Wanandoa na extended family

Wanandoa na extended family

Exactly ila kwa family za kitanzania/ africa bado ni ngumu,umetoka tu honeymoon unakutana na msururu wa ndugu wameshajifungasha virago vyao wsnahamia kwako,daah aisee halafu wao ndo wanakua mababa wenye nyumba on behalf of their brother,just imagine,hii niliishuhudia kwa best yangu,tulisimamia ndoa yake sasa siku amerudi toka honeymoon alikuta ndugu wa mume washahamia

Siajaabu hata tution classes bi harusi anawajibika.... baada ya kuwaandalia chakula ! ( lakini jamanii hosteli zipo nyingi,Mama ntilie zipo kila kona, Khaa sijui tabia gani zisizoeleweka? ) Lifu tunaishi once !
 
Krenea your right.kwenye ndoa nyingi wanawake ni wabinafsi sana sana.wanapenda na kufurahi wakija ndugu zake.lakini wakija wa mume ni matatizo.badilikeni wake zetu
 
ili kuepusha shari na kufanya uwelewane na mkeo/mume ni kuwasaidia ndugu hukohuko waliko, ni ndugu wachache sana ambao wanaweza wakawa waelewa lakini asilimia kubwa ni sheeeda
 
Habari za jioni mabibi na mabwana katika jukwaa hili?

Naomba tujadili changamoto zitokanazo na kuishi na ndugu wa mume/mke, watoto wa kambo katika familia.

Hii imekuwa changamoto hasa kwa wanawake tushindwa kuishi na ndugu ama watoto wa mwanaume.

Kuna msemo huu "Ndugu hawana jema, hata uwabebe mgongoni" je msemo huu una ukweli?

Je tatizo ni nini?

Ni jinsi gani ya kukabiliana na changamoto hizo??

Nina mifano hai miwili ambayo wadada wameshindwa kuvumilia kuishi na ndugu. Wanalalamika ndugu wa mume wana masimango, hawaridhiki na chochote wanachofanyiwa...

Karibu kwa mjadala

kinachonishangazaga mimi ni kwa nini ugonvi wa mke na mashemeji au mawifi uonekane wa ajabu kana kwamba yeye na ndugu zake huwa hawagombani, nadhani tunashindwa tu kuziona hizo kama changamoto tulizo nazo katika familia zetu hata bila mke/mume, tujiulize ukikaa na ndugu zako tu hamgomabanagi? kwa nini ugonvi na ndugu wa mme/mke uonekane wa ajabu? extended familia kwa mtu mwenye akiri timamu haziepukiki, maana wengi ndo tulikotokea.
 
Ndio maana ukikutana na mtu lazima atakuuliza "Kwenu mpo wangapi" alaaa kumbe huwa wanamaanisha hili!

Vipi kwa upande wa wanaume nasi tuwe tunawauliza kwao wapo wangapi ili kuepuka kuwa na mawifi wengi na mashemeji????

EH muhimu kuuliza bwana....mie sitaki mke wangu kwao utitili wa madogo.
 
Mentor, iwapo MJEDA angesema atusaidie huko tulipo, labda hata hapa JF msingenijua.....
Kuna mambo mengine kuyajadili kijumla jumla hatuwezi kupata muafaka, mimi labda tu niseme kwamba sishabikii kuishi na ndugu hasa kwa mazingira ya sasa, lakini wengi wetu hapa tumelelewa na ndugu na kusomeshwa na ndugu, kwa hiyo wakati tunapinga hapa, lazima tukumbuke tulipotoka........

walau hapa umenena vizuri!!!
 
Back
Top Bottom