Wanawake Malawi watishia kuandamana uchi

Mojawapo ya vitu vinanavyonikera nikuona mtu anajivika madaraka ya "ukamanda wa maadili ya mavazi stahili" katika jamii iliyokubwa au hadhara inayoshirikisha watu wa aina mbalimbali. Kama unaamua kuwa kamanda wa maadili ya mavazi stahili ndani ya nyumba yako, sawa. Kama unaamua kufanya hivyo pahali pako unapoajiri watu, sawa. Lakini siyo kujifanya maadili yako katika aina ya mavazi ndiyo bora kuliko ya mwingine, kwa visingizio vya utamaduni, siasa, dini au chochote kile unacho amini na kufata wewe, na kwamba kile uvaacho wewe ni lazima kila mtu avae hivyohivyo.

Kikubwa ambacho unaweza kusema kwa mtu usiyemjua na aliyejivalia linguo lake la ajabu ajabu ni kama - amependeza au hajapendeza, mengineyo mwachie yeye na msimamo wake!

well said SD
 
Sababu ni zile zile. Hao wanaosema hivyo wanafikiria kwamba huyo dada alikua anajionyesha, anajipitisha, anajishebedua, anataka attention hivyo aliyopata inamfaa.

Na ni kweli inashangaza na kusikitisha ila wavaa nguo ndefu (sio wote) hua wanafikiria kwamba kuvaa nguo ndefu ndio heshima/staha/tabia nzuri, hivyo akitokea anaevaa tofauti anaonekana hana tabia nzuri wala hajiheshimu hivyo hastahili kuheshimiwa kwa namna yoyote ile.

Kinachotuathiri ni ile hali ya watu kuona wao ni bora zaidi na wana haki zaidi haswa linapokuja swala la mavazi.

Na ndio hoja ya Ngabu kuwa wanawake hatupendani. Ingekuwa wanawake wote tunapigania kila mwanamke apate haki ya kuvaa atakavyo, ingekuwa ina sauti kubwa zaidi. Wanawake sisi wenyewe tunaruhusu mfumo dume kututawala na wale wachache wanaopinga mfumodume tunawakebehi na kuwadhalilisha wakati mwengine kuliko hata wanaume wanavyofanya
 
Hii bora ije na hapa tz,watanikoma wavaa suruali wa kike.kwa siku lazima niwavue kama mia na kitu hivi.
 
Na ndio hoja ya Ngabu kuwa wanawake hatupendani. Ingekuwa wanawake wote tunapigania kila mwanamke apate haki ya kuvaa atakavyo, ingekuwa ina sauti kubwa zaidi. Wanawake sisi wenyewe tunaruhusu mfumo dume kututawala na wale wachache wanaopinga mfumodume tunawakebehi na kuwadhalilisha wakati mwengine kuliko hata wanaume wanavyofanya

Bado hiyo kauli siikubali, labda kama tutaitumia kwa wanaume pia kwasababu hata wao wanakandia sana wale wanaovaa tofauti na wanavyovaa wao. Yani hii iko pande zote, hamna kundi linaloungana mkono kwa 100%. . . lazima kuwe na wapinzani ndani ya kundi. Kwahiyo hamna haja ya kulebel jinsia moja kana kwamba ndio pekee isiyo na umoja kwenye maswala kama haya.
 
Pole-lakini nadhani siku binti yako wa miaka 17 akivaa gauni linaishia kitovuni utamruhusu akate mtaa eti eeh.. Si kila mtu ana haki ya kuvaa atakavyo..!!!
 
Unategemea nimfanyeje?
 
Bado hiyo kauli siikubali, labda kama tutaitumia kwa wanaume pia kwasababu hata wao wanakandia sana wale wanaovaa tofauti na wanavyovaa wao. Yani hii iko pande zote, hamna kundi linaloungana mkono kwa 100%. . . lazima kuwe na wapinzani ndani ya kundi. Kwahiyo hamna haja ya kulebel jinsia moja kana kwamba ndio pekee isiyo na umoja kwenye maswala kama haya.

Umewahi kuona mwanaume ananyanyaswa na kudhalilishwa kijinsia (na wanawake) kama huyo mama wa Kimalawi kwenye hiyo picha hapo juu kisa mavazi?

Na hapa hatuzungumzii absolutes za asilimia 100! Lakini endapo wanawake wengine hawaoni kuwa wanawake wenzao wananyanyaswa na wanaume kuja kupata heshima stahilifu itakuwa ni ndoto!

Kuna nchi unyanyasaji na udhalilishaji wa hadharani namna hii hauvumiliwi hata kidogo! Dada hata apite na kibikini downton, midtown, au uptown, watu watakachofanya ni kukata shingo tu. Mguse uone utavyoshukiwa na mkono wa sheria! Mguse uone utavyoshukiwa na special interest groups za kutetea haki za wanawake (na watoto).

Lakini Tanzania na sehemu zingine za Afrika wala hutafanywa kitu. Sana sana utaishia kuungwa mkono na hata wanawake kwa kumdhalilisha mwanamke mwenzao. Sasa wewe kama hilo unaona ni sawa wala hamna neno. Labda siku yakikukuta ndiyo utaelewa ni nini ninachozungumzia hapa.
 
Sijui kama ni majinga au vipi, ila hapo ilikuwa Iringa

Mimi sikuona ubaya hata kidogo wa alichokivaa.
hizi tamaa za ngono kwa baadhi yetu ni za kipuuzi kweli usikute hawa jamaa walikuwa na nia mbaya kwake aidha kumuibia au kama ingekuwa usiku labda wangejaribu kumbaka! ndo maana ukimwi Iringa uko juu
 
Umewahi kuona mwanaume ananyanyaswa na kudhalilishwa kijinsia (na wanawake) kama huyo mama wa Kimalawi kwenye hiyo picha hapo juu kisa mavazi?

Na hapa hatuzungumzii absolutes za asilimia 100! Lakini endapo wanawake wengine hawaoni kuwa wanawake wenzao wananyanyaswa na wanaume kuja kupata heshima stahilifu itakuwa ni ndoto!

Kuna nchi unyanyasaji na udhalilishaji wa hadharani namna hii hauvumiliwi hata kidogo! Dada hata apite na kibikini downton, midtown, au uptown, watu watakachofanya ni kukata shingo tu. Mguse uone utavyoshukiwa na mkono wa sheria! Mguse uone utavyoshukiwa na special interest groups za kutetea haki za wanawake (na watoto).

Lakini Tanzania na sehemu zingine za Afrika wala hutafanywa kitu. Sana sana utaishia kuungwa mkono na hata wanawake kwa kumdhalilisha mwanamke mwenzao. Sasa wewe kama hilo unaona ni sawa wala hamna neno. Labda siku yakikukuta ndiyo utaelewa ni nini ninachozungumzia hapa.

We bana. . kwanzia mwanzo nimeonyesha upande niliopo, sitetei wala sifagilii walichofanya au yanayofanyika huko mitaani kwetu.

Tukiturudi kwenye hoja, sijaona wakiwa wanafanya hivyo pengine kwa kukosa ujasiri, wao hua wanatumia maneno zaidi. Tofauti na wanaume ambao wana ujasiri wa kumkamata mwanamama kama hapo juu. Mpaka hapo adui wa kwanza ni hao wanaoona wao wanajua zaidi na wa pili na hao wanaowaunga mkono. Kwa bahati mbaya haya mambo yataendelea kwasababu hao wanaounga mkono (wake kwa waume) wanafanya hivyo kwa sababu binafsi, kama ambavyo wapingaji tunafanya, bila kusahau kwamba sisi hatuna sheria zinazolinda watu na mambo kama haya.
 
Kumbe basi hakuna unachobisha lol :lol::lol::lol:
 
Kwa hiyo Beyonce might be dreaming?

Last edited by a moderator:
Lazima nitanyanyuka na "kengele" za mtu wallahi

Hutopata huo muda wala kukumbuka kushikilia hizo 'kengele' maana utakuwa umeandamwa na kundi kubwa la watu wanaokupigia kelele, miluzi, matusi mazito nk. In other words utakuwa umechanganyikiwa! Kwa mwanamke kufanyiwa hicho kitendo cha kuvuliwa nguo ni sawa na kumkata kichwa chake.
 
Back
Top Bottom