Wanaume anachofanya huyu mwenzenu ni sawa?

Wanaume anachofanya huyu mwenzenu ni sawa?

hesalieyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
378
Reaction score
416
Najua mu wazima wa afya njema, mnaoumwa Mungu awafanyie wepesi mpone haraka.

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwenu na kueleweshwa kama ni sahihi kwa mwanaume kuhitaji mpenzi wako akufanyie kila kitu, unachotaka bila ya wewe kumjali?

Kumjali namaanisha hujui amekuja kwa nauli gani, mnawasiliana na hata ikitokea akisema hana hata credit hawezi kukuwekea, wakati pesa anayo?

Yupo radhi akuonyeshe kiatu cha laki mbili kwenye mtandao na anakuuliza kama ni kizuri ili akinunue lakini sio kukujali hata kwa kidogo wewe mpenzi wake.

Sina maana kwamba ni wajibu wake, lakini anajua wakati ninaopitia sasa kwa sababu kazi sina lakini nipo kwenye mchakato wa kutafuta na ninaamini nitapata.

Kwa upande wangu sijazoea kuomba pesa kabisa kwa mwanaume, najua yeye anajua wajibu wake kwa mpenzi wake, lakini ninajiuliza kwa huyu mwanaume nilienaye ikifikia hatua tumeingia kwenye ndoa, ataweza kunihudumua kweli pamoja na familia? Mwanaume ambaye hawezi kukupa hata senti yake?

Inafika muda natamani nifanye maamuzi magumu ya kumuacha lakini ninawaza labda atabadilika.

Je, nitumie njia gani kumrekebisha kama ipo?
 
Wenzako sikuhizi wanatuekea nyama ukeni wengine wanatufungia kwenye chupa basi unakuta tunazitoa sana noti kama tumeoa bi mkubwa anashindia karoti ela zote kwake




Anyway tuachane na hayo

We kwani unaonaje ? maana kabla hujaandika Uzi tayari jibu unalo
 
Sijui nani alileta Mfumo tegemezi wa wanawake kwa wanaume

Kwani we huna Mikono?
Si ufanye kazi?

Kwani we kwanini usimpe unategemea kupewa? Mnajishusha Sana wanawake, !!!
Nadhani ata ulivosoma hakuna sehemu nimeandika namtegemea kwa Kila kitu, inshu ni kwamba ni mbinafsi ,huyo ata Kama mmeoana ataweza hudumia familia kweli
 
Mmh huyo atakua bahili basi, hata kama uko vizuri ni wajibu wake kukujali hata kwa kidogo. Ila siku akiwa hayuko vizuri anasema unamuelewa sasa ye kila siku anajikausha kha.
Kinachoniudhi ukiwanae anataka umshauri vitu kama viatu au nguo Kama ni nzuri anataka kuagiza,kwenye mtandao,na nivyagharama.hadi nachoka aisee
 
Back
Top Bottom