka usimpuuzie tu, mjibu angalau aridhike.

Asante.
 
Bi Sent 50
Kama Unaipepeka Topik Huko.basi Nisubiri Nitarudi Jioni. Adm Wameanza Niache Nimalizie.
Wanabodi Leo Msilale Nakuja Kumwaga Radhi.
Huyo Mwanakjj Kila Mara Ananitumia Pm.nitaziweka Hapa
 
Mswahili, acheni kutuzingua hapa yaani wewe na Mwanakijiji maanake naona ugonvi wenu unaanzia hapa kwa huyu bibiye senti 50!..

Bi.senti 50,
Mimi nafikiri kuwa wewe ndio sababu ya yote!.. unajua tena Ukame mbaya sana, kipindi toka tuwe na mwanamke humu. haaa haaa haaa!

Tutashukuru sana kama mtaendelea kutumiana PM, maanake haya tena sii maswala yetu!
 
mswahili.. kaka mwaga mambo yote hadharani... ili tujue kumbe ninyi wawili mko "beneti" Sasa mtatupata kina dada wengi hapa, haya ndiyo tunayaita ya udaku. Ya Zitto wewe yaache tuletee ya kwako na ya mwanakijiji, tumechoka kuwazungumzia watu wanaoingia mara moja kwa mwezi. Wewe njoo na umwage vitu hapa. Haya ukweli njoo, uongo njoo, na utamu kolea!

Nilijua kuna kakitu kako ndani ya muroho yako kaka, sema hadharani watu watakuelewa. Na nina uhakika patatosha kabisa!

Halo halo... la bata!!!
 
Mkandara, vipi upo?

Haa, haa, haa, haa, haa, haa, wuui, uhu, uhu, uhu, khu, khu,

Juzi nilikuwa nasoma posts hizi na mke wangu akasema bila shaka kuna mtu alizidiwa kete kwa mrembo huko mtaani hivyo sasa ameamua kuja juu; nikampinga kuwa watu wanatofautiana jinsi wanavyotoa uzito kwa kosa lolote, kwa hiyo kosa hilo hilo wengine wanalipa uzito sana wakati wengine wakiliona dogo. Sasa Bi.seti 50 karudia maneno yale yale aliyotoa mke wangu, naona wanawake wanaangalia swala hilo kwa kina sana.

Haah, haa, haah, haah, ha, ha, haah

Wo lala
 
Kitila,

Nafikiri inatosha kurudia threads mbalimbali za Mwanakijiji na kuona jinsi
watu mbalimbali walivyotoa support. Binafsi nakubaliana na Mwanakijiji 99 % ya muda na hoja zake. Lakini njia aliyotaka kutumia ili Zitto asihojiwe kwenye hili ilinitia kichefuchefu kweli kweli.

Unless una ushahidi wote waliopingana kwa nguvu zote na Mwanakijiji wanafit kwenye hiyo characterisation yako, inakuwa sio vizuri kuanza kuongelea motives bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Lakini pia hii kama Forum lazima mtegemee kuwa na watu wa aina mbalimbali. Kama mtu unafanya kitu unachokiamini, sioni kwanini ukatishwe tamaa na maneno ya watu wengine.

Fundisho hapa ni kwamba kama una scandal, watu wataiongelea. Huwezi kuja na excuse ya kusema utaongea kwa wakati wako. Usipotaka kuongea ni hiari yako lakini huwezi kuwazuia watu wasijadili kwa kisingizio cha eti utasema on your own terms. Hiyo haikubaliki na tumempinga Zitto na tutawapinga wengine pia. Njia pekee ya ku avoid kusemwa hapa ni kuwa clean au kutokuwa public figure. Bahati mbaya wengi wetu sio clean na siku ikifika tutasemwa kama leo tunavyowasema wengine. Sitategemea mtu anikingie kifua watu wasijadili suala langu ili mradi kama lugha inayotumika ni ya kiungwana na haiendani na matusi.
 
Kichuguu,

Lakini pia huenda wanaangalia kwa kina kidogo zaidi. Wanaona ni jambo la kawaida. Kumbuka weusi walivyosema kwa Clinton, walimwona ni mwenzao
na ana sifa zote zinazolingana na wao ikiwemo hiyo ya kuzunguka nyuma ya nyumba.
 
Mswahili + Dr DAU,

I wish ushauri ama shinikizo analolitoa Mswahili kwa Zitto angelitoa kwa Dr DAU pia kutokana na ile kashfa za wizi wa mabilioni na nyinginezo NSSF.

Tanzanianianjema
 
Kichuguu,

Lakini pia huenda wanaangalia kwa kina kidogo zaidi. Wanaona ni jambo la kawaida. Kumbuka weusi walivyosema kwa Clinton, walimwona ni mwenzao
na ana sifa zote zinazolingana na wao ikiwemo hiyo ya kuzunguka nyuma ya nyumba.


Jambo hili halikuwa dogo kwangu binafsi, ukipitia maandiko yangu utaona wazi kuwa sikuwa nimesema ni jambo dogo. Ila nimetofautiana kabisa na approach ya wenzangu hasa baada ya Zitto kuwa amesema kuwa hakuhusika na skendo ile. Nilikuwa naamini kabisa kuwa hivyo ndivyo atakavyojibu, na baadaye tungeweza kumwuliza maswali ya ziada kiungwana. Tungeuliza kiungwana, angeweza kutoa taarifa nyingine hata zile ambazo hakutegemea kutoa, halafu by connecting dots tungeweza kupata picha zaidi ya what happened. Kudhani kuwa utamwuliza aseme moja kwa moja kuwa "ndiyo nilimkamata yule mama mara kumi nilikuwa natumia soksi" na vitu kama hivyo ni kutokuwa serious, na I guess ndiyo hiyo hata Mwanakijiji alikuwa akipinga.
 
Kichuguu,

"hasa baada ya Zitto kuwa amesema kuwa hakuhusika na skendo ile"

Zitto lini alisema hilo? Hii hapa juzi baada ya kumpigia makelele au unasema ile aliyokaririwa na mwandishi wa gazeti? Kama ni ile ya gazetini nafikiri ulisoma hoja za wengine. Ile habari kisheria ilikuwa sio ya Zitto kwasababu hakuandika yeye kama article. Unless kama mwandishi alikuwa na kanda akimnasa Zitto akisema yale maneno, vinginevyo yale maneno ni udaku tu ambao mahakamani
angeweza kuuruka kirahisi. Hata hapa JF angeweza kuja kuruka kama mambo yanaharibika huko mbele. Refer case ya Clinton na utajua nina maana gani.

Alichokiandika hapa JF kwa maandishi yake ndicho tunakubaliana nacho. Amesema yale maneno ya gazetini ni sahihi kwahiyo wengine tumemuelewa.

Na ukisoma hoja zangu zote kwamimi huo ndio ulikuwa mwisho wa hoja yangu kwa Zitto. Kilichofuata ni kuhusu Mwanakijiji na jitihada yake ya kuzuia watu wasiulize maswali ambayo ni valid na yeye mwenye amekuwa akiyauliza mara nyingi huko nyuma. Hicho ndio kilichonisikitisha mimi zaidi maana hiyo ni double standard. Hii ingeachiwa ilikuwa hatari zaidi kuliko hata kutembea na mke wa mtu.

Hata kama hatasema lakini nina ahakika Mwanakijiji amejifunza kwamba JF ni huru na haitaburuzwa hata mhusika awe nani na kwa misingi hiyo JF itadumu, vinginevyo ingeonekana CCM nyingine yenye wenye nayo.
 
Back
Top Bottom