Nisome tena
Wapi nimerukaruka
Mi nimekujibu ulichoandika!
Na nimesema personally siwezi ku handle hayo mambo...sina huo moyo kabisa...
Nimekujibu ni bora ahonge hizo pesa zake sio atafute mke ale mchepuko...sio fair..
Sijasema kuwa watu wawe tayari kuvumilia umalaya wa waume zao...
Ndo maana divorce rate ni kubwa, na zinaombwa na wanawake
Sijui hata unachokataa ni nini wewe mwanamke, wakati comments zote unakubaliana na nadharia yangu.
Angalia comment yako ya kwanza hii halafu tuichambue kimantiki sawa.
"
Tuanze chini , tukijipata anaanzq kuongeza michepuko pesa inaenda nje , ndani unaanzq kuhangaika pesa yote nje
Ya nn yote hayo?"
Katika muktadha wa ndoa kwenye comment yako hii unamaanisha kwanza sisi wanaume tukianza kushika pesa lazima tuwe na michepuko na lazima tuhonge hiyo michepuko.
Sass basi wewe binafsi hauko tayari kuolewa na mwanaume kapuku, kwa sababu siku wewe na mwanaume huyu kapuku mkiaanza kupata pesa, mwanaume huyu kapuku ataanza kuwahonga michepuko kitu ambacho kitakuuma sana maana atakuwa anahonga pesa ambazo wewe na yeye mmeshirikiana kuzitafuta, yaan utaona ni kama vile jasho lako linaenda kuliwa na mwanamke mwingine... na ndio maana ukamaliza kwa kusema "ya nini yote hayo".
Katika muktadha huo huo wewe uko tayari kuolewa na mwanaume ambaye tayari ana pesa zake, na mwanaume huyu unaona ndio sahihi kwa mwanamke anayetaka kuolewa... kwa mwanaume huyu haujatilia maanani sana possibility ya yeye kuchepuka, kama ambavyo umetilia maanani possibility ya mwanaume yule kapuku kuchepuka akishapata pesa kwenye scenario ya kwanza.
Sasa swali, kichwani mwako unaamini sisi wanaume kuchepuka ni kasumba yetu, kwanini haujali kabisa suala la mwanaume huyu tajiri kuchepuka? Jibu liko wazi tu ni kwa sababu haukushiriki kuzitafuta pesa za huyu mwanaume wewe umezikuta tu ndio maana hata akichepuka huko na kuzihonga zote wewe hauumii kwa chochote kama ambavyo ungeumia endapo kma mngekuwa mmeshirikiana wote kuzitafuta.
Sijajua nini kinakufanya mpaka unakataa hii fact na wakati fikra zako zinaonesha huu ukweli ulio uchi... naona mwenzako hapo kakubali wazi kwa sababu kila mwenye akili timamu anaye reason properly ndio kitu anachokiona kwenye maandishi yako.
Hata kwenye hii comment yako unakubali, lakini bado unaiweka kinamna ya kukataa angalia "
ni bora ahonge pesa alizotafuta mwenyewe, lakini sio zile alizotafuta mke.. sio fair... sasa hapa si unakubaliana na mimi?