Wanaume wajiandae kwa usawa mkubwa zaidi na wanawake wenye nguvu badala ya kulalamika

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,277
Nimemsikia mmojawapo wa wachungaji wa KKKT akilalamika na kusikitika kuhusu wanawake wengi zaidi kuzidi kuimarika kiuchumi kiasi cha wanaume kushindwa kuwamudu. Ameenda mbali zaidi akiwataka waumini wake wanaume kwa wanawake kukemea roho hiyo ya aliyoiita ya Yezebel!

Huko Kenya mke wa makamu wa Rais ni mwanaharakati wa utetezi wa wanaume! Pia kumeibuka harakati kubwa za kinachoitwa kumpambania "boy child" kutoka kwa wanaharakati mbalimbali. Wapo pia wanaopiga kelele za kuongezeka kwa single mothers wakilaani na kulaumu mmomonyoko wa maadili wa wanawake kama chanzo kimojawapo.

Kinachokosekana kwa wengi wa wachungaji hawa wanaharakati wa boy child na raia wengine wengi kuhusu suala la usawa wa kijinsia kuzidi kuimarika na wanawake kuzidi kufanikiwa ni ukosefu wa maarifa ya kihistoria na evolution.

Kwa ufupi ni kwamba katika kipindi kirefu cha historia ya mwanadamu mafanikio makubwa ya kiuchumi, uongozi na jamii yalitegemea nguvu za misuli zaidi na aggressiveness ya mtu ila kadri muda ulivyoendelea mafanikio ya binadamu yamezidi kuegemea zaidi uwezo wa akili.

Pia kutokana na mambo na mazingira hayo kwa muda mrefu zaidi wanawake walikuwa wakitegema wanaume kwa ajili ya kupata mahitaji yao na hasa zaidi ya watoto wao hali iliyowafanya wakukubali kuwa chini ya dominance ya wanaume. Mazingira ya sasa yamebadilika sana na yanazidi kubadilika kutohitaji misuli na mabavu bali akili kwa ajili ya kupata mafanikio na mahitaji ya maisha na hii inapelekea mabadiliko makubwa ya usawa wa kijinsia kwa sababu binadamu wa jinsia zote wana kiwango sawa cha akili.

Wachungaji na wanaharakati wengine wa wanaume au "boy child" msihangaike kuwapigania watoto wa kiume hakuna conspiracy dhidi yao wanaume wala hakuna masuala yoyote ya kiroho, ni mabadiliko ya kimazingira na evolution inayoendelea kutokea taratibu vinavyoratibu huu usawa unaotishia nafasi ya mwanaume.
 
Mfumo wenu wa 50/50 sijawahi kuuelewa hata kidogo.

Sio kila kitu kinaenda na wakati kuna vitu vinahitaji wakati ndio uende navyo.
Kuna mfumo wa 50/50 unaozungumziwa kisiasa na kinadharia ila kuna mfumo wa 50/50 ambao ni wa kiuhalisia unaotokana au kujiunda kutokana na mabadiliko makubwa ya kimazingira katika historia ya binadamu.
 
Ebu nipe ufafanuzi wa huo mfumo wako wa 50/50 ambao unaona ni wakihalisia.
 
me na ke kushabihiana

hakuna atakaekua juu ya mwenzake

gender roles zitabadilika na zingine kutoweka kutokana na mabadiliko ya kijamii, na kiteknolojia

itafika mahali hakuna kitu me anaweza mfanyia ke, ambacho ke hawezi mfanyia me, labda kuzalisha tu

kwa mtazamo wangu ni kitu kizuri
 
Huo ndio ukweli na uhalisia, bila kujali kama ni kitu kizuri au kibaya huko ndiko ulimwengu unaelekea.
 
Watarahisishia kazi mwanaume. Kazi Ni kuweka mimba Basi anawamudu kuwahudumia na wewe pia anaakuhudumia si ndicho wanachokitaka
 
Kuna Baadhi ya Majukumu kwa hawa mama zetu inabidi tuingilie kati tu. la si Hivyo Chombo kinazama huku Mapambio yakikolezwa na Muimbishaji. No . 50/50 .at all.
 
Mfano majukumu gani?
 
Nimemsikia mmojawapo wa wachungaji wa KKKT akilalamika na kusikitika kuhusu wanawake wengi zaidi kuzidi kuimarika kiuchumi kiasi cha wanaume kushindwa kuwamudu. Ameenda mbali zaidi akiwataka waumini wake wanaume kwa wanawake kukemea roho hiyo ya aliyoiita ya Yezebel!

Huko Kenya mke wa makamu wa Rais ni mwanaharakati wa utetezi wa wanaume! Pia kumeibuka harakati kubwa za kinachoitwa kumpambania "boy child" kutoka kwa wanaharakati mbalimbali. Wapo pia wanaopiga kelele za kuongezeka kwa single mothers wakilaani na kulaumu mmomonyoko wa maadili wa wanawake kama chanzo kimojawapo.

Kinachokosekana kwa wengi wa wachungaji hawa wanaharakati wa boy child na raia wengine wengi kuhusu suala la usawa wa kijinsia kuzidi kuimarika na wanawake kuzidi kufanikiwa ni ukosefu wa maarifa ya kihistoria na evolution.

Kwa ufupi ni kwamba katika kipindi kirefu cha historia ya mwanadamu mafanikio makubwa ya kiuchumi, uongozi na jamii yalitegemea nguvu za misuli zaidi na aggressiveness ya mtu ila kadri muda ulivyoendelea mafanikio ya binadamu yamezidi kuegemea zaidi uwezo wa akili.

Pia kutokana na mambo na mazingira hayo kwa muda mrefu zaidi wanawake walikuwa wakitegema wanaume kwa ajili ya kupata mahitaji yao na hasa zaidi ya watoto wao hali iliyowafanya wakukubali kuwa chini ya dominance ya wanaume. Mazingira ya sasa yamebadilika sana na yanazidi kubadilika kutohitaji misuli na mabavu bali akili kwa ajili ya kupata mafanikio na mahitaji ya maisha na hii inapelekea mabadiliko makubwa ya usawa wa kijinsia kwa sababu binadamu wa jinsia zote wana kiwango sawa cha akili.

Wachungaji na wanaharakati wengine wa wanaume au "boy child" msihangaike kuwapigania watoto wa kiume hakuna conspiracy dhidi yao wanaume wala hakuna masuala yoyote ya kiroho, ni mabadiliko ya kimazingira na evolution inayoendelea kutokea taratibu vinavyoratibu huu usawa unaotishia nafasi ya mwanaume.

Wanachofanya wanaume ni kukaa pembeni, wanaume hawashindani tena
 
Wachungaji na wanaharakati wengine wa wanaume au "boy child" msihangaike kuwapigania watoto wa kiume hakuna conspiracy dhidi yao wanaume wala hakuna masuala yoyote ya kiroho, ni mabadiliko ya kimazingira na evolution inayoendelea kutokea taratibu vinavyoratibu huu usawa unaotishia nafasi ya mwanaume.
Mtoto wa kiume anaonekana amesahaulika tena wakati mwingine akichukuliwa kana kwamba yeye ndiye mkandamizaji, hata haki zake za mtoto anaminywa kwa hoja eti 'woman first'.

Kama watoto wa kiume wamepata watetezi ni jambo jema Sana
 
Back
Top Bottom