Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,618
Wanabodi,
Huku nikiisubiri kesho kwa hamu kushuhudia akili za wanawake kwenye kilele siku ya wanawake duniani hapo Machi 8, huku nikitafakari mwelekeo na mustakabali wa siasa zetu za hapa nyumbani Tanzania, nimekuja kujiridhisha kiukweli kabisa ukubali, ukatae, kumbe wanawake wana akili sana kutushinda sisi wanaume!, ila wengi walikuwa hawalijui hili kwasababu siku zote sisi wanaume tumekuwa tunawabania, tunawazibia na kuwakandamiza!.
Na hata huyu Mwanamke Numero Uno Tanzania, kiukweli alibaniwa sana na kama sio Mwenyeenzi Mungu kuingilia kati na kumuibua, kamwe tusingeutambua uwezo wake na akili zake!.
Hata kwenye medani za siasa na uongozi, kiukweli kabisa wanawake wameonyesha uwezo na kuwa na akili nyingi zaidi ya nanaume!, na akili kubwa kuliko wanaume ambao ni akili ndogo!.
Kesho tutashuhudia kundi fulani la wanawake 19 wenye akili kubwa, likiibuka kidedea dhidi ya kundi fulani kuubwa na watu fulani ambao huwa wanataniwa jina fulani la Utani!.
Hata wale wanyama Nyumbu, kwenye Serengeti migration, ,je ulijua kumbe mnyama ambaye huwa anaongoza kuvuka mto ni jike?. Kama ulikuwa hujui sasa ndio ujue na usubirie kesho na kushuhudia wanawake wenye akili kubwa wakifanya vitu vikubwa!.
Nahitimisha hili swali, ni wangapi humu walikuwa wanajua wanawake wana akili na uwezo kuliko mwanaume?. Yaani hata Eva, kumbe alikuwa na akili kuliko Adamu na kiukweli ndio maana wakiamua kitu ni wameamua!. Na usikute sisi ambao ni dhaifu kwa jinsia ile ndio maana tunapelekwa pelekwa, kwa kifupi tunapelekeshwa!.
Tena sio tuu wanawake wana akili kuliko wanaume bali hata uwezo!, Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ...
Hata kwenye kazi Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
Baada ya kuujua ukweli huu, sasa ni mwendo wa heshima na adabu kwa wanawake wote. Siku ya wanawake duniani, hongera wanawake wote duniani.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali.