Wanawake Malawi watishia kuandamana uchi

Kuna kipindi ilikuwa mtu akikatisha Kariakoo, Dar es Salaam na miniskirt, lazima mayowe na miluzi imfuate. Kule pande ingine kikundi cha Mungiki kiliwahi kuwatoa kamasi Wadada wa aina hiyo
 
Fafanua Mkuu.

Hawa akina dada zetu wanaona ni raha kwao kuvaa visivyo mbele ya uma, hawana elimu kuwa mavazi haya huwakera watu wengine, wao wanaona ni fashion. Basi kama makasisi ambao wamepewa nafasi hiyo ya kuelimisha jamii wako kimya, watu wataanza kuchukua sheria mikononi mwao, kisa ambacho tunashuhudia malawi.
 
20 Januari 2012 13:07 Takriban watu 3,000
wamekusanyika Blantyre
nchini Malawi kupinga
mashambulio dhidi ya
wanawake wanaovaa
suruali. Baadhi ya wachuuzi wa kike
wiki hii walipigwa na
kuvuliwa nguo kwenye
mitaa ya mji mkuu,
Lilongwe, na Blantyre kwa
kutovaa mavazi ya asili. Mmoja aliyeandaa
maandamano hayo
ameiambia BBC amewasihi
wanawake kujitokeza
wakiwa wamevaa suruali na
fulana nyeupe kuonyesha kukasirishwa kwao. Rais Bingu wa Mutharika
alisema kupitia redio ya taifa
kuwa wanawake wana haki
ya kuvaa wanachotaka. Alikana taarifa kuwa
aliamuru wanawake waache
kuvaa suruali. Mpaka mwaka 1994,
wanawake kwenye nchi
hiyo ya kusini mwa Afrika
yenye misimamo mikali
walikatazwa kuvaa suruali
au sketi fupi chini ya uongozi wa kidikiteta wa Hastings
Banda. Wanaume pia walikatazwa
kuwa na nywele ndefu. Wanawake pia
wameshambuliwa kwa
kuvaa suruali katika nchi za
Kenya, Afrika Kusini na
Zimbabwe katika miaka ya
hivi karibuni. 'Kukatishwa tamaa
kutokana na hali ya
uchumi' Mwandishi wa BBC aliyopo
Blantyre Raphael Tenthani
alisema makamu wa Rais
Joyce Banda, waziri wa jinsia,
wabunge kadhaa, wahadhiri
wa chuo kikuu na wanaharakati walihudhuria
maandamano ya Ijumaa. Seodi White, mwanasheria na
mwanaharakati wa haki za
wanawake na aliyeandaa
maandamano hayo, alisema
wanawake hao hawakuvaa
mavazi yasiyo ya heshima. "Ndio Malawi ni nchi yenye
msimamo mkali. Lakini
tumekuwa tukivaa
tunavyotaka, kwa kiwango
cha heshima inayotakiwa,
ambayo ni kiwango cha watu wote duniani, kwa
miaka 18. Na hakuna
anayeweza kusimama
akasema ni kinyume na
Wamalawi, " alikiambia
kipindi cha Network Afrika cha BBC. Alisema wanawake
walikuwa wakilengwa na
vijana ambao
hawafurahishwi na hali ya
kiuchumi nchini humo. "Wachuuzi unaowaona
mitaani si watu wazima.
Hawa ni vijana, wadogo wa
kuwa hata umri wa watoto
wangu. "Wananieleza mimi kuhusu
utamaduni? Wananiambia
mimi namna ya kuvaa? "Hivi hili suala kweli ni
kuhusu utamaduni au kitu
kingine kinachohusiana na
hali ngumu ya uchumi
wanayokubaliana nayo watu
wakitafuta namna ya kutoa hasira zao? Awali, Bi Banda pia alilaumu
mashambulio hayo kutokea
kutokana na uchumi nchini
Malawi, ambapo kwa sasa
kuna upungufu mkubwa wa
mafuta na fedha za kigeni.
 
20 Januari 2012 13:07 Takriban watu 3,000
"Hivi hili suala kweli ni
kuhusu utamaduni au kitu
kingine kinachohusiana na
hali ngumu ya uchumi
wanayokubaliana nayo watu
wakitafuta namna ya kutoa hasira zao? Awali, Bi Banda pia alilaumu
mashambulio hayo kutokea
kutokana na uchumi nchini
Malawi, ambapo kwa sasa
kuna upungufu mkubwa wa
mafuta na fedha za kigeni.

Hiyo hali ngumu ya uchumi inawagusa wanaume tu? Halafu mwanamke kiongozi ndo anatoa hoja kama hiyo.....!

Kwanini hasira zao watolee wanawake na si viongozi wao??
 
Hiyo hali ngumu ya uchumi inawagusa wanaume tu? Halafu mwanamke kiongozi ndo anatoa hoja kama hiyo.....!

Kwanini hasira zao watolee wanawake na si viongozi wao??


umeona eeeh??................... ndio maana afrika haipigi hatua za maana kimaendeleo kwa kuwa na viongozi kama hao...................
 
Back
Top Bottom