Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 62,599
- 112,334
Hoja yako usiiweke kidunia wewe bado haujatembea na ukitembea utaona tofauti kubwa tu.Ngoja niwasanue wanaume wenzangu leo.
Hakikisha hauingii kwenye mahusiano kama unajua fika kuwa hauna "the upper hand", yaani kama hauna maokoto usidiriki kuchase mwanamke.
Tunaishi katika jamii ambayo survival ime base kwenye hela.. Yaani mwanamke hawezi kuishi na mwanaume mwenye hali ya wastani.
Dunia ya leo yenye shinny objects za kutosha, sahau kabisa kupata mwanamke atakaye vumilia ki IST chako na huku kuna wanaume wengine wanampigia miruzi na wana drive Range rover...
Achana na wanawake broo, tafuta intimacy kwenye purpose yako. Trust me that's one of the most intimate thing you can have as a human being.... Hakuna stability unayo weza kuipata kutoka kwa mwanamke kwa miaka hii, ambayo wanawake wana comparison Mchungu mzima, utaishiabkuimpress mtu asiye ridhika tu...
Kuna mzee mmoja alifiwa na mkewe, akaamua aoe millenia single mother ambaye alikuwa na mtoto nje, aisee yule mzee alikuwa ana mpa zawadi lukuki yule mwanamke, ila alipenda vikubwa zaid ya uwezo wa mwanaume, na mwanaume alikuwa wanazidi kupanda dau, utafikiri amerogwa.. Alikuwa ananunua katoni za nguo, vyakula vya kila aina, yule mwanamke alipenda kupata degree, na mzee akagharamikiabkila kitu, wakati yule mwanamke alikuwa ana kazi, yake.
Yaani baada ya yote hayo, bado nyumba ilikuwa haina utulivu, kila day vihoja, sisi kama majirani ilikuwa week ikipita bila kuitwa mkasuruhishe mgogoro, nasema ni kama miujiza.
Ndugu yangu mwanaume, zama zimebadilika, jali afya yako ya akili na mustakabali wa maisha yako binafsi, na watoto wako kama unao.. Achana na wanawake ndugu, utaishia kuchizika tu.
Nakumbuka familia kipindi tunakuwa, ilikuwa hata kama kuna ugomvi baina ya wanandoa hautakuja skia, ilikuwa wanayamaliza, upendo wa kweli na amani vikitawala. Wanawake hawakuwa malimbukeni wa mali, wali chukua ndoa kama kitengo nyeti ambacho no amount of money could ever buy it. Walijua kuwa familia ndo msingi bora wa jamii na koo iliyo imara... Ila leo people don't give a damn about family. Ndo maana unaona jamii ya watoto hasa wale wanafunzi walio trend wakisema wanawake walinde mabwana zao...
Ni hayo, tu ndugu zangu...
Mimi sio mgeni, jf nimekuwa humu toka kitambo. Nawatakia jpili njema na yenye baraka.
Tatizo la Tanzania siyo mapenzi bali ni umaskini ndio chanzo cha kuhisi upendo hakuna.
Vijana wengi wa kike na wa kiume hawana ajira wala biashara yoyote sasa mwanaume ndio anageuzwa kama fursa yake kiuchumi.
Katika nchi nilizotembea haya mambo huwezi kuyakuta kwa sababu wasichana wakiwa shule ni jukumu la wazazi na wakimaliza shule wanapata ajira mtoto mdogo lakini ana kipato chake halali, kazi ya mpenzi ni kumnunulia zawadi na siyo kutegemea kuhongwa pesa, pesa zinapatikana kwa kufanyakazi.
Mfano majirani tu nimeona Dubai mademu wa Kikenya ndio wanaowatumia pocket money mabwana zao waliowaacha Kenya.
Tukienda kimagharibi kwenye bill za nyumba lazima kuwe na makubaliano mume atacover bill zipi na mke atacover bill zipi hilo mimi nimeliadot mpaka Bongo sina mke goigoi, ana bill zake na nina bill zangu maisha yanakwenda fair play.