Wanandoa na extended family

Hahahaa everlenk kwanza tumepotezana pili huo mtego wa kutaja kabila huninasi ng'o maana utaniuliza na makabila/kabila linaloweka kambi

Hahahahaha!! Una bahati maana pangechimbika hapa. Nipo rafiki missing you much.....
 
Last edited by a moderator:
Nipo likizo mkuu, ndio maana unaona niko JF 24/7..

charminglady;
Kweli dada tulia kwa laptop yako hapoo chumbani. Baba anahitaji ulinzi shirikishi kwa vidume vya siku hizi. Ukiwa na charming lady ka weye ni shida tupu. Hodi za kuomba maji ya kunywa toka kwa vidume ni nyingi mpaka mama anasahau saa za kupika
 
Watu wa kanda ya kaskazini esp wachaga............

Aah!! Wapi!! Tena hawa usipime kwa visa tena ndo uwe chasaka utakoma!!,labda mchaga wa marangu maana kwa kujiskia ndo wenyewe,tena akiwa na uwezo kukuzidi ndo kabisa nyumbani kwako hakanyagi.
 

Hili ni jambo la kawaida sana na tumeshawatibia wazazi na ndugu kibao. Jambo la msingi ni kwa mwanamume kuweka wazi kwa wazazi wake kuwa boss wa nyumba ni wife. Kama kuna mtu anakwazika na hilo basi aende kwa ndugu mwingine.

Bahati nzuri wazazi wangu hawawezi kwenda kinyume na maelekezo yangu. Ila kama mwanamume unayumba basi ujue itakuwa kasheshe.
 
Vere turuu

Mie nimeona wazazi wangu wamesaidia ndugu weeeeeeeee wakalipwa ubaya...

Ndio ilonitia ukakasi

Labda hilo limeniathiri


 
Uzuri wa ndugu yako utamchamba na kumpa za uso....

Ndugu wa mwenzio unamuanzaje sasa? Si ndo mwanzo wa kuambiwa una roho mbaya huwapendi mbomoaji



 

Wanaume wachache wanaoliweza hili.
 
Haswaaaa na hili ndio tatizo

Kuketa taratibu zako kwenye nyumba ya mwenzio..... na ndio mifarakano inapoanzia



 
Well said,kabila gani hilo unalolisemea hawaweki kambi?

Kuna hawa wajita mayoweee wakija kwako wanakuja 10 au 7 ongeza na family yako, wasukuma nao akikutembelea ujue wanajibeba wengiii na hawajali hata kama una chumba kimoja na sebule
Tena ukiwa karibu na hospital yaan mjini ndugu wanaopata mimba kazi yao kuja wajifungue kwako mwingine anaweza kuja na mimba ya miez 5 anakaa mpaka ajifungue
Mi nishaona familia ambayo ni wakali wageni hua hawaji sana
 
Dah unajua babu kuna watu wana ndugu wazuri....

Mfano upande wangu mume wangu ndugu zake safi sana wana upendo na hawana hila yaani mpaka nawatamanigi


Sasa njoo upande wangu (hapa ni ndugu wa kiukoo si tuliozaliwa tumbo moja) ni vigego balaaaaaaaa......... hakuna jema. Na haikuanza na sisi ilianza enzi. Wanafikia kiasi cha kufanya fujo kabisa punde shida zao zinapoisha... kutangaziwa ubaya all over.

Sasa ndugu wa namna hiyo moyo wa kumsaidia utautoa wapi???? Matokeo yake tunaonana kwenye matukio tu ili kuepusha mifarakano... harusi misiba komunyo


 
Nyumba nyingi kimekosekana hiki na ndio chanzo cha tatizo, mtu akikaa kwako hajaja kutembea au kukua, kama ni mwanafunzi apige shule kwa kwenda na akitoka shule anatekeleza majukumu madogo madgo ya hapo nyumba kisha usiku anaingia prepo, jumamosi ni kufuta madirisha vumbi na wengine wanafyeka na kazi zingine ndogo ndogo alafu mchana wana relax na jumapili. Lakini mkiwa pande mbili alafu kila mtu anaita watu wake na kukaa nao lazima kutakuwa na shida. Na ndugu wa kiswahili ni noma kwa kusimangana maana wengi wamekaa katika pozi la kujiona kama hapo sio kwao
 
Loh wametisha!!!!!!


 
nmelelewa kwenye extenda family tangu naanza shule. mwanzoni wakati bado mdogo it was hard kwa kweli, nilikuwa najiona mtoto ninaestahili matunzo ya mama bila kutambua niko kwa watu. thank God kadiri umri ulivyoenda ndivyo nilivyopatana na yule shemeji yangu. cha msingi kwa wale wenzangu ni kujitambua uko wapi kwa sababu gani. na daima kumbuka 'YATIMA HADEKI'
 
Hahahaha kuna mtu shemeji yake kila.akishisha mzigo anaacha mavi
Hehehe akiambiwa aflash anazua ugomvi na kutaka kumpiga mke,



Halaf ukute choo cha ndani mbona mtajutraaaaaa ukimwambia tu kosaaa
 
Umetusema aisee, anyway ila kiukweli ukikaa mjini especially kama mmoja either mume au mke wazazi wake wote ni kutoka kijijini na bahati mbaya huyo partner wako ndio katokamo alafu wadogo zake wote wameishia darasa la 3A hapo tegemea wageni tu kila siku vinginevyo ni kujitahidi kutoa support wakiwa huko huko maana maisha yetu watz kama wewe hujapata extended family basi wazazi wako walikuwa wanaishi maisha extended family. Kwa ujumla hii hali ipo karibu kote especially kama unakaa katika mkoa ambao mmoja wa wanandoa anatoka hapo.
 

Hivyo ndivyo inatakiwa maana wengine huwa tunaishi nao kwenye hizi familia na ukiangalia ni dogo tu alafu amefanya blunder yaani ukimkoromea tu kama ilivyo kawaida yetu wabantu kumkoromea dogo anakuona kama unamnyanyasa wakati the same kama ukimkoromea mdogo wako wa damu kwa level ile ile anachukulia poa. Kikubwa ukikaa kwa mtu kuna baadhi ya vitu hutakiwi kujilinganisha na mtoto wa anaekuweka mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…