Mkalukungone mwamba
Member
- Aug 29, 2022
- 71
- 134
Wanaume ambao mnawatoto embu tupeni uzoefu wenu kwa mara kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua,hiyo siku ilikuwaje na kipi utoweza kusahau kabisa
Andaa chakula cha kutosha na kizuri kwa ajili ya mama na mtoto, uwe na nyumba nzuri, mtu wa kusaidia kupika na shughuli nyingine. Uwe na bunda la kutosha la hela kuanzia sasa na kuendelea manake hiyo sasa ni familia, hakuna tena mambo ya kula kwenye migahawa, nguo za kutosha na fedha za matibabu ziwe hapo. Hapo ndio maisha yanaanza mzee.Wanaume ambao mnawatoto embu tupeni uzoefu wenu kwa mara kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua,hiyo siku ilikuwaje na kipi utoweza kusahau kabisa
Kabla ya kumpeleka hospital kujifungua jambo la kwanza unapaswa kumpeleka kuanza kliniki pale tuu anapokuambia tayari ni mjamzito kwaajili ya vipimo vya awaliWanaume ambao mnawatoto embu tupeni uzoefu wenu kwa mara kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua,hiyo siku ilikuwaje na kipi utoweza kusahau kabisa
Hongera sana mkuu wewe ni mume bora kabisa. Utakuwa baba bora pia.Uzazi wa pili Kipindi kile corona imepamba moto 2020 ingawa ilikua vyepesi sana lakini kidogo akili iliyumba.
Uzazi wa kwanza ndio sita sahau!
Kwanza kabisa hospitali ya jirani walisema uzazi wa kwanza lazima mwananyamala ama sinza.
Nikaomba sinza tukaelekezwa maana tulikuwa wa geni dar, hatuna mwenyeji hata mmoja.
tukaenda, kipimo tukaambiwa kurudi tarehe fulani, siku hio tulivyorudi nikaambia anabaki nirudi nikaandae chakula na vinginevyo, bahati nzuri tulipewa abc za kujifungua so vifaa alikuwa navyo.
Siku ya kwaza ikakata, siku ya pilli nayo ikakata!
Nikashauriwa na daktari kwamba njia imekataa kufunguka inatakiwa dawa fulani kama kumbukumbu ziko vizuri ni dinoproston, bei 50,000 kidonge kimoja! Nilizunguka mji wa dar es laam karibu kila famasia hio dawa hamna, siku inayofuata nikarudi pale namwambia ness nimekosa akanijibu ongea na watu vizuri dawa ipo hapa hapa lete hela nikuchulie!
Nusu saa nyingi dawa ikapatikana!
Akapewa dawa hata haikusaidia, siku ya nne ikaisha , siku ya tano asubuhi na fika pale mtu wa kwanza naulizia mapokezi pale nikaambiwa bado, mwanamke alishuka gorofani maana sehemu ya kujifungulia pale sinza ipo juu, ile tunakutana alikua ana lia! Nilijikaza kiume ingawa machozi yalikua yananilenga mno! Tulivyo achana nisiseme uongo nilitoka nje nikalia kwa kweli! Akaja mama mmoja simjui ila alisha nisoma, akanipeleka kwenye mgahawa akanunua chai akanipa, akaniambia wewe ni mwanaume kuwa mwanaume!
Nikarudi nyumbani kuandaa chakula jioni nikaenda tena hali ni ile ile.
Mungu ni mwema asubuhi siku ya sita saa 12 asubuhi nafika pale nikajitambulisha nikaambiwa panda juu, kufika naonyeshwa mtoto mama bado hakaa sawa katika operation dakika kumi zilizopita, nilishukuru aisee mtoto wa kiume uzito kg 4.2.
hujifungua kwa opereshen alafu mnasubiria mpaka uchungu umkamate hebu muwe mnajiongezaPicha limeanza saa tisa usiku,,baby mama uchungu umempata na kumbuka baby mama wangu hujifungua kwa operesheni
So mwelekeo ni muhimbili na ndio mtoto wangu wa kwanza,nipo makazi africana mbezi,,mungu mkubwa nje kuna nissan march kadogo kadogo hivi ndio nikakapiga start hao muhimbili,,yaan baby mama anaugulia maumivu mwamba namtaja Allah kwa sana na kumtukuza atufikishe salama
Dah ilikuwa experience ya kipekee sana