Wanaume wenye Tabia hii mbaya na inayoharibu Mahusiano yenu na inayowakera 99% ya Wanawake badilikeni tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,252
110,836
Yaani kabisa Mwanamke wako ( Mtoto wa Watu ) umempenda Mwenyewe na kuamua kuwa nae lakini cha Kushangaza uko nae Kwako Dar es Salaam ila Maelekezo yote ya Kuishi na Mkeo au Mpenzi wako ( Mchumba ) yanatoka Kijijini ( Mkoani ) aliko Mama yako Mzazi au Mlezi wako. Huu ni Ujinga wa Kiwango cha Kimataifa achaneni nao tafadhali.

Mama zetu mliotuzaa na Mama Walezi wote tunawapenda sana na tunajua kuwa bila nyie Leo hii dunia tusingeiona ila nasi Watoto wenu wa Kiume tunawaomba acheni Kutuingilia katika Ndoa na Mahusiano yetu kwa Kutupangia kila Kitu na kututisha kuwa kama tusipowasikiliza basi mtatuachia Radhi. Hakina mnachangia mno Kuharibu Ndoa na Mahusiano ya Watoto wenu wa Kiume.

Pongezi nyingi ziende kwa Wababa ambao Wao huwa wala hawatuingilii Watoto wao wa Kiume katika Mahusiano yetu yawe ya Ndoa au ya Kiuchumba na hata yale ya Kirafiki. Tena Wababa wengine kwa Kutupenda Watoto wao wa Kiume hutupa hadi na Maujanja ya Kubandua vyema ili Wakwe zao wasije Kubanduliwa kunakotukuka na Masela wengine.

Haiwezekani Mama Mzazi utake Kumpangia kila Kitu Mwanao wa Kiume ipo Siku utampangia hadi Bao za Kubandua!!!!
 
Back
Top Bottom