Wanaume anachofanya huyu mwenzenu ni sawa?

Wanaume anachofanya huyu mwenzenu ni sawa?

Mnaingiaga mikenge Sana na watanashati..
Wengi wao very selfish..
Kiatu cha laki mbili halafu mpenzi hata nauli hampi?..

Atakua akukosha moyo na anavyo vaa na u handsome wake...ukimpost watsaap unajiona
Umepata ...huku unaumia kimyakimya..

Akija jamaa Sura personal..kiatu cha elfu kumi
Hata salam hupokei kumbe ana uwezo wa kukujali mara tano ya huyo
Mi namwambia aje kwangu sura ya Ugwadu nimpe maisha anajifanya haoni mualiko 🤣🤣🤣 anataka kupambania maumivu kwa Hemedi PHD
 
Kuitwa geto haimaanishi umeitwa kufua.

Kama ukitaka kufua fua at your own cost sio ufue utegemee mwanaume akupe malipo in terms of cash
Sijui wanaume wengine mnakwama wapi.Kumpa mtu kitu huwa hakulazimishwi ila kumpa mtu kitu kunaonyesha appreciation. Mf.amekuja geto kwako kwa mara ya kwanza.unatakiwa ujiongeze hata kwa kununua zawadi.na zawadi huwa ni kitu chochote ila kama hujafanya hivyo anapokuaga mpe hata nauli ya kurudia bas kama huna pesa.
 
Kuitwa geto haimaanishi umeitwa kufua.

Kama ukitaka kufua fua at your own cost sio ufue utegemee mwanaume akupe malipo in terms of cash
Kwahiyo mkuu wewe ukimuita mpenzi wako kwako akaja akakuta nyumba chafu nguo chafu vyombo vichafu chakula hakuna akaja mkafanya yenu akaondoka bila kufanya chochote kama vile kaja hotelini utaona poa tu na wala hautakuwa na kinyongo siyo
 
Kwa kuwa hilo ni swali umeniuliza mimi binafsi nami nitalijibu kibinafsi.

Sijawahi kuishi kwenye nyumba / chumba kichafu katika maisha yangu ya kujitegemea labda itokee nipo ugenini. Ila nakuapia ukifika kwangu utatamani kulamba sakafu kwa jinsi palivyo pasafi na kila kitu kipo kwenye mpangilio sahihi.

Suala la nguo kuwa chafu ni nadra sana maana sina utaratibu wa kurundika minguo michafu.

So akija jambo pekee analoweza kufanya japo sio lazima ni kupika ambapo mwisho wa siku tunafaidika wote.

Ila kufua sijui kudeki anayefaidika ni mmoja, kitu ambacho siungi mkono. Labda awe mke wangu au mchumba. Ila sio mpenzi tu halafu nikubebeshe majukumu ya mke wa ndoa

Nb: wakati wa kuondoka siwezi kukuacha uende mikono mitupu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom