Wanaume mamwinyi

Wanaume mamwinyi

Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunywa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
Vipi kuhusu Posa.....maana mi naona n moja ya vtu ambavyo vinaleta umwinyi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani lazima uolewe?
Maana kila siku mada zako ni kulalama tu.

Ukiona uko sawa na mmeo basi nawewe oa mke akuhudumie.

Labda kama wewe sio mwanamke, kama wewe ni mwanamke na umeolewa basi ndoa huiwezi maana unalalama sana.

Mada yako nyingine hii hapa ukilalama

Ewe mwanaume, zama zimebadilika, upikiwe? Kwanini wewe hupiki?
 
Inategemea mnaishi mazingira yapi na kila mmoja ana majukumu gani.?
Huwezi niambia nikatafute chumvi jikoni huku nawahi meeting ofisini ya saa 12 asbh.
Hapana aisee, labda weekend ndo ntakupikia, kukuogesha na kukubeba na mbeleko mgongoni
 
Hayo mambo tushazoea kwenye ndoa we r Tanzanian hata usomeje mwanamke lazima mumeo umhudumie kila kitu wengi tunafundishwa hvyoo
Ni jambo la kawaida pia kwetu ukiona ananuna mke hajafundwa au uzungu mwingi

My own brand!!
Patia namba yako nikutumie hela ya supu.
 
Mimi nimekuwa naambiwa ni fahari sana mwanamke kumhudumia mumewe na mwanaume anajisikia mwanaume haswaa akiwa anahudumia vyema familia yake.
 
That's nature

Sent using Jamii Forums mobile app
Nature mbona mkiwa kwenye mageto yenu hamfanyi hivyo !?
Huwa inaboa sana mtu anasimama anavua nguo anaacha hapo hapo.
Taulo kitandani,upo unapika anakuita kamletee glass mara kidogo kaita umtafutie charger,
Hujarudi vizuri anaulizia remote,
Ukikaa ujiandae uepue unaitwa ukawashe ac/feni.
Mpaka ifike jioni unatamani aondoke tu walau upumzike !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom