Wanaume mamwinyi

Wanaume mamwinyi

Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
Ndoa itakuwa imeshakishinda rudi nyumbani kamuulize kungwi upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
NDIO SABABU YA KUSHAURI WANAWAKE WAFANYE JUHUDI JUU CHINI YA KUISHI NA MCHUMBA WAKE ANGALAU MUDA MFUPI ILI UELEWE KABISA KWAMBAA NI MWINYI AU SIO. VININEVYO KAMA UNAMTAKA MTU WA KUFANYA PAMOJA HAYO MAENEO NAELEWA NI SHIDA KAMA VILE MKE MWENYE UWEZO WA KUPANDA JUU YA MTI NA KUKATA MATAWI AU KUANGUSHA NAZI
 
Hayo mambo tushazoea kwenye ndoa we r Tanzanian hata usomeje mwanamke lazima mumeo umhudumie kila kitu wengi tunafundishwa hvyoo
Ni jambo la kawaida pia kwetu ukiona ananuna mke hajafundwa au uzungu mwingi

My own brand!!

Ukiona ananuna ujue hata hizo Nguo, hicho chakula, hata hayo maji yote ni mke ndio anagharamia. Mi kafurahia sana kutunza Mme coz na yeye ananitunza. Raha ni kutunzana na kila MTU ajue majukumu yake
 
Hiyo ni kawaida kabisaa... Mume wako kumhudumia ni jukumu lako kama mke.
 
Hongera kwa kuyajua majukumu yako kwa mume!

D.A "Mwanaume mashine"
 
Cheka tu mpenzi MBITIYAZA hapo akisikia simu inaita yupo bafuni na povu lakini anatoka mkuku mkuku..
Ila kuchukua toothpick hawezi..
haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa !uwiiiiii ! kwakweli leo mie burdaniiiiiii ! bora mseme nyie tukisema sie tunaambiwa ndoa imetushinda
Haha ujue nimejigongeza mezani kwa ulivyonichekesha. Shikamoo simu

Hahahaa!, atatoka na mapovu...lol

Kuweni na moyo wa kupondeka nyie muwahudumie mamwinyi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom