Wanaume mamwinyi

Wanaume mamwinyi

RAHA YA KUWA PAMOJA NI KAMA HIVYO...ILA SIKU UKIONDOKA NDO HAPO NDANI PATAKUWA KAMA (UWANJA WA FISI)*maana zote utakazo
 
Ni kweli remote ipo hapo karibu yako, nipo jikoni unaniita nikupe remote kama huo sio ulemavu ni nini?
Sasa kamasiioni nimuulize nani, nikimuita house girl aniletee unanikata jicho kama la mbuzi.

Alafu muache kutaja mahari nyingi, wengine utafkikama unanunua gari!!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
Umeshaanza uanaharakati.
Wanawake wengi wanaharakati walishaachika au ni masingle mamas
 
Unataka uishije na mwanaume?!!! Kama Mwanaume au kama mwanamke?!!
 
Hayo mambo tushazoea kwenye ndoa we r Tanzanian hata usomeje mwanamke lazima mumeo umhudumie kila kitu wengi tunafundishwa hvyoo Ni jambo la kawaida pia kwetu ukiona ananuna mke hajafundwa au uzungu mwingi My own brand!!
Kabisa kabisa mama, uzungu kwa kweli wavuruga ndoa nyingi Bongo, inasikitisha sana kwa kweli...
 
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.

Hata akikwambia ongeza/punguza speed ya kiuno utamuona mshenzi tu.
 
Huyo ni babaangu Baba Zurie ....amekaa karibu na friji na kabati la vyombo lakini atakuita wewe wa chumbani umuwekee maji ya kunywa. Umemuwekea chai ukasahau kijiko cha kuwekea sukari, anakiona kabatini lakini hawezi kukichukua bali atakuita umletee.

Mkewe akaamua kurahisisha maisha akaweka kikabati kidogo na friji chumbani kwao, yuko kitandani anamuita mama aliye nje aende kumpa juice. Hahahaahah...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom