Riwaya ya kipelelezi: Maiti 15 tu nitafurahi tena

gilbert35

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
247
474
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 01
SURA YA KWANZA
Zimepita takribani dakika 15 tangu awasili ndani ya ofisi yake. Ofisi ndogo tu iliyoweza kuendana na cheo chake cha uinspekta wa jeshi la polisi. Ameketi juu ya kiti, mikono yake miwili imetamalaki juu ya meza ya mbao huku juu ya mikono kukiwa na faili kubwa lenye maandishi makubwa yanayosomeka "MAUAJI KISHUMUNDU". Naam, ni faili lililobeba maelezo kuhusiana na mauaji yanayoendelea katika kijiji cha Kishumundu kilichopo wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro. Ni siku ya kumi tangu akabidhiwe kesi hii lakini hakukuwa na hatua yoyote ile ambayo ameshaipiga ingeweza kumpa mwangaza.

"Inspekta, Inspekta Jasmine, unaitwa na mkuu ofisini kwake sasa hivi" Sauti ilimkurupua na kumuondolea utulivu aliokuwa nao. Jina lake ni Jasmine Wahab. Mwanamke shupavu mwenye cheo cha uinspekta wa polisi.
Akalifunga faili lile na kuliweka juu ya meza, akanyanyuka na kuelekea hadi ilipo ofisi ya mkuu wake wa kazi.
Alipofika Ofisini kwa mkuu wake wa kazi alikaribishwa kiti kwa ishara ya mkono. Ni ishara ya mkono ilitumika kumkaribisha kitini kwa sababu mkuu wake anaongea na simu kutoka kwa kamanda wa polisi wilaya ya Moshi.

"Inspekta Jasmin, leo ni siku ya kumi tangu ukabidhiwe kesi hii lakini hujapiga hatua yoyote ile. Inamaana muuaji anakuzidi akili? Maana tangu nikukabidhi hadi sasa wameshauwawa tena watu saba na kufanya idadi kamili kutimia kumi." Bwana Elius Benjamin alizungumza bila kuweka tuo. Alikuwa akimtazama Inspekta Jasmine usoni.

Inspekta Jasmine hakujua aseme nini kwa wakati huo, kichwa chake kilikuwa kikitafakari mambo mengi kwa wakati mmoja. Moyoni alishanyanyua mikono yake juu kuashiria kwamba alikosa namna. Angesema nini Jasmine mbele ya mkuu wake? Kwamba atafutwe mtu mwingine aifanye kazi hii? Alikuwa kimya akitafakari.

"Leo mchana atafika hapa mpelelezi kutoka idara ya usalama wa taifa, utakuwa naye na pia nahitaji umpatie ushirikiano wa kutosha. Mtakuwa mnaripoti kwa kamanda mkuu wa polisi wilaya kila hatua mtakayoipiga, Sawa?" Alisema Bw Elius

"Sawa Mkuu" Inspekta Jasmine akaitikia. Akasimama, akapiga saluti na kutoka nje ya ofisi ya mkuu wake wa kazi.

"Bora hata wamepanga kuniletea wa kusaidiana naye. Hata Adam aliwekewa msaidizi kule bustanini bwana." Inspekta Jasmine alijiambia huku akitabasamu. Tumbo lake likamshtua kidogo, akaelekea mgahawa uliopo jirani na kituo cha polisi kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.

"Kama kawaida yangu. Supu ya kushiba na chapati nne. Pilipili na limao usisahau" Inspekta Jasmine alisema baada ya kuingia ndani ya mgahawa ule. Ilikuwa yapata saa nne asubuhi.

Jua lilizidi kuzidisha kero na manung'uniko kwa wakazi wa Kishumundu. Lilikuwa likiwaka litakavyo. Lakini kuhusu joto wala halikuwa kali kivile, kwa sababu mlima Kilimanjaro haukuwa mbali sana na kijiji hiki. Baridi linalocheuliwa na mlima nalo si haba. Ni mchana wa saa saba sasa katika kituo cha polisi cha Kishumundu. Gari aina ya Haier Hybrid nyeusi inafunga breki zake mbele ya jengo la kituo cha polisi. Anateremka kijana aliyevalia suti nyeusi akiwa na briefcase nyeusi. Haraka anapokelewa na kupelekwa hadi ilipo ofisi ya mkuu wa kituo.

Jina lake ni Gilbert Mwaitika, mpelelezi na askari kijana aliyedaiwa kutokea usalama wa taifa kuja kusaidiana na Inspekta Jasmine. Anafanikiwa kuonana na mkuu wa kituo cha polisi Kishumundu, wanateta pamoja kwa dakika sita kabla ya mkuu kuagiza kuitwa kwa Inspekta Jasmine.

Inspekta Jasmine haraka anatii wito na baada ya muda mchache watu watatu wanaizunguka meza na kuteta pamoja. Gilbert Mwaitika, Inspekta Jasmine pamoja na mkuu wa kituo, bw Elius Benjamin wanajadiliana pamoja kwa dakika takribani kumi na tano kisha Mkuu anawaruhusu kuondoka tayari kwa kuanza uchunguzi wao.

Ilikuwa ni saa kumi na nusu jioni Gilbert Mwaitika akiwa pamoja na Inspekta Jasmine ndani ya Tulizo Restaurant wakipata chakula.

"Lile faili la mauaji haya si lipo kwako?" Akauliza Gilbert Mwaitika wakati wanakula.

"Yeah, lipo ofisini kwangu." Akajibu Inspekta Jasmine.

"Utanipatia hilo pamoja na magazeti yote ambayo yamehawi kuandika habari kuhusiana na mauaji haya. Halafu kesho asubuhi tutapata pa kuanzia" Gilbert Mwaitika akasema huku akijipangusa mikono yake kwa tishu. Akagida juisi yake kisha akaegemea kiti chake kutazama juu akionesha kumsubiri Inspekta Jasmine amalize kula waondoke.

Baadae wakaagana. Ni baada ya Inspekta Jasmine kumkabidhi Gilbert Mwaitika vitu vyote alivyohitaji. Gilbert Mwaitika alikuwa amepewa nyumba nzuri ya kuishi iliyopo jirani kabisa na kituo. Inspekta Jasmine yeye alikuwa akiishi nyumbani kwake, umbali wa kilomita moja na nusu kutoka kituo cha polisi.

Gilbert Mwaitika alifungua mlango baada ya kufika, akaweka briefcase lake mezani, akaelekea moja kwa moja hadi chumbani na kuvua nguo zake, akachukua taulo kubwa kutoka kwenye sanduku la nguo. Akaelekea bafuni kuoga. Baada ya dakika kadhaa akatoka bafuni na taulo lake, akaelekea hadi sebuleni na kukamata briefcase lake, akalifungua na kutoa faili pamoja na magazeti aliyopatiwa na Inspekta Jasmine. Yalikuwa ni magazeti tisa. Akayapangilia magazeti yale kuanzia la awali kuchapishwa hadi la mwisho. La awali kabisa lilionekana kuchapishwa tarehe 12 Januari. Huku gazeti la mwisho kuchapwa likionesha tarehe ya kuchapwa ni 27 Januari.

Alianza kufungua kurasa iliyoandikwa habari kwa kina kuhusiana na mauaji yale katika gazeti la tarehe 12 Januari. Baada ya kusoma habari ile akagundua waliuwawa watu wawili usiku wa tarehe 11 Januari, yaani mtu na mkewe ndio waliouwawa majira ya saa mbili usiku wakiwa wanatoka baa kuelekea nyumbani kwao. Akachukua kitabu chake cha kutunzia kumbukumbu kilichokuwa ndani ya briefcase na kuandika maelezo mafupi, akaweka kando gazeti lile na kukamata gazeti linalofuata. Gazeti hili lilichapwa tarehe 14 Januari.

Liliripoti mauaji ya mzee mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 79 mchana wa tarehe kumi na tatu nyumbani kwake. Lakini pia aligundua wale watu wawili waliouwawa awali pamoja na mzee huyo wameuwawa kwa kupigwa mshale wenye sumu. Yaani ilionekana muuaji alikuwa akiua kwa mtindo wa kizamani, na kwa staili moja tu ya kutumia mshale. Na kweli hata alipolipitia gazeti la tatu hadi la tisa yote yalionesha waliouwawa wote walipigwa kwa mshale shingoni ama kifuani, na mshale huo ulikuwa na sumu kali iliyoweza kuushambulia mfumo wa damu kwa haraka sana.

"Waliouwawa ni wanaume sita na wanawake wanne. Kati ya wanaume sita, mzee ni mmoja tu, huku wanawake wanne pia mzee ni mmoja tu. Kumi waliouwawa ni wanne tu wenye undugu wa damu. Kwanini Muuaji anatumia mshale wenye sumu wakati kuna silaha nyingi tu kwa sasa katika ulimwengu huu wa kitekinolojia? Lazima kuwe na sababu. Katika ulimwengu wa kipelelezi kila kitu lazima kiwe na sababu." Gilbert Mwaitika alikuwa akiwaza huku akichora na kuandikaandika kwenye kile kitabu chake kidogo. Akalikamata na faili alilopewa pia. Hili hakulisoma kwa kina kama alivyofanya kwenye yale magazeti. Alilipitia tu juujuu na kisha kulifunga.

" Muuaji ni mwanamke bila shaka. Ni lazima awe mwanamke" Gilbert Mwaitika akawaza huku akitabasamu.
Akaandika pia kwenye kitabu chake kisha akakusanya kila kitu na kuhifandhi ndani ya briefcase. Akatazama saa ya ukutani na kugundua ilishatimu saa nne usiku. Akapeleka briefcase lile chumbani na kulihifadhi chini ya uvungu wa kitanda. Akakamata simu yake na kufungua uwanda wa ujumbe mfupi.

'Kesho saa mbili asubuhi tukutane palepale mgahawani. Nina jambo' alichakata ujumbe mfupi na kuutuma kwa Inspekta Jasmine. Akazima taa ya chumbani na kisha kupanda kitandani, akavuta shuka tayari kwa kuusaka usingizi. Lakini kabla ya kujifunika vizuri simu yake ikawaka mwangaza kwenye kioo na kisha mlio mfupi ukafuatia.

'Sawa, usiku mzuri kwako' aliona ujumbe mfupi uliotoka kwa Inspekta Jasmine. Akatabasamu na kisha kuiweka simu pembeni. Akalala.

Sauti ya jogoo ilisikika kwa mbali, baadaye kukafwatiwa na sauti za ndege wa angani. Ni siku nyingine kwa Gilbert na wanakishumundu. Gilbert Mwaitika aliyafumbua macho yake taratibu na kisha kujinyoosha akiwa bado amelala. Sauti ya chaga ikasikika ikionekana kukereka kutokana na kitendo cha Gilbert kujinyoosha angali amelala bado. Bila shaka kitanda hiki kilionekana kuwa chakavu ama hakijakazwa nati zake vizuri.

Gilbert Mwaitika hakujali sana, aliamka na kuvalia traksuti nyeusi ya mazoezi na kuelekea nje. Ilikuwa ni desturi yake kila asubuhi kuamka na kupiga mazoezi ya kukimbia ili kuimarisha viungo vya mwili. Alikimbia hadi katika shule ya msingi Kishumundu, akauzunguka uwanja wa shule ile mara mbili na kisha kuanza safari ya kurejea katika ile nyumba aliyolala usiku. Akiwa njiani akakumbuka kwenye magazeti aliyoyapitia jana usiku, gazeti la saba liliripoti mauaji ya mwalimu wa shule ya msingi Kishumundu palepale shuleni. Ilikuwa ni asubuhi wanafunzi na walimu walipoenda shuleni na kumkuta mwalimu huyo amefariki akiwa nje ya mlango wa bafu kwani ilionesha mwalimu huyo alikuwa akielekea bafuni majira ya usiku kwani alikuwa ikiishi shuleni pale.

Gilbert Mwaitika alikuwa akikumbuka wakati anarejea katika nyumba aliyopewa. Alifika na kuingia bafuni kujiandaa tayari kwa kuingia kibaruani. Ndani ya muda mfupi alikuwa tayari ndani ya suti safi ya kijivu, akajihakikisha yupo vyema, akakamata briefcase lake na kuelekea hadi Tulizo restaurant alipopanga kukutana na Inspekta Jasmine saa mbili asubuhi.

Saa mbili ikawakuta pamoja wakipata supu safi ya Ng'ombe ndani ya Tulizo restaurant. Wakipata supu Gilbert akaanzisha mazungumzo.

"Inspekta Jasmine" Gilbert Mwaitika aliita

"Abee" Inspekta Jasmine aliitikia kwa adabu

"Muuaji wa watu wote kumi waliouwawa ni mwanamke bila shaka" Gilbert Mwaitika akasema na kisha kupangusa mafuta kwenye lipsi ya mdomo kwa kutumia tishu iliyokuwa pembeni ya sahani aliyowekewa bakuli la supu.

"Mmmh! Inawezekanaje? Umejuaje Gilbert?" Inspekta Jasmine akaachia mguno na kuachia maswali mawili mfululizo. Alishangaa kivipi muuaji akawa mwanamke.

"Ni hivi, Muuaji anaonekana kutumia mshale wakati wa shambulio. Na sote tunajua sio mara zote mshale unaweza kuondoa uhai wa mtu, ni mara chache haswa unapopiga sehemu ambazo ni dhaifu kama kifuani, kooni au mara chache tumboni. Sasa muuaji anatumia mshale ambao tayari ameupakaa sumu ili iwe rahisi kwa mlengwaji kufa haraka, ikimaanisha kwamba mtu huyu anaonekana ni dhaifu kimwili na ni mwoga pia ndiyo maana anaona atumie mshale wenye sumu kwani bila kuuwekea sumu hawezi kumfwata mpinzani wake na kummalizia kama hatofanikiwa kumuua kwa mshale huo."

"Bado sijakupata vizuri. Kwahiyo muuaji ametumia njia hii kwa sababu anaonekana ni dhaifu? Sasa kwanini awe mwanamke wakati hata mwanaume ambaye ni kilema anaweza kuwa dhaifu?" Inspekta Jasmine akauliza tena

RIWAYA HII INAUZWA KWA TSHS 2,000/= TU YA KITANZANIA.
KAMA UTAIHITAJI HADI MWISHO FANYA MALIPO KWENDA M PESA NAMBA 0765824715 AU HALOPESA NAMBA 0621249611 KISHA NJOO WHATSAPP AU INBOX HAPAHAPA FB UWEZE KUIPATA.
PIA UNAWEZA KUWASILIANA NASI KWA NJIA YA EMAIL mushigilbert28@gmail.com

Ahsanteni..

FB_IMG_1697127513680.jpg
 
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 03

Wakati huohuo Inspekta Jasmine pamoja na Gilbert Mwaitika walikuwa wakisogea karibu na pale alipo Bi Sandra.

"Inspekta Jasmine kile nini pale?" Gilbert aliuliza.

"Kama mtu kalala pale, halafu mbona kama ule ni mkokoteni wa Bi Sandra?" Inspekta Jasmine alisema huku akiongeza mwendo. Mapigo yake ya moyo yalianza kudunda kwa kasi kuashiria kulikuwa na hatari. Gilbert naye hivyohivyo, mikono yao ikaelekea viunoni mwao ikijitahidi kupapasa kitu, na kitu hicho kilikuwepo.
Walichomoa bastola zao kutoka viunoni mwao, zikakokiwa tayari kwa kukabiliana na adha yoyote itakayojitokeza mbele yao.
Walifika pale na kukuta mwili wa bi Sandra umeanza kuvimba kutokana na sumu ya mshale ule. Kwa mara nyingine tena walipishana na muuaji ambaye bado hafahamiki ni nani na kwanini anaua.
Inspekta Jasmine aliiona simu ya mkononi pembeni kidogo ya mwili wa bi Sandra. Akaiokota, lakini Gilbert Mwaitika hakuiona.
Siku ilikuwa ikiisha taratibu kwa magharibi ya jua kuzama. Gilbert Mwaitika na Inspekta Jasmine hawakuwa wamepata chochote kile. Mwili wa balozo Ruwenzori pamoja na wa Bi Sandra haukuwa na chochote chenye kuwapa faida katika uchunguzi wao. Mwili ukakabidhiwa kwa ndugu ili taratibu nyingine ziendelee. Vichwa vya hawa wapelelezi wawili vikabaki vikiuma.
'Muuaji ni nani? Kwa nini anaua?'
Yakawa ni maswali tu yasiyokuwa na majibu.

************

Ibada ya misa jumapili ndiyo ilikuwa imefikia ukingoni huku Waumini wakionekana kuanza kutawanyika ndani ya kanisa katoliki Kishumundu. Gilbert Mwaitika anaonekana ndani ya gari yake akiwa pamoja na Inspekta Jasmine. Walikuwa ni miongoni mwa waumini walioshiriki katika ibada ile. Wakaiondoa gari yao na kuelekea Tulizo Restaurant. Hupendelea Tulizo Restaurant kwa sababu ya utulivu wa pale na isitoshe ni karibu na kituo cha polisi. Kama kawaida wakapata kifungua kinywa baada ya kufika pale, wakiwa bado na mavazi yao waliyotoka nayo kanisani.

"Unayakumbuka maswali yetu mawili ambayo yanatuumiza vichwa vyetu?" Gilbert akavunja ukimya

"Naam" Inspekta Jasmine akasema huku akifungua juisi ya embe kutoka kwenye kopo kubwa. Akaimimina katika glasi moja na kumkabidhi Gilbert Mwaitika. Gilbert akaipokea na kuimiminia kinywani bila kupumzika mithili ya mtu aliyekuwa na kiu sana.

"Sasa yatupasa kukomaa na swali namba mbili kwanza. Tukishajua kwanini anaua basi ni rahisi kujua muuaji ni nani." Gilbert akaeleza.

"Tuanzie wapi?" Akauliza Inspekta Jasmine huku akifuta lipsi zake kwa kutumia tishu.
Alikuwa akifuta mafuta yaliyobakia katika lipsi zake kutokana na kunywa supu. Yeye hakunywa juisi ile, madai yake ni kwamba angekesha maliwatoni kwa siku nzima kama angesubutu kuchanganya supu na juisi ya embe kwa wakati mmoja.

"Kila kitu kinachotokea na kutendeka kina sababu. Muuaji anaua kwa sababu, wanaouwawa wanauwawa kwa sababu. Ni lazima tujue kwanini wanauwawa ndipo iwe rahisi kumjua aliye nyuma ya haya. Wameshafika watu kumi na mbili waliouwawa. Wanne kati yao wana undugu wa damu, wengine saba, watano kati yao ni majirani huku wawili wakiwa ni balozi wa mtaa na mkewe waliouwawa jana. Bila shaka muuaji anajaribu kulipa kisasi kwa watu fulani waliowahi kumtendea ubaya. Twende kwenye familia za hao ndugu wanne waliouwawa kwa mara nyingine, kuna kitu nimekihisi. Wakanyanyuka na kumwita mhudumu aweze kuchukua malipo ya supu na juisi.
Lakini katika kunyanyuka kukazuka kizaazaa. Gilbert Mwaitika alianguka chini ghafla na kupoteza fahamu.

Ilikuwa ni Saa kumi na moja jioni. Gilbert Mwaitika alirejewa na fahamu akiwa juu ya kitanda cha wagonjwa ndani ya hospitali kubwa ya Kibosho Mission. Aliyashangaa mazingira ya pale kwani hakutarajia kuwa pale.
Katika kuangaza akafanikiwa kumwona nesi aliyevalia gauni jeupe akipita. Akajaribu kumpungia mkono lakini hata mkono wake haukuwa na nguvu kama ilivyo kawaida.

"Nini kimenisibu?" alijiuliza bila kupata jibu.

"Ooh! Umeamka? Pole sana. Unahitaji muda zaidi wa kupumzika ili mwili wako uweze kurejea katika hali yake ya awali uliyoizoea." Nesi yule akasema mara baada ya kufungua mlango wa kioo na kuingia ndani ya chumba alicholazwa Gilbert.

"Kwani kimenipata nini?" Gilbert Mwaitika akamuuliza nesi. Nesi huyu alikuwa amesimama pembeni ya kitanda chake.

"Ulikunywa juisi iliyokuwa imechanganywa na sumu. Kama usingewahishwa hospitalini basi ungepoteza maisha kwani sumu hiyo ilikuwa ni kali sana." Nesi huyu akamwacha Gilbert kinywa wazi.

"Eti sumu. Kivipi?"
Halmashauri ya kichwa cha Gilbert ikaanza kuushughulisha ubongo. Analolisema nesi linamwacha kinywa wazi
Akajaribu kuvuta kumbukumbu ya mara ya mwisho ni nini kilitokea kabla ya kuwa hapa. Naam, akakumbuka mara ya mwisho alikuwa na Inspekta Jasmine Wahab ndani ya tulizo Restaurant wakipata supu baada ya kutoka kanisani. Akakumbuka pia Inspekta Jasmine alimmiminia juisi ya embe katika glasi na kumpatia. Akaipokea na kuimiminia kinywani.
Baada ya hapo je? Hakumbuki tena kilichoendelea.

"Inspekta Jasmine. Umefanya nini?" alikuwa akiwaza. Lipsi za mdomo wake zilikuwa zikichezacheza kuashiria ni hasira zilifika kunako.

Akamgeukia Nesi huku akijitahidi kuinuka angalau akae na sio kulala. Alishindwa, bado hakuwa na nguvu za kutosha. Nesi akamsaidia kumwinua aweze kuketi kama anavyotaka.

"Unaweza kuniambia ni nani aliyenileta hapa?" akamuuliza Nesi.
Kabla Nesi hajasema lolote mara mlango ukafunguliwa, anayeingia ni daktari akiongozana na mkuu wa kituo cha polisi Kishumundu Bw. Elius Benjamin akiwa na sare yake ya kazi.
Gilbert anafanyiwa baadhi ya vipimo tena na daktari yule huku akimtaka afungue kinywa chake ammulike kunako mdomoni, anahamia machoni kuyamulika, anapima mapigo yake ya moyo kisha anamgeukia bwana Elius.

"Angalau kwa sasa sio mbaya, japo anahitaji bado muda zaidi wa kupumzika." Dokta anasisitiza

"Siwezi kuendelea kulala hapa angali bado kazi yangu iliyonileta huku haijakamilika." Gilbert naye anavunja ukimya. Anachomoa dripu ya maji na kujitahidi kunyanyuka.
Maskini, anahisi kizunguzungu lakini kabla hajaanguka anashikiliwa vyema na kuketishwa juu ya kitanda.

"Sumu bado haijaisha mwilini kijana, kuwa na subira utapoteza maisha" Dokta anamsisitiza Gilbert Mwaitika.

"Ni kweli Gilbert, kwa sasa pumzika hadi hali yako itengamae. Nimeagiza vijana wangu kumtafuta Inspekta Jasmine maana tangu saa nne ulipodondoka pale mgahawani alitoweka na simu yake haipo hewani kabisa." Bwana Elius anasema kwa mara ya kwanza tangu afike pale.

"Unaamini kama yeye ndiye anayehusika na hili?" Gilbert Mwaitika anamkazia macho bwana Elius.

"Kwa asilimia chache. Kuna kitu nyuma ya pazia, Jasmine hawezi kufanya hivi. Na kama kafanya basi kuna sababu kubwa. Ni yeye pekee anayeweza kutufafanulia zaidi kuhusiana na hili lililotokea." Bwana Elius akatetea.
Haikuwa rahisi kwake kuamini kama ni kweli Inspekta Jasmine kahusika na tukio la kumwekea sumu mpelelezi kutoka idara ya usalama wa taifa aliyekuja kijijini kwao kutokana na mauaji yanayoendelea. Alikuwa anamwamini sana Inspekta Jasmine.
Gilbert Mwaitika alikuwa akiwaza mambo mengi kichwani mwake. Kwanza ni nani muuaji, japokuwa alikuwa na uhakika kwamba muuaji ni wa kike. Pili ni nani yupo nyuma ya swala la yeye kutaka kuuwawa kwa kuwekewa sumu kwenye juis ambayo Inspekta Jasmine alimpatia.

"Hii siwezi kuinywa sasa hivi eti. Nitakesha maliwatoni kwa siku nzima kama nitsthubutu kuchanganya supu na juisi ya embe kwa wakati mmoja."
Maneno haya yakapita katika ufahamu wake Gilbert. Maneno haya yalisemwa na Inspekta Jasmine wakati yeye anauliza kulikoni anywe juisi ya embe peke yake.

"Inspekta Jasmine" Alitamka kwa sauti kubwa huku akiachia pumzi ndefu itoke nje.

"Kwani ilikuwaje Gilbert?" Bwana Elius Benjamin aliuliza. Ndipo Gilbert Mwaitika akamwelezea kuanzia walipotoka kanisani hadi kufikia Kicheko Restaurant.
Wote walishangaa. Hawakutegemea kama Inspekta Jasmine angefanya vile.

"Kama si yeye ni kwanini akimbie na azime simu?" Bwana Elius akauliza huku akijaribu kurudia kupiga namba ya Inspekta Jasmine.

"Hilo swali hata mimi najiuliza nakosa jibu" Gilbert Mwaitika akasema.

Vipi na wewe unajiuliza kama wao? Hebu vaa sura ya kipelelezi leo, unahisi muuaji ni Nani? Usikose mwendelezo wa riwaya hii, uzuri ni kwamba kila lililojificha majibu yatapatikana ndani ya riwaya yetu nzuri
Cha kufanya ni wewe kulipia Tshs 2000 tu kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie.
Ni lazima maiti 15 zitimie
 
MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA

Inspekta Jasmine anamsaka Muuaji anayezidi kuteketeza roho za wanakijiji wa Kishumundu. Cha kushangaza ni kwamba Bi Sandra kabla ya kupoteza maisha alidai kwamba Jasmine amerudi, na bila shaka ndiye anayewamaliza.
Kama haitoshi mpelelezi Gilbert Mwaitika anajikuta yupo hospitali kisa kuwekewa sumu katika juisi ya embe aliyopatiwa na Inspekta Jasmine. Hapo sasa ndio nazidi kuchoka nikijiuliza inamaana ni Inspekta Jasmine ndiye muuaji au kuna Jasmine mwingine? Na kama kuna mwingine kwanini Inspekta Jasmine alipoiokota simu ya marehemu Bi Sandra alivunga kimya bila kumshirikisha Gilbert?

Riwaya ya Kipelelezi iitwayo MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA inapatikana whatsapp kwa bei ya Tshs 2000 tu. Njoo whatsapp kwa namba 0621249611 uweze kujipatia yote
 
MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA

Inspekta Jasmine anamsaka Muuaji anayezidi kuteketeza roho za wanakijiji wa Kishumundu. Cha kushangaza ni kwamba Bi Sandra kabla ya kupoteza maisha alidai kwamba Jasmine amerudi, na bila shaka ndiye anayewamaliza.
Kama haitoshi mpelelezi Gilbert Mwaitika anajikuta yupo hospitali kisa kuwekewa sumu katika juisi ya embe aliyopatiwa na Inspekta Jasmine. Hapo sasa ndio nazidi kuchoka nikijiuliza inamaana ni Inspekta Jasmine ndiye muuaji au kuna Jasmine mwingine? Na kama kuna mwingine kwanini Inspekta Jasmine alipoiokota simu ya marehemu Bi Sandra alivunga kimya bila kumshirikisha Gilbert?

Riwaya ya Kipelelezi iitwayo MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA inapatikana whatsapp kwa bei ya Tshs 2000 tu. Njoo whatsapp kwa namba 0621249611 uweze kujipatia yote
Hongera mkuu mzigo uko poa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom