Wanawake Malawi watishia kuandamana uchi

Wanawake Malawi watishia kuandamana uchi

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Wanawake nchini Malawi wametishia kuandamana uchi kama "wamachinga" wa huko wataendelea kuwanyanyasa kisa kuvaa suruali, miniskirts na leggings. Bado haijajulikana ni kwa nini hasa Wamachinga hao wanawavua wanawake nguo lakini inasemekana kuwa wanapinga kuondolewa kwenye mitaa wanayofanyia biashara zao.

Lakini wengine wanadai wamachinga hao wanawavua nguo wanawake kwa sababu kuvaa suruali, mini-skirts na leggings kunadhalilisha wanaume. Pia wapo wanaodai wanafanya hivyo kupinga utawala mbaya wa Rais Bingu wa Mutharika. Wanadai kwa vile utawala wa Mutharika umepiga marufuku maandamano ya amani hawana jinsi ya ku-express jinsi utawala wake ulivyo mbovu zaidi ya kuwavua wanawake nguo.

Hadi mwaka 1996 ilikuwa marufuku kwa mwanamke kuvaa suruali nchini Malawi. Baadhi ya wanawake wamevuliwa nguo na hao wamachinga. Pichani mmoja ya wanawake ambaye alivuliwa suruali kwenye hiyo kampeni ya wamachinga inayoitwa "anti-trouser and mini-skirt campaign to ladies"

383942_221249971294174_100002275195268_500052_1830283998_n.jpg
 
Wanawake nchini Malawi wametishia kuandamana uchi kama "wamachinga" wa huko wataendelea kuwanyanyasa kisa kuvaa suruali, miniskirts na leggings. Bado haijajulikana ni kwa nini hasa Wamachinga hao wanawavua wanawake nguo lakini inasemekana kuwa wanapinga kuondolewa kwenye mitaa wanayofanyia biashara zao.

Lakini wengine wanadai wamachinga hao wanawavua nguo wanawake kwa sababu kuvaa suruali, mini-skirts na leggings kunadhalilisha wanaume. Pia wapo wanaodai wanafanya hivyo kupinga utawala mbaya Rais Bingu wa Mutharika. Wanadai kwa vile utawala wa Mutharika umepiga marufuku maandamano ya amani hawana jinsi ya ku-express utawala wake mbovu zaidi ya kuwavua wanawake nguo.

Hadi mwaka 1996 ilikuwa marufuku kwa mwanamke kuvaa suruali nchini Malawi. Baadhi ya wanawake wamevuliwa nguo na hao wamachinga. Pichani mmoja ya wanawake ambaye alivuliwa suruali kwenye hiyo kampeni ya wamachinga inayoitwa "anti-trouser and mini-skirt campaign to ladies"

383942_221249971294174_100002275195268_500052_1830283998_n.jpg

mama yangu

huyu askari wame mkamuzu banda nini?

safi sana,kwasababu kila nguo wavaazo ooh wadhalilisha wanaume,sasa bola watembee uchi ilimfurahi
 
mama yangu

huyu askari wame mkamuzu banda nini?

safi sana,kwasababu kila nguo wavaazo ooh wadhalilisha wanaume,sasa bola watembee uchi ilimfurahi

Hueleweki.
 
mama yangu

huyu askari wame mkamuzu banda nini?

safi sana,kwasababu kila nguo wavaazo ooh wadhalilisha wanaume,sasa bola watembee uchi ilimfurahi

Wewe nguo ya mwanamke inakudhalilisha vipi?

Hao waMalawi wapumbavu kweli, sasa kama hawaridhi na na utawala walio nao ndio wazalilishe wanawake wao? Vichwa maji kweli.
 
sipati picha wa TZ wakiiga hiyo lol

Haya yananikumbusha picha ya mdada mmoja huko Iringa aliyevaa sketi yenye kufanana na shumizi halafu akaenda mjini na kuishia kuzongwa na kundi la wahuni waliotumia kisingizio cha utamaduni kumnyanyasa kijinsia mdada wa watu.

Nyambaf zao hao mamburukenge!
 
hawa jamaa tatizo walibanwa sana na Banda,sasa haya ndio matunda ya uhuru ?maana kipindi cha Banda mwanamke wa malawi alikua na guvu ile mbaya,akikushitaki umemkonyeza tu haukuhitajika ushahidi zaidi ya maneno yake,banda aliwapenda sana kina mama japo hakua na "madhara" yeyote kwao...
 
dah.....ushamba mzigo....

tupeleke tv kwa ndugu zetu wa vijijini kwa kweli
 
Here is the kicker....usishangae kuna idadi kubwa tu ya wanawake huko Malawi wanaounga mkono udhalilishwaji huo. Usikute wanasema hao wanaopatwa na hizo dhahma wamejitakia wao wenyewe kwa kuvaa hivyo walivyo vaa.

Kuna ukweli mwingi tu katika usemi wa adui wa mwanamke ni mwanamke!
 
Acha weee. . . na hao wanaowavua ni marafiki zao?
Wanaume wanaopinga kama wewe ni adui za hao wanaume wanaofanya hayo?

Kila mtu anakubali/pinga mambo kuendana na uelewa wake bila kujali jinsia. Kwahiyo sioni sababu ya kutumia misemo kama hiyo, labda kama tutaitumia kwa jinsia zote.
 
Back
Top Bottom