Hapo umeweka na Walatino?
Maana Michael Jordan na Shaq wao wana Walatino ati.
Akina dada lazima mfahamu jambo moja, wengi wa hawa wanadai wana Wazungu wanaume, huwa wanachoropoka mara moja moja na kupata Gwaride la Mpingo. Na hasa waliokuwa mabwana zao kabla hawajakutana na huyo Mudhungu.
Kwa sisi akina Kaka weusi, wengi huwa wanakimbilia Wadhungu kutokana na sehemu wanayoishi. Tuseme unaishi kule juu Sweden, kule Weusi wachache na utajikuta unaishia kuchukua Mama Yeyo wa Kiswidi ukame ukizidi. Mwanzo unaona kama ni kujiokoa tu na baridi kali ya Sweden/Norway ila siku zinavyozidi kuongezeka, unajikuta una mtoto/watoto na maisha yanakwenda. Mwisho unamzoea huyo Mamaa na unajikuta bila yeye, maisha hayaendi.
Sasa utamuachaje huyo mamaa na watoto wako/mtoto wako ambao ni damu yako mwenyewe? Kisa tu WIFI zake akina KAUNGA watakushambulia eti umewaletea Zeruzeru pale nyumbani Sikonge Usupilo.
Dunia sasa hivi inaungana, utake usitake itakuwa hivyo. Kuna wanakaofanya muungano huo kwa mapenzi. Kuna watakaofanya kwa kuona tu "ngoja wanione na mie nina MUDHUNGU" na kuna watakaofanya kwa bahati mbaya yaani Hit and Run.
Ila kwa sisi Wanyamwezi/Wasukuma, tuna kaugonjwa sana kwa NGOZI NYEUPE. Hata kwenye Mahali basi Ng'ombe huwa wanaongezeka kutokana na weupe wa Mamaa. Sasa ukipata sehemu Mwaarabu au Mudhungu na tena hulipi hata senti tano, lohhh, KATAVI(Shetani) akupe nini tena?
Wanyamwezi hadi tuna wimbo "toka ndani wakuone ulivyopendeza Mama Kaunga......."
Kaunga hebu malizia, hehehee...