Charminglady;
Sikujua kuwa na weye una inda! Loh! Tabasamu loote hilo kumbe ndani moyo korosho! Weye huna hakika na aliye kuoa? Waliokuja woote wawekee full stop. Pale pale mwanzoni, hata kabla hujafua zile nguo ulizotoka nazo kwenyu. Hakikisha wanaijua mipaka yako na mumeo kwao. Uliolewa na mtu mmoja sio ukoo.
Wa kuja kwenu aje lakini akijua kakayao, kijana wao, au baba mdogo wao, kesha oa. Alimwoa Charminglady. Hajaoa kijiji. Ukiisha kuweka misimamo yako hiyo, sasa wale ambao umewakuta kwake, watoto wa kambo, wapende kwani walikutangulia. Waoneshe kuwa, unawapenda, utawaheshimu nao pia wakuheshimu.
Ukianza kuwa nyanyasa, itakula kwako. Waswahili husema; Nkune nami nkukune! Heshima ni reciprocal!
Sikuona sababu ya wewe kum attack mtoa mada wakati kauliza swali na wali hili swala haliitaji mtu kuwa amelifanya ndio alijadili maana kila mtu anajua kabisa kuna ukweli! Pengine hukumsoma vyema!
Back to topic!
Ukweli ni kwamba wanaopata shida kwenye hili ni wanawake hasa wanapo kutana na ndugu wakorofi!
Lakini mara nyingi huwa najiuliza kwanini huwa linawasumbua wanawake hili swala hata kabla ya kuingia kwenye ndoa? Na ni Ukweli ulio wazi wanawake walio wengi hawapendi kuishi na ndugu wa mume hata kama hawakuwai kuwa kosea!
Pengine ni kweli ina hitaji kifua na uvumilivu sana kuishi na ndugu na watu tuna mifano mingi unaona mwanamke wanapo kuja ndugu wa mume anachukia Lakini wa kwakwe hata wakikaa hapo mwaka hana shida!
Wanawake muda mwingine wana sahau kabisa kuwa mtu anajengwa na aina ya familia aliyo kuwa nayo! Na mara nyingi swala la kuishi na ndugu huwa haliwasumbui sana wanaume hata kama wangekuwa wa mwanamke!
Kibaya zaidi baadhi ya wanawake wanakuwa wameshajenga kabisa kichwani kuwa ndugu wa mume wana gubu ,chuki hivyo anaweka kichwani na huwezi kumbadilisha na kweli hataki kuwaona!
Kwa upande mwingine kama mwanaume una kuwa sio makini Ndugu wanaweza vunja ndoa maana Kuna wengine kabisa na ni ukweli ni wakorofi na wana gubu hivyo kuishi nao ina hitaji kifua na uwe mtu wa kupuuza na hili lina washinda wana wake wengi!
Kuna baadhi ya wanawake wanafikiri wanaweza kuwatenganisha ndugu wa mume na mume wake anasahau kabla ya kuolewa hao ndugu walikuwepo na wengine wana diriki kwenda hadi kwa waganga kuhakkisha Mume ana wachukia ndugu zake!
Hivyo katika mitihani ambayo wanawake wengi wanafeli na wengine walishajitolea kufeli ni kuishi au jinsi ya kuishi na ndugu hasa wa Mume!
Mwanamke ana hitaji kifua,uvumilivu na busara kuishi na ndugu hasa wa Mume!