Waziri Dorothy Gwajima ni waziri anayefanya mambo makubwa mno bila kelele,sifa za kijinga na majivuno!

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Salamu nishamuchia ndugu yangu GENTAMYCINE na ndugu zake wa Butiama & Nyamuswa, kwangu mambo yote ni shega tu bila salamu!.

Kwanza niseme mimi si mwanasiasa,naipenda siasa ila nawachukia wanasiasa baadhi wenye mambo ya ovyo na ambao wanadhani baadhi ya watanzani ni wapumbavu kwa kukubaliana na mambo yao ya kipumbavu wayafanyayo!

Kiukweli bila unafiki nampenda na namkubali sana huyu Bi Mkubwa Dorothy Gwajima kwa namna anavyopiga kazi kimya kimya lakini inayoeleweka,no kelele,no machawa,no unafiki & no kujitapa!

Dkt. Gwajima D

Ni waziri asiyekuwa na Kelele nyingi ila anafanya mambo makubwa sana ya kuisaidia jamii ya watanzania ambao wanapata matatizo mbalimbali,pia nimekuwa nikimfuatilia ni mwana mama ambaye huwa hana majivuno japo amepewa madaraka na chef kikubwa kwenye nchi yetu!.

Kuna mahali nilikwenda kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wenzangu waliokuwa na changamoto,sasa kuna mambo fulani fulani nilikwamishwa na watendaji wapuuzi wa serikali lakini hili jambo lilipomfikia Mh waziri alilitatua mara moja na mambo yakaenda sawia.

Sijawahi kuwapongeza wanasiasa kwasababu ya matendo yao maovu kwa wananchi lakini huyu mama nisipompa sifa zake muda huu nitakuwa mnafiki!

Hajikwezi,mtu wa watu,na mtatua shida za watu!

Kwakuwa wanasiasa wengi hulewa sifa ninamuomba Mungu amsaidie na amjalie hekima na maarifa ya kutatua shida za watu!,Mungu amuepushe na chuki,kibri cha madaraka na ufisadi wa baadhi ya wanasiasa!

Mh Dkt. Gwajima D wewe ni mwanamke wa shaka!
 
Na mimi namsifia anikope hata milioni nikomae nayo kitaa basi mambo magumu😐😐😐😐😐😐😐😐😐😐😐
 
Back
Top Bottom