Uchungu wa uzazi unatokana na kutanuka kwa cervix?? SawaKwani unapodungwa sindano ya ganzi ili kung'oa jino inakuwaje husikii uchungu?
Naelewa ni vitu viwili tofauti lakini vinalingana.
Uchungu wowote mwilini hutokea pale receptors zinapopeleka habari ya uchungu kwenye ubongo na ubongo kutoa jawabu kuwa hakika huu ni uchungu.
Uchungu wa uzazi unatokana na kutanuka kwa cervix ambayo inakuwa imefuka kabisa kuzuia hata tone la maji kutoka halafu hutanuka mpaka ukubwa wa sentimeta 10.
Ganzi inachofanya ni kuzuia receptors kupeleka habari ubongoni kwa hiyo uchungu hupati.
Kitu kingine ni wakati wa kukata roho,hiki ndio kichungu zaidi kuliko
Tunahitaji mafundisho zaidi lakini siyo sehemu Za wazi Kama hizi ambako wanaume wanatusoma na watoto pia!
Kila ktk maisha kinahitajika mafundisho iki kiweze kufanyika Kwa usahihi !
Kwa sababu ni boy acha nikusamehe
Tukiacha kuzaa wewe yamkini usingezaliwa
Mmmhh shikamooh mama mie nilivyoenda leba nasikia nilisema "uwiii wanaume wote wafe" manesi wakanijibu afe wa kwangu tu maana waume zao bado wanawapenda hahahhaha sitaki kusikia leba maana akili haikuwa yangu mweehh shkamooh mama
Hivi mjamzito asipofanya mapenzi kipindi chote cha ujauzito,anaweza akapata shida kujifungua?
kwani wewe unafikiri uchungu wa uzazi kiini chake ni nini?Uchungu wa uzazi unatokana na kutanuka kwa cervix?? Sawa
Ahsante sanaPole sana kwa wakati mgumu uliopitia
Ni kweli mnapitia magumu sana lakini je,unakua uchungu wa kupigwa teke la korodani!?Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.
kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.
Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee[emoji23][emoji23][emoji23] mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.
Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata
Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
mada ya cku nying , hakuna dawa inaitwa hvo, kuna mahali panaitwa epidural space kwenye spinal cord huwa panachomekwa sindano ya kama mama anafanyiwa operation , lakin kama mama anatakiwa kuongezewa uchungu, dawa yake inaitwa oxtocinHata nilikuwa naijua sasa
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] nimecheka sana-Kula kwa jasho na kuzaa kwa uchungu.
-Wanaume tumeumbwa mateso kuangaika.
-Mwanammke maumivu masaa kazaa lakini mwanamme jasho linamtoka 24/7 365 days.
Iwe siri kwa sababu gani wakati tukianzia O level shule mnachorewa hadi picha jinsi mwanamke anavyozaa??? Vitabu vimejaa mitaani na video za jinsi watu wanavyozaa Hiyo ni siri? Afterall wanaongelea maumivu ya labor na sio jinsi walivyozaa?Wanaozalisha wanaume, I mean, hamna wasichojua unless kuna watoto wa kindergarten hapa.
Don’t make life too serious utakufa mapema bure!
Hapana, unajua kila mtu ana namna yake ya kupunguza maumivu. Mwingine akipiga kelele anaona kupata nafuu na wengine tunapenda ukimya tu.
Mie siku zangu zilipofika, sikupiga kelele wala mayowe hata sikuinua mdomo wangu kusema neno ila nilikuwa nauma meno balaa. Na kwa kufanya vile nilikuwa naona napata nafuu
Hapana siwezi kufa mapema Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu!
Imeandikwa " Mwenye Haki wa Mungu ataishi Kwa Imani"
Haya tuje Kwenye hoja ya msingi;
Kama ni hivyo basi Hata chumbani kwa baba na mama watoto wakubwa wawe wanalala na wazazi wao kwa kuwa kinachofanyika kule wanakijua kuanzia four form wamefundishwa Kwenye somo la baiolojia? Au siyo?!
Unatafuna meno yako mwenyeweHapo mwishoni sijakusoma vizuri , ulikuwa unauma meno watu ? Yani unawang'ta?
Au ile ya kuuma meno wewe mwenyewe ktk kujikaza huku ukiugulia uchungu kimoyomoyo ?