ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
duh aisee mshukuru sana baba yako! kila siku ubusu hata hilo kaburi lake!
aisee huu uzi hadi naona aibu hapa yaani namuomba tu mungu mwaka kesho niwe hata na room moja aisee! ukiona wanawake tunavochezea hela miaka hii? kila siku nguo mpya? kuoshwa miguu saluni ..kuogeshwa yaani kila wiki kuna mtu saluni na mashoping laki tano inaisha
bado michango ya kitchen party na sare zake na masendoff! hapo bado ndugu si unajua tulivo na huruma?
eeh MUNGU tusaidie!
sisi hatujawahi ishi kota na mimi siishi kwa wazazi Asprin nitake radhi .ila baba yetu alilipwa mafao meengi baada yakustafu hatujui hela alihonga wapi na alianza kazi akiwa na 17 yrs serikalini hahahahaahahah
kweli ndugu yangu kama miguu nitatafuta jiwe nisugue mwenyewe!yaani maisha ni kujipanga dear...kuna kesho etii? mabwana wenyewe wanatutegemea nani atajenga sasa?cheki gurumo keshamiliki zaidi ya m 500 hana chochote wanaume tunaowategemea watusitiri ndo hao kina gurumo! tutakomaje?usiendekeze hayo matumizi, yatakulemaza kabisa, kichwani una akili kwamba lazima utenge fungu fulani la saloon jmosi, sijui lacewig la namna gani, hutaendelea, mie nimepunguza sana hata michango, nachanga ile ya muhimu sana sana kwangu, bwana we usinitie aibu mie, na usitake kuanza na bangaloo anza na nyumba ya kishikaji utamalizia mdogo mdogo usijinyime sana kisa unajenga.
ahahaaaa jamani wewe?????????Baba ako alistaafu bado kikojoleo kina nguvu. Akaenda kula mafao na mashosti zako. Ponda raha kufa kwaja.
kweli ndugu yangu kama miguu nitatafuta jiwe nisugue mwenyewe!yaani maisha ni kujipanga dear...kuna kesho etii? mabwana wenyewe wanatutegemea nani atajenga sasa?cheki gurumo keshamiliki zaidi ya m 500 hana chochote wanaume tunaowategemea watusitiri ndo hao kina gurumo! tutakomaje?
baba ako alistaafu bado kikojoleo kina nguvu. Akaenda kula mafao na mashosti zako. Ponda raha kufa kwaja.
Na nyie mpunguze maudhi nyumbani , ndio maana tunakaa bar sio kwamba tunapenda, bali tunafarijika na kujiepusha na magonjwa ya Moyo. Fanyeni nyumba kuwa sehemu ya amani.
Listening to the elders does'nt mean that they are perfect but we have to listen tothem simply because they have an experience for so many mistake what they did during their teenagers life.so anapaswa kuwa somo kwetu!
kweli dear i promise from today nachange ! yaani nipe mwaka namiliki ka mjengo .. bora hata nioe kwenye kamjengo kangu akinipasua kichwa natimua! mambo ya kuumbuka hapa mjini hata konda hakupigii mluzi siwezikuna mwanaume anataka mtu asiye na kitu,kama vile wewe ambavyo hutaki asiye na kitu na wao hawataki wasio na kitu, kuna siku nilisema humu kama mwanadada unaweza kujichumia kivyako kabla hujaingia kwenye ndoa jamani chumaaa, ni kwa faida yako baadae, au ya watoto wako, hizi mambo za kusema unamfanyia nani zina wacost, jifanyie japo mwenyewe basi kwa faida yako ya baadae, mie huwa nashangaa mdada anapanga nyumba ya laki 4 kwa mwezi anaishi mwenyewe,kila aina ya bill inamhusu hapo ndani, salary laki 8 anaishije? hizi status zenu za kimjini mjini zitawa cost kabisa, mie watu walikuwa wananishangaa enzi hizo sina gari, mie naona gari kitu gani bwana, lakini sijutii maamuzi yangu ya kutokujua kununua gari mpaka msukuma alipokuja kunitoa ushamba, Lol, gari/nakaa self/ bills za kujitakia niligoma kabisa, lakini nashukuru mgomo ulinifikisha nilipo plan japo kwa kiasi fulani.
mtafute gurumonaomba kuponda raha na wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mimi naona ni dhana potofu tu hiyo. Nailinganisha na kitambi ambacho pia eti ni ishara kwamba mambo ni safi kumbe wapi!!
Kuna Mzee mmoja alikuwa jirani yetu, tulizoea kumwita Nzenganwa (jirani). Basi alikuwa na kitambi na alipendelea sana kuchomekea na kuvaa kofia kama zile za Notorious B.I.G. Basi watu walimwona mambo safi kiasi kwamba aliitwa "digala" huko usukumani ikimaanisha tajiri, enzi hizo. Guess what? Nyumba aliyokuwa akiishi ilikuwa ya kupanga...landlord akaihitaji...Nzenganwa a.k.a Digala sijui alipotelea wapi, sadly with his family...
naomba kuponda raha na wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
duh aisee mshukuru sana baba yako! kila siku ubusu hata hilo kaburi lake!
aisee huu uzi hadi naona aibu hapa yaani namuomba tu mungu mwaka kesho niwe hata na room moja aisee! ukiona wanawake tunavochezea hela miaka hii? kila siku nguo mpya? kuoshwa miguu saluni ..kuogeshwa yaani kila wiki kuna mtu saluni na mashoping laki tano inaisha
bado michango ya kitchen party na sare zake na masendoff! hapo bado ndugu si unajua tulivo na huruma?
eeh MUNGU tusaidie!
The Boss
umenikumbusha kitu,ila kwa upande mwingine kidogo!
kuna bibi mmoja hv wa kimanyema maeneo ya magomeni,alikuwa bibi yake na msusi wangu!
huyo bibi matusi yake kwa wasichana wa siku hiz ni kuwa wanafanya umalaya bila faida!
mmweneywe anakwambia ""enzi zetu sisi ukiwa ma.laya m.alaya kweli!
hizi nyumba za magomeni hizi zote ni kutokana na pesa za wanaume!siku hizi mlivyo wajinga mbnafanya u.malaya bila kuwa na akili!mna wanaume weeengi halafu hakuna faida!'"
pia waliosoma riwaya ya MIRADI BUBU YA WAZALENDO ,wanaweza kumkumbuka mhusika bi ntwara na binti yake
scenario hiz mbili zinaelezea kwa uhakika!wanaume wa miaka hiyo pesa zao zilikuwa zinaenda wapi!
Ok hizo ni kanuni za kiuchumi nazielewa vizuri sana. Mimi msingi wa maswali yangu ni kwamba hata huyo aliepata ufahamu wakielimu akajua how much to consume kulingana na income yake nae kabarikiwa akili hiyo na Mungu. Kwakuwa wapo wenye ujuzi huohuo lakini hawautumii kujipatia hayo maisha safi. Mzee Ngurumo na watu wamfano wake waliobahatika kupata neema kipindi cha ujana wao wakazichezea wao walikosa neema ya ufahamu wa kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadae. Nikiwa na maana kwamba umaskini na utajiri pia ni sehemu ya mipango ya Mungu. Mungu anajua nani atakuwa mzembe ktk utajiri alionao na mwisho ataja kuwa maskini. Sema ni siri yake Mungu kwani hakuna aliezaliwa anajua kuwa yeye atakuwa tajiri au maskini. Huwezi ukakaa tu chini ukawa na fikra kuwa utapata tu kwakuwa Mungu ndie anaejua wewe utakuwa tajiri bali mtu unapaswa kuhangaika na kujitafutia ila ikitokea umekosa pamoja na juhudi zote ulizoonyesha katika kutafuta unapaswa kuamini kuwa Mungu ndie aliepanga hayo na hapo itakusaidia pia Kumshukuru kwakila jambo la furaha au la shida. Ndio maana as a human being we do our best and God do himself the rest. Unapokuwa unasema Mungu hajui nani atakuwa maskini au tajiri manake wewe unakuwa mpingaji wa kwamba Mungu hajui mambo ya siri. Wakati yeye ndio anaejua yaliokuwa, yanayotokea sasa na yatakayotokea kesho tusioijua wewe na mimi. Cc Kibibi Jongo.
wakati naanza kabisa kazi fresh from chuo, kampuni niliyokuwa nafanyia ilikuwa inatujali sana wafanyakazi wake, mikopo nje nje, baada ya mwaka wenzangu wote nilioanza nao kazi wana magari mazuri mie bado naenda job na taxi but wanajua nimechukua mkopo mzuri tu, ilikuwa maulizo kila siku, nyamayao mkopo wako umepeleka wapi, hivi kwanini huna gari jamani, bla bla kibao, wengine mawazo yetu yalikuwa kushika viwanja kadhaa wao ilikuwa magari na masimu mazuri, kupanga ni kuchagua.
na ukipata mume wa hovyo je?
Mimi nafikiri ukipata mke wa hovyo na ukakubali kufuata uovyo wake nawe ni wa hovyo au akili zako ni za kushikiwa. Ofcourse kama couple mnahitaji kuwa na malengo mliyokubaliana na strategy mlizokubaliana.
rafiki, dont underestimate the power of a woman....never......
hawa ni wajanja tu wakiwa nje yetu..... wakiwa ndani ya 18 hawafurukuti, hata uwe smart namna gani
Mkwe wewe umeshajipanga? Ama bado upo upo? Mie sijielewi kama nishafikia pa kilujipanga ama bado!
Babu nakumbuka kukusifia hapa wewe na TIMING kwa kukiri wazi juu ya msaada wa mawazo na kubanwa na bibi. Sasa sie wanawake tuna taabu sana. Unamshauri mume hasikii, unakaba hakabiki ndo kwanza anakimbia na kulalamika humfai. Ndio maana mie na paw tumekubaliana kutofautiana baadhi ya mambo. Hata kama haamini kwenye ndoto yangu at least nataka baraka za kuota na sio kuanza kujenga nyumba kwa siri.
Kuna ndugu yangu alijenga nyumba kwa siri, mume akajua akaenda kuipiga nyundo. Wakati huo huyo mama anaishi nyumba line polisi, na mume ni mishen tauni! Mama alianza kujengewa na mwanae kwa uongo mwingi na lile limwanaume lilikufa baadae. Yaani leo tukikaa hapo kwenye nyumba yao tunasimuliwa na watoto wanarecall yale maisha! Mama asingekomaa sijui wangeishia wapi saa hizi!
Kwanza, za kuadimika?
Kwa maneno mengine, mwanaume akiharibu au akitengeneza ni sababu ya mwanamke? Akicheat au akiwa mwaminifu ni sababu ya mwanamke? yeye hana will na uwezo wa kufanya maamuzi yake mwenyewe?
wababa wengi wametawaliwa na mfumo dume, kwao kisa hela ni zao basi wanataka matumizi yao wayasimamie wenyewe. Wazzazi kama hawa huwaga wanatafuta mtu wa kumlaani baadae.
Nakumbuka baba mmoja mchaga wanae walipoona baba anaendekeza starehe na ni meneja wa sida kanda fulan walianza kuwa wakaksi wao na mama yao. Dingi kama halipi school fees kids wanabaki home, wala mama hastuuki anasema kabaisaa baba yenu awalipie.
Baba akaanza kuona maisha ya kupanga ndio bomba mama akaanza mkakati kila akirudi job, wanagombana kisaha anasaula pesa zote akiachiwa pesa ya msosi hapiki anabana dingi akirudi anaambiwa msosi hakuna pesa zimekwenda kununua site hadi akili ikamkaa sawa.
Huyu mama alihangaika hadi akaweza kununua site na kujenga tena kwa mbinde, mzee wa watu kwa ulevi sukari ikamuadabisha hajakaa sawa maini yakafeli, sasa ikaanza kuwa msala wa mama na watt lkn bora alikomaa wakapata mjengo na watt wakasoma.
Ninachoweza kusema muda mwingine mwanamke unapaswa kuwa ngangari kwa mumeo yani bora lawama kuliko fedheha. Unakaza uso kama mume haelekei.