Wanaume mamwinyi

Wanaume mamwinyi

Kakaa kuna wanaume ma mwinyi akimaluza kula anaondoka mezani Huku anakutuma upo lush viatu vyake
Hakuna umwinyi, ni kazi yako kumfanyia tena kwa upendo bila kujinyanyasa. Tena wale "stay home wives" wala wasilalamike, wafanye tu maana hakuna namna!!!
 
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
elewa hukupata mwanaume kama mimi yaani hiyo ndoa ingevunjika njiani!
Nitaendelea kupenda na kusifia watoto wa kike toka kabila langu maana hayo yote ndio majukumu ya mwanamke anaejitambua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza tujue je umeolewa?? Ni ngumu sana kulisema jambo hilo kwa ujumla wake...ndoa ni katiba/mkataba wa watu wawili me na ke jinsi watakavyoendesha mambo yao, kama ndo wamekubaliana hivyo nani wa kuingilia?? Wakati wewe unataka mwanaume afanya hayo wapo ambao mwanaume akifanya humkatalia na kumsihi aache atafanya yeye (ke) kwani ni majukumu yake.
Ndio maana hamwendelei mtabaki kununua vya watu cz hamuwazi mnawaza ujinga wenu tuu na uvivu plus hela zenyewe za mawazo...utajiitaje mwanaume we we utakuwa ni zaidi ya sugar daddy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nature mbona mkiwa kwenye mageto yenu hamfanyi hivyo !?
Huwa inaboa sana mtu anasimama anavua nguo anaacha hapo hapo.
Taulo kitandani,upo unapika anakuita kamletee glass mara kidogo kaita umtafutie charger,
Hujarudi vizuri anaulizia remote,
Ukikaa ujiandae uepue unaitwa ukawashe ac/feni.
Mpaka ifike jioni unatamani aondoke tu walau upumzike !
Uwiii ningemfukuza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na mie nikila nan aniliwaze?mtoto! hv unataka uliwazwaje kwenye kula? yaan ubembelezwe km mtoto au unatakaje? kha makubwa haya
Mnakula wote huku mnasifiana mapishi ya mezani na ya chumbani. Sasa usitenge chakula bila maji ya kunawa, utaitwa kwa nguvu na hata kusifiwa mapishi itakuwa ndoto tena
 
Mtoto bila ndoa inashindikana vipi mkuu? Sidhani km ni sahihi kuingia kwenye taasisi ambayo unatambua kabisa huiwezi. Not fair kwa mwenzako na kwako pia maana utapata stress sizizo na sababu maisha yako yote
Sasa kumzalisha mwanamke hlf namuacha ndo sitaki...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
Ndo raha ya kuwa na mke...akimaliza huduma zote akija sitting room nampakata nampozapoza kwa mahabbat anafurahi siku inapita vizuri....Sasa Sky wewe unataka 50/50 nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom