Ukweli ni mchungu na asiyeubali ni mtumwa wa fikira. Wanawake na Wanaume hili mnalijua?

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
Kwanza kabisa niwape pole wale wanaopitia changamoto za mahusiano. Poleni sana Ila wakati mwingine poleni kwa kujitakia.

Tatizo watu wengi hutengeza tatizo na baadaye mnakimbilia JF kuomba huruma. Leo tuambizane ukweli ulio mchungu, wanawake 90% hawateswi na waume zao bali wanatengeneza mazingira ya wao wenyewe kujitesa. Wanaoteseka ni wale walioolewa kwa sababu za kimaisha na matamanio ( mume mwenye mali, six pack, mrefu, mweupe, handsome nk).

Kuna maneno ya "kijinga" ambayo baadhi wanawake "wasioridhiki" (uwepo wao hapa duniani ni sifuri yani walizaliwa bahati mbaya);huyatumia kuwaaminisha wanawake wote duniani kuwa " wanaume wote ni walewale, wametoka kwa mama mmoja). Mara "wanaume wote ni mbwa" ( hapo kamjumlisha na baba yake). Kwa maneno hayo tu wanayoropoka vinywani mwao tayari ni mateso kwa kichwa na ubongo wao.

Wanawake jua kuwa ukweli ni mchungu na leo mezeni hii pilitoni ili muweze kujirekebisha. Ukweli ni kuwa mara nyingi ukiona mwanaume ndani ya nyumba kabadilika jua kuna sehem wewe km mwanamke umekosea. Km mnavyoimba na kuvimba kila siku eti "kila mwanaume mwenye maendeleo nyuma yake kuna mwanamke". Hivyohivyo na leo muelewe kuwa "kila mabadiliko ya tabia ya mwanaume ndani ya nyumba nyuma kuna ujinga wa mwanamke".
Pia kuna baadhi ya wanaume wanadai kuteseka ktk ndoa/mahusiano. Baadhi ya wanaume wanaoteseka ni wale waliooa kwa sababu za "kijinga" (ana tako kubwa, ni mrembo/mzuri, mrefu, mweupe, wakimuona washikaji wanisifie, ana hips, ananywele za kiarabu("shenzi type), ana miguu ya bia, nk). Wanaume wenye sababu/vigezo hivi ndiyo wengi wao huzaa watoto "tahira" (watoto wenye udumavu wa akili), vibaka, changudoa, nk. Hii inatokana na wazazi badala ya kuhangaika ktk kujenga maadili mema ya watoto wao wanahangaika na kukuza six pack, kujingalia makalio km bado yapo asije kuachika, kuhangaika na saloon, nk. Sasa kwa mfano mwanaume unahangaika na "matako" ya mwanamke yakusaudie nini au ndiyo nyie huwa mnaenda kwa "mparange!" Unakuta kijana kasoma vizuri lakini kuja kuoa anatafuta vigezo vya kijinga ambayo hata "gumbaru" hana muda navyo.

"Men and women consider petty criteria when they want to get married". Ndiyo maana ndoa/mahusiano mengi huangukia pua. Wanaume/wanawake jirekebisheni ndoa siyo maonesho, ndoa ni tasisi inayojengwa na akili zilizotulia siyo six pack, pesa, hips, matako makubwa, weupe, urefu, nk.

Mlishajiuliza kwa nini ndoa nyingi za watu masikini hudumu kuliko matajiri au wasomi. Ni kwa sababu watu masikini hawajali vigezo vya kijinga nilivyoorodhesha hapo juu.

Mwisho: Ukiona mwanaume anachepuka jua kuna mahali mwanamke umekosea na ukimuona mwanamke anachepuka basi mwanaume jua kuna mahali umechemka.
 
Karibuni Moshi leo kumepambazuka namna hii

 
Pole sana kwa kupigwa tukio, huna haja ya makasiriko juu ya wanawake, simama upya, tafuta hela, enjoy life kabla hujafa.
 
Karibuni Moshi leo kumepambazuka namna hii

Guten morgen Bruder
 
Back
Top Bottom