Wanandoa na extended family

Wanandoa na extended family

Pole sana ndugu yangu. Naamini hutoi na kujiumiza mwenyewe.

Kwa upande wangu, siwezi kumlaumu mke wangu kwa jinsi yoyote atakavyowatendea ndugu. Hata mimi nilikuwa na mawazo kama wanaume wengine kwamba labda hawapendi ndugu zangu. Ila uzoefu umenifunza kwamba ndugu hawabebeki, hawashibi, hawatosheki.....Kadri unavyojitesa ndivyo wanavyodai zaidi.

Dawa ni kutoa pale unapoweza na kuwahudumia wakiwa kwao!

Asante sana,wewe sasa ni baba kamili,ukikuta mwanaume kaongea haya ujue amekomaa haswaa,nikupongeze kwa hilo.

Haswaa ni kutoa kadri unavyoweza,uchoyo wa nini?kikiwepo ni kutoa tu,kisipokuwepo ndugu aelewe tu hilo halipo na haliwezekaniki.
 
Kwa kweli ndugu wengi upande wa mume sio wote wako hivyo best hawabebeki , hawashikiki hii ni kutokana na mfumo wa kitamaduni wetu wa kupenda kukaa pamoja kindugu mfano wale wanaotoka kule kaskazini juu wao hupenda kukaa pamoja kama nchi fulani iliyopakana na mkoa wa nyanda za juu kusini wao chumba kimoja wanakaa rukuki utadhani ndege wanaatamia vifaranga vyao kwa uwingi walionao

nirudi katikamada hapo juu:

Kweli ndugu wengi hawabebeki ni watu ambao uleta matatizo ndani ya ndoa ya ndugu yao cha kufanya
ni bora kuwaambia ukweli pindi unapoona mambo yameparaganyika au kuna utofauti kati yao na mke /mume wako, na kuwaambia wawapishe waende makwao utawahudumia khuko huko waliko kwani pale wanaweza kuweka shubiri mbaya ndani ya ndoa yenu cousin
 
Heri yangu mie nilepiga marufuku ndugu zangu kukaa kwa wanandoa. Tena hili ndio lilikuwa la kwanza kusisitiza kati ya yote. Ndugu asaidiwe huko aliko.
kwani ni ndugu wote wanaohitaji msaada?? wangine yaweza kuwa ni matembezi tu! lkn km ni msaada bhac asaidiwe hukohuko aliko!! pia jambo hili mm nilihusisha na kipato kidogo, maana mtu anapoingiwa na roho ya uchoyo ndo bifu linapoanza!!
 
Kuishi na ndugu inahitaji moyo hua wanataka anachokufanyia mume nae awafanyie hivyo hivyo
 
Asante sana,wewe sasa ni baba kamili,ukikuta mwanaume kaongea haya ujue amekomaa haswaa,nikupongeze kwa hilo.

Haswaa ni kutoa kadri unavyoweza,uchoyo wa nini?kikiwepo ni kutoa tu,kisipokuwepo ndugu aelewe tu hilo halipo na haliwezekaniki.

Hahahahah, hivi unajua kuwa ukiwaeleza ndugu kwamba huna hawakuamini?

Ushauri wangu ni kwamba wanandoa wakubaliane jinsi ya kusaidia ndugu wa pande zote. Sisi baada ya majaribio ya zaidi ya miaka 20, tumeshaamua kutoka hi na mtu zaidi ya mfanyakazi. Na huko mbele ya safari tunaweza kuishi peke yetu pale watoto wakishapata makazi yao.

Inconvinience za ndugu hazivumiliki.
 
Kuishi na ndugu inahitaji moyo hua wanataka anachokufanyia mume nae awafanyie hivyo hivyo

Kweli, tena baadhi ya ndugu hawataki kutambua hadhi ya mke kwa mume wake. Utakuta mama wa mume anajiona kuwa ni nambari one kwa kijana wake!
 
Habari za jioni mabibi na mabwana katika jukwaa hili?

Naomba tujadili changamoto zitokanazo na kuishi na ndugu wa mume/mke, watoto wa kambo katika familia.

Hii imekuwa changamoto hasa kwa wanawake tushindwa kuishi na ndugu ama watoto wa mwanaume.

Kuna msemo huu "Ndugu hawana jema, hata uwabebe mgongoni" je msemo huu una ukweli?

Je tatizo ni nini?

Ni jinsi gani ya kukabiliana na changamoto hizo??

Nina mifano hai miwili ambayo wadada wameshindwa kuvumilia kuishi na ndugu. Wanalalamika ndugu wa mume wana masimango, hawaridhiki na chochote wanachofanyiwa...

Karibu kwa mjadala

Kuishi na ndugu ni ujima.

Naelewa kutembeleana kwa muda, lakini kuishi na ndugu dunia ya leo kunaongeza msuguano.
 
Kuishi na ndugu ni ujima.

Naelewa kutembeleana kwa muda, lakini kuishi na ndugu dunia ya leo kunaongeza msuguano.

Word!

Nashangaa bado kuna watu wanaamini kuwa kuwa na team ya ndugu wengi uliowabeba ni sawa na life insurance!
 
Mh, Mie mwenyewe nilikulia kwa kaka yangu na kusomeshwa na kaka yangu...
Kwa kweli nakosa hata la kusema maana shemeji yangu yaani mke wa kaka yangu yeye nadhani yuko kwenye nafasi nzuri kueleza kuhusu jambo hilo.

Lakini labda niseme tu kwamba kwa mila za Kiafrika kuishi na ndugu haikwepeki, hata kama umezaliwa peke yako.

Naamini wale wadau wa Leo Tupo Hapa Pub wanamjua MJEDA

CC: charminglady, Paloma, watu8, Asprin, Kaizer, Ruttashobolwa, Mentor, Madame B KakaKiiza, LiverpoolFC, Erickb52, Filipo, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi
 
Last edited by a moderator:

Hakika.
 
Kuna ndugu wanakera balaa.

Anakula vitu ovyo kwenye friji, viguu anaweka juu ya sofa, haflash choo wala nini.
 
Ukiweza..wasaidie huko walipo!
Mentor, iwapo MJEDA angesema atusaidie huko tulipo, labda hata hapa JF msingenijua.....
Kuna mambo mengine kuyajadili kijumla jumla hatuwezi kupata muafaka, mimi labda tu niseme kwamba sishabikii kuishi na ndugu hasa kwa mazingira ya sasa, lakini wengi wetu hapa tumelelewa na ndugu na kusomeshwa na ndugu, kwa hiyo wakati tunapinga hapa, lazima tukumbuke tulipotoka........
 
Last edited by a moderator:
Mh, Mie mwenyewe nilikulia kwa kaka yangu na kusomeshwa na kaka yangu...
Kwa kweli nakosa hata la kusema maana shemeji yangu yaani mke wa kaka yangu yeye nadhani yuko kwenye nafasi nzuri kueleza kuhusu jambo hilo.

Lakini labda niseme tu kwamba kwa mila za Kiafrika kuishi na ndugu haikwepeki, hata kama umezaliwa peke yako.

Naamini wale wadau wa Leo Tupo Hapa Pub wanamjua MJEDA

CC: charminglady, Paloma, watu8, Asprin, Kaizer, Ruttashobolwa, Mentor, Madame B KakaKiiza, LiverpoolFC, Erickb52, Filipo, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi

Mjeda njoo hapa useme kitu...
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni tabia mbaya inabidi ikemewe kwa nguvu zote.................

Mzee Mtambuzi pale ambapo utaanza kumkemea ndipo atakapoanza kusema ubaya wa mke.

Kuna wanaoenda mbali na kusema maneno ya uongo na uchonganishi.

Wanataka kila wafanyalo hata liwe baya lisikemewe.
 
Last edited by a moderator:
Mentor, iwapo MJEDA angesema atusaidie huko tulipo, labda hata hapa JF msingenijua.....
Kuna mambo mengine kuyajadili kijumla jumla hatuwezi kupata muafaka, mimi labda tu niseme kwamba sishabikii kuishi na ndugu hasa kwa mazingira ya sasa, lakini wengi wetu hapa tumelelewa na ndugu na kusomeshwa na ndugu, kwa hiyo wakati tunapinga hapa, lazima tukumbuke tulipotoka........

Mkuu kwa sisi tulio kulia kwenye extended family hatushangai unayo yasema.
Na wanaongoza kusema tutawasaidia huko huko walipo ndio hao hao wengi wao walio saidiwa kwa karibu na wakavutwa lakini hawakusaidiwa walipo kuwa.

Tunayo yaandika si tunayo yatenda na tukiyatenda tuna yatenda kwa pressure za watu.
 
Mzee Mtambuzi pale ambapo utaanza kumkemea ndipo atakapoanza kusema ubaya wa mke.

Kuna wanaoenda mbali na kusema maneno ya uongo na uchonganishi.

Wanataka kila wafanyalo hata liwe baya lisikemewe.

Unajua katika swala kama hili ina hitajika busara sana hili kulifikisha kwa muhusika na ni vyema ukamwambie mkiwa peke yenu tena akiwa katika mood nzuri na unatakiwa kutumia njia ambayo hatogundua kuwa umeambiwa na mtu.
Sasa kama utamwambia haya mbele ya wifi au shemeji yake unategemea nini kama si mtiti?
 
Back
Top Bottom