Wanawake Malawi watishia kuandamana uchi

Acha weee. . . na hao wanaowavua ni marafiki zao?
Wanaume wanaopinga kama wewe ni adui za hao wanaume wanaofanya hayo?

Kila mtu anakubali/pinga mambo kuendana na uelewa wake bila kujali jinsia. Kwahiyo sioni sababu ya kutumia misemo kama hiyo, labda kama tutaitumia kwa jinsia zote.

Umekurupuka! Yaani you totally missed the point.

You should have at least tried to ask what I meant and I'd have been more than happy to explain it to you.

But since you didn't, let's just say you are right and I was wrong. How about that missy?:lol:
 
Here is the kicker....usishangae kuna idadi kubwa tu ya wanawake huko Malawi wanaounga mkono udhalilishwaji huo. Usikute wanasema hao wanaopatwa na hizo dhahma wamejitakia wao wenyewe kwa kuvaa hivyo walivyo vaa.

Kuna ukweli mwingi tu katika usemi wa adui wa mwanamke ni mwanamke!

Ngabu naikumbuka sana ile thread ya mvaa skirt ya shumivi. Walikuja wanawake hapa wakasema ni stahili yake na amejitafutia zahma lile kwa sababu ya alivyovaa.

Waafrika hatuna tabia ya kuheshima uhuru wa mtu mwengine. Wakati wote tunataka kufikiri kuwa dunia inazunguka kufuatana na matakwa yetu. Kuna watu walifikia kusema uvaaji wa yule binti unaingilia uhuru wa wanaume katika jamii.....how?
 
01.jpg

00.jpg

sasa hapa nyie mliopenda hizi picha zina ubaya gani? kama si upuuzi...mbona huyo dada amevaa vizuri tu tena amependeza? hawa wanaomzonga ni majinga ya wapi?
 
Ikija kwenye udhalilishwaji na unyanyaswaji wa kijinsia dhidi ya wanawake mimi nilitegemea (labda naively) kuwa angalau wangekuwa na mshikamano katika kupinga na kulaani kwa nguvu zote matendo kama hayo kumbe wapi bana!

Tuna safari ndefu katika kuelewa na kuheshimu uhuru wa mtu mwingine - kwamba uhuru wa mtu A unaishia pale ambapo pua ya mtu B inapoanzia.
 
sasa hapa nyie mliopenda hizi picha zina ubaya gani? kama si upuuzi...mbona huyo dada amevaa vizuri tu tena amependeza? hawa wanaomzonga ni majinga ya wapi?

Sijui kama ni majinga au vipi, ila hapo ilikuwa Iringa

Mimi sikuona ubaya hata kidogo wa alichokivaa.
 
sasa hapa nyie mliopenda hizi picha zina ubaya gani? kama si upuuzi...mbona huyo dada amevaa vizuri tu tena amependeza? hawa wanaomzonga ni majinga ya wapi?

Hakuna ubaya wowote katika alichovaa huyo dada na hakustahili kuzongwa hivyo hata kidogo.
 
Mojawapo ya vitu vinanavyonikera nikuona mtu anajivika madaraka ya "ukamanda wa maadili ya mavazi stahili" katika jamii iliyokubwa au hadhara inayoshirikisha watu wa aina mbalimbali. Kama unaamua kuwa kamanda wa maadili ya mavazi stahili ndani ya nyumba yako, sawa. Kama unaamua kufanya hivyo pahali pako unapoajiri watu, sawa. Lakini siyo kujifanya maadili yako katika aina ya mavazi ndiyo bora kuliko ya mwingine, kwa visingizio vya utamaduni, siasa, dini au chochote kile unacho amini na kufata wewe, na kwamba kile uvaacho wewe ni lazima kila mtu avae hivyohivyo.

Kikubwa ambacho unaweza kusema kwa mtu usiyemjua na aliyejivalia linguo lake la ajabu ajabu ni kama - amependeza au hajapendeza, mengineyo mwachie yeye na msimamo wake!
 
Ikija kwenye udhalilishwaji na unyanyaswaji wa kijinsia dhidi ya wanawake mimi nilitegemea (labda naively) kuwa anagalau wangekuwa na mshikamano katika kupinga na kulaani kwa nguvu zote matendo kama hayo kumbe wapi bana!

Tuna safari ndefu katika kuelewa na kuheshimu uhuru wa mtu mwingine - kwamba uhuru wa mtu A unaishia pale pua ya mtu B inapoanzia.

Natamani hata ningeijua ile thread ilipo ningeenda kuisaka nikaleta link humu, ili watu wasijifanye kuwashangaa sana hao wa Malawi. Wabongo tuna mentality karibu na hizo (kuna watu walisema wangembaka!!)
 
Majitu yanayoweweseka yaonapo mtu akiwa hajajisitili au kuvaa yatakavyo myenyewe ndiyo hayo yanayobaka vichaa waliouchi mabarabarani na kuwapatia mimba!! Mijitu inajifanya inajua nguo wakati mibabu na mibibi yao miaka 150 tu iliyopita ilikuwa inatembea uchi au ikiwa imejisitili na magamba ya miti pekee!!!
 
https://www.jamiiforums.com/jamii-p...i-msiingie-uhuru-wetu-wa-kuvaa-tutakavyo.html

Ushahidi kamili. Na cha ksuhangaza hadi wale unaoweza kusema wanaonekana na hulka njema humu, walilalia kuwa ni haki kwa aliyotendewa huyo dada!
 
Halafu unawasikia wanarejea maadili na utamaduni wa Mwafrika!

Najuta sijui kwa nini sikuzaliwa kule kwa Mswati...kule ni boobies galore 😛oa
 
Umekurupuka! Yaani you totally missed the point.

You should have at least tried to ask what I meant and I'd have been more than happy to explain it to you.

But since you didn't, let's just say you are right and I was wrong. How about that missy?:lol:

Ushindi wa mezani SITAKI.

Nwy kikubwa nilichokua napinga ni sentesi yako ya mwisho inayosema kwamba usemi wa 'adui wa mwanamke ni mwanamke' una ukweli mwingi ndani yake. Ingekua hivyo kusingekua na kesi kama hizi za wanaume kudhalilisha na kuonea wanawake, wanawake ndo wangekua wanawavua wanawake wenzao.
 
Haya sawa. Ila naona kama hatujaelewana vizuri.
 
https://www.jamiiforums.com/jamii-p...i-msiingie-uhuru-wetu-wa-kuvaa-tutakavyo.html

Ushahidi kamili. Na cha ksuhangaza hadi wale unaoweza kusema wanaonekana na hulka njema humu, walilalia kuwa ni haki kwa aliyotendewa huyo dada!

Hulka nzuri yao iko kwenye kujifunika.

Binafsi sikuwahi kuchangia hiyo thread ila naona watu wengi waliona kama huyo dada alipata stahiki yake.

Ukweli ni kwamba baadhi ya wanaume wa kiAfrika wanaongoza kwa kuendekeza tamaa zao ndio maana wanasumbuka na vitu kama hivyo. Yani yeye akishamwona mwanamke kavalia suruali/kasketi kake basi akili yake inaenda kwingine, tayari anahisi/fikiria huyo mwanamke kamvalia yeye vile, anajipitisha, anajionyesha, sasa ukute kajichokea na maisha ndo hapo matatizo yanapoanzia.
 
Kilichotushangaza sio tabia ya baadhi ya wanaume wa Kiafrika, bali tabia ya wanawake wa Kitanzania. Waliosema ni halali yake kilichompata kwa sababu alijitafutia balaa hilo
 
Mbona wamemvua nguo zote tayari? Au suruali wanazovaa wanawake wa Wamalawi ni Overall?

Mkuu hao wamachinga wana lao jambo,ubakaji unaweza kujificha nyuma ya hili.A true Man should handle himself regardless of whatever attire a woman has put on..All the excuses are lame and irrelevant to their actions.
 
Kilichotushangaza sio tabia ya baadhi ya wanaume wa Kiafrika, bali tabia ya wanawake wa Kitanzania. Waliosema ni halali yake kilichompata kwa sababu alijitafutia balaa hilo
Sababu ni zile zile. Hao wanaosema hivyo wanafikiria kwamba huyo dada alikua anajionyesha, anajipitisha, anajishebedua, anataka attention hivyo aliyopata inamfaa.

Na ni kweli inashangaza na kusikitisha ila wavaa nguo ndefu (sio wote) hua wanafikiria kwamba kuvaa nguo ndefu ndio heshima/staha/tabia nzuri, hivyo akitokea anaevaa tofauti anaonekana hana tabia nzuri wala hajiheshimu hivyo hastahili kuheshimiwa kwa namna yoyote ile.

Kinachotuathiri ni ile hali ya watu kuona wao ni bora zaidi na wana haki zaidi haswa linapokuja swala la mavazi.
 
Back
Top Bottom