Wanandoa na extended family

Wanandoa na extended family

Sikuona sababu ya wewe kum attack mtoa mada wakati kauliza swali na wali hili swala haliitaji mtu kuwa amelifanya ndio alijadili maana kila mtu anajua kabisa kuna ukweli! Pengine hukumsoma vyema!

Back to topic!
Ukweli ni kwamba wanaopata shida kwenye hili ni wanawake hasa wanapo kutana na ndugu wakorofi!
Lakini mara nyingi huwa najiuliza kwanini huwa linawasumbua wanawake hili swala hata kabla ya kuingia kwenye ndoa? Na ni Ukweli ulio wazi wanawake walio wengi hawapendi kuishi na ndugu wa mume hata kama hawakuwai kuwa kosea!

Pengine ni kweli ina hitaji kifua na uvumilivu sana kuishi na ndugu na watu tuna mifano mingi unaona mwanamke wanapo kuja ndugu wa mume anachukia Lakini wa kwakwe hata wakikaa hapo mwaka hana shida!

Wanawake muda mwingine wana sahau kabisa kuwa mtu anajengwa na aina ya familia aliyo kuwa nayo! Na mara nyingi swala la kuishi na ndugu huwa haliwasumbui sana wanaume hata kama wangekuwa wa mwanamke!

Kibaya zaidi baadhi ya wanawake wanakuwa wameshajenga kabisa kichwani kuwa ndugu wa mume wana gubu ,chuki hivyo anaweka kichwani na huwezi kumbadilisha na kweli hataki kuwaona!

Kwa upande mwingine kama mwanaume una kuwa sio makini Ndugu wanaweza vunja ndoa maana Kuna wengine kabisa na ni ukweli ni wakorofi na wana gubu hivyo kuishi nao ina hitaji kifua na uwe mtu wa kupuuza na hili lina washinda wana wake wengi!

Kuna baadhi ya wanawake wanafikiri wanaweza kuwatenganisha ndugu wa mume na mume wake anasahau kabla ya kuolewa hao ndugu walikuwepo na wengine wana diriki kwenda hadi kwa waganga kuhakkisha Mume ana wachukia ndugu zake!

Hivyo katika mitihani ambayo wanawake wengi wanafeli na wengine walishajitolea kufeli ni kuishi au jinsi ya kuishi na ndugu hasa wa Mume!

Mwanamke ana hitaji kifua,uvumilivu na busara kuishi na ndugu hasa wa Mume!

Umenena vyema.Point ya msingi ukiishi na ndugu yeyote ukaona habebeki mrudishe kwao.Tafuta ambae kweli anaonesha anajua anachoitaji.
 
Heri yangu mie nilepiga marufuku ndugu zangu kukaa kwa wanandoa. Tena hili ndio lilikuwa la kwanza kusisitiza kati ya yote. Ndugu asaidiwe huko aliko.
 
chakula ndo kila ktu hasa kwa sisi wabongo
hata ukirudu kwenu watakuuliza vp kula lakini
mtu mwenye roho mbaya lazma akunyime kula maana atahisi we unammalizia au umezidisha bajeti
bila kula husomi,hulali usiku utahesabu kenchi
bila kula utadhoofika
kula kwqnza ndo msingi wa yote

Unafikiri walosema adui yako muombee njaa walikosea.
 
hakuna guarantee kwenye chochote duniani mkuu, hata vitega uchumi vinaweza kufa, hata bima watoto bila msaada na ushauri mzuri wanaweza itumia vibaya, kumsaidia ndugu yako unamsaidia sababu ni damu yako, na ni investment kama nyingine tu unaweza pata return au usipate, mimi naamini katika kusaidia ndugu zangu ila sio kukaa na nao kibao home kwangu, huo ulikuwa mfano tu.

unapotoa msaada usiufanye deni wala usingoje shukrani!

Naomba mnisaidie kitu ndugu zangu,

Haya mnayoyasema ni kutokana na uzoefu au wishful thinkng plus sweet delirium?
 
Wanawake wamejaa na roho mbaya sana, mbona ndugu zao wakijazana kwa mume hawanung'uniki?...binafsi sioni tatizo kuishi na ndugu wa mke/mume as long as wanajibehave katika maadili yaliyo mema.
 
Na hicho ndicho ninachomaanisha..

Jaribu kuangalia kwenye kamusi ya kiswahili maana ya neno "kufuga". Na kama bado lina utata tunaweza kuendelea na mjadala wa hilo neno.

Na kama umekuwa ukifuatilia michango yangu, ni kwamba nilishachoka na mambo ya ndugu. Na kwa kweli nakosa neno zuri zaidi la kutumia. Sorry, kama nimekukwaza!

hahahaa, unikwaze nini ndugu yangu wewe una familia yako na misingi yako na mini nina familia yangu na misingi yangu, nilitakak uelewa tu kama unamaanisha kufuga kwa maana ya mtu anakaa tu hana aa wala bee au na mtoto wa dada yako unayemsomesha naye unamfuga? Tunatofautiana makuzi mkuu, wengine tumetoka familia duni sasa tukiwa wabinafsi tutakuwa hatutendi haki. Kama mtu hana kazi na amekuja kwangu obviously anataka nimtafutie kazi, nitamtafutia, kama hana vigezo mashamba yapo atakwenda kusaidia kazi huko na kuwa usefull!
 
Wanawake wamejaa na roho mbaya sana, mbona ndugu zao wakijazana kwa mume hawanung'uniki?...binafsi sioni tatizo kuishi na ndugu wa mke/mume as long as wanajibehave katika maadili yaliyo mema.

Picture this wewe ndio mama mwenye nyumba anakuja binamu yako kakorofishana na mume wake kwa sababu alisahau birthday yake. anakuja kukuomba wewe dada yake akae kwako, mimi ninakutimua saa hiyo hiyo hata kabla haujaketi. Ndugu wa aina hii awe wa mume au wa mke natimua tu. kuzoeana kunapunguza heshima.
 
Naomba mnisaidie kitu ndugu zangu,

Haya mnayoyasema ni kutokana na uzoefu au wishful thinkng plus sweet delirium?

kaka tunatofautiana makuzi, marehemu babu yangu mimi alikuwa mfugaji mkubwa sana, watoto wake wote hakukaa nao ni shuleni kutoka shule wakaajiriwa wakawa wa mjini, "wafugwa" na watu baki, wengine raiya wa kigeni ndiyo waliomsaidia kazi za shamba, shuguli za nyumbani, alipofariki mifugo na mashamba iligawanywa mpaka kwa hao "wafugwa" wakaanzisha maisha yao! usiwachukulie ndugu wenye shida kama wafugwa, binafsi nawachukulia kama watu wanaohitaji msaada tu na najitahidi kuwasaidia kwa faida yangu na yao pia!! again, tunatofautiana makuzi, aliyekulia familia bora ni ngumu kuelewa!
 
Na sijui kwanini wanawake tumejijengea picha ya kwamba ndugu wa mume wote ni mizigo. Kuna ambao hawana shida jamni ukiishi nao.Binafsi siwezi shindwa kuishi na ndugu yeyote.Labda yeye ashindwe kuishi na mimi au tushindwane tabia.

Mtu ambae nkiishi nae itabidi Mungu anioongezee hekima ya mara mbili nlonayo labda mama mkwe.
 
kaka tunatofautiana makuzi, marehemu babu yangu mimi alikuwa mfugaji mkubwa sana, watoto wake wote hakukaa nao ni shuleni kutoka shule wakaajiriwa wakawa wa mjini, "wafugwa" na watu baki, wengine raiya wa kigeni ndiyo waliomsaidia kazi za shamba, shuguli za nyumbani, alipofariki mifugo na mashamba iligawanywa mpaka kwa hao "wafugwa" wakaanzisha maisha yao! usiwachukulie ndugu wenye shida kama wafugwa, binafsi nawachukulia kama watu wanaohitaji msaada tu na najitahidi kuwasaidia kwa faida yangu na yao pia!! again, tunatofautiana makuzi, aliyekulia familia bora ni ngumu kuelewa!

Naomba tuelewane walau kwenye hili dogo. Sina maana kwamba sina ndugu wenye shida na wala siwasaidii. Ni kikupa undani wa jinsi ninavyowasaidia utashangaa. Hata hivyo msimamo wangu ni kwamba ndugu hatakaa kwangu. Period!

Nina sababu nyingi na InshaAllah, nitaeleza baadaye!
 
kiukweli mie kwangu ukija ndugu wala sijiulizi mara mbili mbili, na hata kama utakuwa mgonjwa nitakutibia ukipona utaondoka kwa amani na hata kama utanilipa baya sitawaza manake najua majaribu yapo na mtu hujaribiwa kwa akipendacho.

iko hivi mara nyingi sana akina mama/wake mioyo yetu huwa kwenye ndoa zetu na ndicho kitu tukipendacho zaid na shetan naye kwa kulijua hilo huwa anatujaribu kupitia ndoa zetu. ujue pale moyo wako ulipo ndipo hazina yako ilipo na wengi badala ya kumfanya Mungu kuwa hazina zetu na mioyo yetu kuwa kwake siye tumefanya hazina zetu kuwa ndoa zetu na mioyo yetu kuwa hapo. kinachotokea NI iBILISI kukujaribu kupitia ndoa iyo iyo.

chunguza kwa wanawake wote wanaopitia magumu kwenye ndoa wengi watakuambia ndoa zao wanazipenda na ndo mana zikileta shida wanakonda na kuchoka kabisa yaani ata kama akitafuta mchepuko ataenda tuu kwa tabia za kimwili lkn moyoni hilo linamuuma kuliko jambo lolote lile.

Tumtangulize Mungu zaid kwenye maisha yetu na yeye atahangaika na yale yaliyo ya haki yetu

Kweli kabisa ukimtanguliza Mungu hakuna jambo gumu,mimi kuna wakati nilikuwa naumia kwanini kila ninapowatendea hawa ndugu mema ndivyo ambavyo inakuwa shida,nikamwomba Mungu anipe njia ya kutatua hilo,nikaona njia ya kwanza ni kuacha mashindano,pili ni kutoa zaidi ya mwanzo,ikawa ndugu akija kwangu akiomba mkate mmoja mimi ntatoa miwili hata mitatu. Akija kwangu akakuta sijui nina mapazia gani mazuri akiomba namtolea na mengine,kataka sijui kitenge changu nitaenda kununua na vingine viwili nimpe. Na hii imesaidia sana kuondoa kelele za kuvutana vitu vidogovidogo visivyo na maana. Na hata wenyewe wamefika mahali wameshindwa wanaona labda mtu anichokoze kwenye hili ananikuta mie peace tu.
 
Hongera, you real deserve it ... mimi pia nimeoa, I thought bado nikukaribishe kupambanisha chemistry na bro wangu!Anyway, kila la kheri na maisha mema ...

Asante sana nawe pia uwe na maisha mema.
 
Kweli kabisa ukimtanguliza Mungu hakuna jambo gumu,mimi kuna wakati nilikuwa naumia kwanini kila ninapowatendea hawa ndugu mema ndivyo ambavyo inakuwa shida,nikamwomba Mungu anipe njia ya kutatua hilo,nikaona njia ya kwanza ni kuacha mashindano,pili ni kutoa zaidi ya mwanzo,ikawa ndugu akija kwangu akiomba mkate mmoja mimi ntatoa miwili hata mitatu. Akija kwangu akakuta sijui nina mapazia gani mazuri akiomba namtolea na mengine,kataka sijui kitenge changu nitaenda kununua na vingine viwili nimpe. Na hii imesaidia sana kuondoa kelele za kuvutana vitu vidogovidogo visivyo na maana. Na hata wenyewe wamefika mahali wameshindwa wanaona labda mtu anichokoze kwenye hili ananikuta mie peace tu.

Pole sana ndugu yangu. Naamini hutoi na kujiumiza mwenyewe.

Kwa upande wangu, siwezi kumlaumu mke wangu kwa jinsi yoyote atakavyowatendea ndugu. Hata mimi nilikuwa na mawazo kama wanaume wengine kwamba labda hawapendi ndugu zangu. Ila uzoefu umenifunza kwamba ndugu hawabebeki, hawashibi, hawatosheki.....Kadri unavyojitesa ndivyo wanavyodai zaidi.

Dawa ni kutoa pale unapoweza na kuwahudumia wakiwa kwao!
 
Hakuna sababu ya ndugu kutoka kijijini kuhamia kwako, watu lazima wakubali maisha ni magumu kila sehemu mjini na vijijini na inatubidi kufanya kazi kwa bidii. Afadhali ukae na ndugu unamsomesha, sasa mtu mzima asie na aaa wala bee kazi kubadili station za TV hata mimi tutakosana. Kafanye kaziiii full stop
 
Nadhani hii husababishwa na kati ya moja ya au kwa pamoja sababu tatu kuu. 1)Malezi 2) maisha duni/changamoto za maisha 2)Tabia mbaya binafsi.

1)Malezi;
Msingi wa malezi yenye tabia mbaya ndiyo chanzo.Wapo waliolelewa kibinafsi ambao hujijali wao na ndugu zao tu kwamba wanastahili zaidi.Hawa huziendeleza tabia hizo za wivu, umbea, vijimaneno,kunung'unikia mambo madogo n.k hata pale achukuliwapo na familia ya ndugu yake huyo kwajili ya msaada tu.

2)Maisha duni/changamoto za maisha;
Hii hutokea pale familia iliyojikokota kwa shida kutoka kimaisha(kupeleka watoto shule n.k) na hatimaye mmoja wa wanafamilia akapata nafasi nzuri/akaweza kujimudu vizuri tu bila shida...basi wanafamilia/ukoo huwa na hisia kuwa chochote akipatacho ndugu yao huyo ni sharti kiwafae wana familia/ukoo kwanza kabla ya mke/au mume aliyeolewa wakati wa maisha yakiwa vizuri.Hapo vitimbi huanza.

3)Tabia mbaya binafsi.
Ukiachilia sababu mbili ziizotangulia,baadhi yetu tumeumbwa,au tumeendekeza kwa kujizoesha tabia za ubabe,ubwana au ubibi...hii ni kwa wanandoa binafsi ambayo pia hupandikiza kwa ndugu zake au hulka tu na mwelekeo wa jumuiya na marafiki.

Kukabiliana ni vyema familia ikaishi yenyewe na kutoa msaada kwa mbali tu...binadamu tuna mapungufu, heri mapungufu na kukosoana wakosoane wanandoa wenyewe.
 
Umenena vyema asante kwa mchango wako...
 
Back
Top Bottom