Wanawake muolewe. Wanawake waliofanya mambo makubwa katika Biblia walikuwa ni wake za watu

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,371
Ni Ibris ndio anakudanganya eti ukiwa siglemama ndio utafanikiwa, utakuwa huru na utajitawala.

Wale ambao kama mimi wameruhusu akili zao ziathiliwe na Biblia watajua wanawake wenye ushawishi, matajiri na wanawake wa maana wenye adabu walikuwa ni wake za watu, sio Masingle mama au wanakejeli ndoa.

Mifano:

1: Mwanamke wa Kwanza kuongea na Mungu live, ambaye pia nyumbani kwake misafara ya malaika ilikuwa haikatiki ni Sarah Mke wa Ibrahim.
Ni moja ya wanawake wachachr ambao aliweza kuishi na watu zaidi ya 1000 nyumbani kwake. Wewe Shemeji mmoja tu anakushinda.

2: Mwanamke Mshurami.
Alikuwa ameolewa. Lakini alikuwa ni Kigogo wa Serikalini enzi hizo. Alikuwa tajiri tena mwenye mashamba makubwa, mwenye uwezo wa kujengea hadi wageni wake nyumba za kufikia. Alikuwa mnyenyekevu, hafanyi kitu bila kumshirikisha mumewe.

3: Debora. Alikuwa mke wa mtu. Mama mwenye adabu. Lakini alikuwa ndio kwa sasa tuseme Rais au PM wa Israel. Lakini pia alikuwa ni kama CDF wa majeshi ya Israel na Alipigana vita na Kumshinda Sisera. Lakini huna ilipoandikwa kwa mafanikio yake aliona bora awe singe mama.

4: Malkia wa Sheba. Huyu Muethiopia. Tajiri mkubwa mwenye uwezo wa kutembea popote. Alikuwa maarufu kuliko hata mumewe. Maana hata hafaamiki. Lakini hatuoni popote akiona bora awe peke yake kama malkia wa Nyuki.

5: Yoaha. Mke wa Kuza. Kuza alikuwa ni Mwanasheria wa Rais Herode. Huyu mama alikuwa yuko vizuri. Ukiona Yesu amefanya misheni yake hadi anakufa na kufufuka bila kuacha madeni ya pesa duniani. Ni huyu mama na shoga zake. Huyu ndiye alikuwa sponsor wa Yesu. Alitoa pesa zake. Licha ya kuwa na Pesa nyingi hakutamani kuachika. Wewe umepata kaPasso tu kamkopo kazini na Masters yako unasema eti wanaume wa nini?

6: Nabii Hulda. Huyu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa. Enzi zake Serikali yote ikiongozwa na Mfalme Josia ilikuja kwa unyenyekevu awadadavulie Neno. Na wakalia sana na akawapa maelekezo kimamlka. Lakini alikuwa mke wa mtu, hakujiona bora kiasi cha kupuuza ndoa.

Na wengine wengi.

Wanawake wa kisasa msijiingize kwenye mafugufugu na ubishoo wa kupuuza ndoa. Au kudhani unaweza kufanikiwa zaidi ukiwa peke yako, Au kufanikiwa kidogo unasema waume wa nini?

Jitafakari.

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom