Wanandoa na extended family

Wanandoa na extended family

Hahahaa everlenk kwanza tumepotezana pili huo mtego wa kutaja kabila huninasi ng'o maana utaniuliza na makabila/kabila linaloweka kambi

Hahahahaha!! Una bahati maana pangechimbika hapa. Nipo rafiki missing you much.....
 
Last edited by a moderator:
Nipo likizo mkuu, ndio maana unaona niko JF 24/7..

charminglady;
Kweli dada tulia kwa laptop yako hapoo chumbani. Baba anahitaji ulinzi shirikishi kwa vidume vya siku hizi. Ukiwa na charming lady ka weye ni shida tupu. Hodi za kuomba maji ya kunywa toka kwa vidume ni nyingi mpaka mama anasahau saa za kupika
 
Watu wa kanda ya kaskazini esp wachaga............

Aah!! Wapi!! Tena hawa usipime kwa visa tena ndo uwe chasaka utakoma!!,labda mchaga wa marangu maana kwa kujiskia ndo wenyewe,tena akiwa na uwezo kukuzidi ndo kabisa nyumbani kwako hakanyagi.
 
Hili ni kweli kabisa ndugu ukimwambia huna haamini kabisa,kwangu mimi kama sina kweli aongee tu awezavyo na wala sitachukia kwa maneno yake.

Mimi naomba unisaidie hapa,mfano wewe babu DC baba yako anaumwa huko kijijini aliko,wewe wakaa DSM,ukaamua baba yako aje DSM ili umsaidie matibabu na bila hiyana lazima akae kwako,na umekuja kugundua matibabu yake yanachukua muda sana,na umejitahidi kufanya kila liwezekanalo mgonjwa akae sawa,siku 2 mzima siku 2 mgonjwa , na tabia ya baba yako kiasili ni mtata,kiasi fulani kwa miezi kadhaa aliyokaa kwako ni kero kwa mkeo. Utafanyaje juu ya hili swala?

Hili ni jambo la kawaida sana na tumeshawatibia wazazi na ndugu kibao. Jambo la msingi ni kwa mwanamume kuweka wazi kwa wazazi wake kuwa boss wa nyumba ni wife. Kama kuna mtu anakwazika na hilo basi aende kwa ndugu mwingine.

Bahati nzuri wazazi wangu hawawezi kwenda kinyume na maelekezo yangu. Ila kama mwanamume unayumba basi ujue itakuwa kasheshe.
 
Vere turuu

Mie nimeona wazazi wangu wamesaidia ndugu weeeeeeeee wakalipwa ubaya...

Ndio ilonitia ukakasi

Labda hilo limeniathiri


Hakuna guarantee kwamba ukiwasaidia ndugu watahudumia familia yako ukikutwa na mauti. Kama hao ndugu hawawezi hata kukusalimia ukiwa hai, wataanzia wapi kuhudumia familia yako ukitangulia mbele za haki?

Kwa nini tusiwekeze kwenye vitega uchumi vyenye uhakika au bima?

Habari yandu sitaki kusikia kabisa!
 
Uzuri wa ndugu yako utamchamba na kumpa za uso....

Ndugu wa mwenzio unamuanzaje sasa? Si ndo mwanzo wa kuambiwa una roho mbaya huwapendi mbomoaji



ukishakuwa na msemo kuwa NDUGU WA MUME HATA UMBEBE MGONGONI HARIDHIKI kwenye akili yako hutakaa ukawa na amani....
kila watakachofanya hata kama ni yale ya kawaida ambayo hata mamaako au dadaako au kakaako angefanya ww utaona wanafanya kwa sababu ni ndugu wa mume..

WANAWAKE; acheni kuwa na inferiority complex.. itawatesa sana..

chukulia maisha simple... MBONA SIMPLE TU?
 
Hili ni jambo la kawaida sana na tumeshawatibia wazazi na ndugu kibao. Jambo la msingi ni kwa mwanamume kuweka wazi kwa wazazi wake kuwa boss wa nyumba ni wife. Kama kuna mtu anakwazika na hilo basi aende kwa ndugu mwingine.

Bahati nzuri wazazi wangu hawawezi kwenda kinyume na maelekezo yangu. Ila kama mwanamume unayumba basi ujue itakuwa kasheshe.

Wanaume wachache wanaoliweza hili.
 
Haswaaaa na hili ndio tatizo

Kuketa taratibu zako kwenye nyumba ya mwenzio..... na ndio mifarakano inapoanzia



Wengi wetu hatuwezi kufuata mifumo tunayoikuta kwenye nyumba za wengine, tunataka tuishi tunavyotaka bila kufuata taratibu zilizoko. Na kuna wengine wanafanya kwa makusudi judt to provoke wenye nyumba na hapa siongelei ndugu wa mume, hata ndugu wa mke wanaweza kuwa tabu tupu.

Ni muhimu kuweka wazi kwa ndugu that your house is not a hotel to hang around. Ndugu watakaribishwa kusalimia au kama wana jambo la kufanya muda utakapoisha na wamemaliza kilichowaleta kila mtu arudi kwake.
 
Well said,kabila gani hilo unalolisemea hawaweki kambi?

Kuna hawa wajita mayoweee wakija kwako wanakuja 10 au 7 ongeza na family yako, wasukuma nao akikutembelea ujue wanajibeba wengiii na hawajali hata kama una chumba kimoja na sebule
Tena ukiwa karibu na hospital yaan mjini ndugu wanaopata mimba kazi yao kuja wajifungue kwako mwingine anaweza kuja na mimba ya miez 5 anakaa mpaka ajifungue
Mi nishaona familia ambayo ni wakali wageni hua hawaji sana
 
Dah unajua babu kuna watu wana ndugu wazuri....

Mfano upande wangu mume wangu ndugu zake safi sana wana upendo na hawana hila yaani mpaka nawatamanigi


Sasa njoo upande wangu (hapa ni ndugu wa kiukoo si tuliozaliwa tumbo moja) ni vigego balaaaaaaaa......... hakuna jema. Na haikuanza na sisi ilianza enzi. Wanafikia kiasi cha kufanya fujo kabisa punde shida zao zinapoisha... kutangaziwa ubaya all over.

Sasa ndugu wa namna hiyo moyo wa kumsaidia utautoa wapi???? Matokeo yake tunaonana kwenye matukio tu ili kuepusha mifarakano... harusi misiba komunyo


Pole sana ndugu yangu. Naamini hutoi na kujiumiza mwenyewe.

Kwa upande wangu, siwezi kumlaumu mke wangu kwa jinsi yoyote atakavyowatendea ndugu. Hata mimi nilikuwa na mawazo kama wanaume wengine kwamba labda hawapendi ndugu zangu. Ila uzoefu umenifunza kwamba ndugu hawabebeki, hawashibi, hawatosheki.....Kadri unavyojitesa ndivyo wanavyodai zaidi.

Dawa ni kutoa pale unapoweza na kuwahudumia wakiwa kwao!
 
binafsi nimekulia kwenye extended family, ndugu wa pande zote mbili na watu wengine baki wasiopungua wanne, lakini wote ilikuwa sheria moja, shuleshule, kazikazi, kilizo kijijini kusaidia kulima, wote tulikuwa respect na hakuna muda wa kupiga pelepete zisizo na msingi. kwangu mimi extended family haiepukiki, kikubwa ni misingi tu, hakuna upendelleo wa ndugu wa upande wowote, wote ni sawa, na mwanamke anatakiwa ajue hilo.
Nyumba nyingi kimekosekana hiki na ndio chanzo cha tatizo, mtu akikaa kwako hajaja kutembea au kukua, kama ni mwanafunzi apige shule kwa kwenda na akitoka shule anatekeleza majukumu madogo madgo ya hapo nyumba kisha usiku anaingia prepo, jumamosi ni kufuta madirisha vumbi na wengine wanafyeka na kazi zingine ndogo ndogo alafu mchana wana relax na jumapili. Lakini mkiwa pande mbili alafu kila mtu anaita watu wake na kukaa nao lazima kutakuwa na shida. Na ndugu wa kiswahili ni noma kwa kusimangana maana wengi wamekaa katika pozi la kujiona kama hapo sio kwao
 
Loh wametisha!!!!!!


Karucee; Hukopeshi?? Sio mzigo ila ni upendo wa kuzidiiiii. Usiogope, nawe funga mizigo, hamia kwa shem mkubwa. Hayo ndo maisha. Ngoja sasa, atoke, Ba mkwe na ma mkwe wanahamia. Hawajali una chumba cha pili au la.
Rafiki yangu mmoja aliletewa Ba mkwe na ma mkwe wote wanasema wanaumwa. Akawapokea, akadhani watamwonea huruma, vyumba viwili naye ana watoii wawili. Mshindo ulishuka kwani baada ya siku mbili wakaja shemeji zake 2 wa kiume na dada yao ati tunakuja kuwahudumia wazazi. Nilichokaaaa
 
nmelelewa kwenye extenda family tangu naanza shule. mwanzoni wakati bado mdogo it was hard kwa kweli, nilikuwa najiona mtoto ninaestahili matunzo ya mama bila kutambua niko kwa watu. thank God kadiri umri ulivyoenda ndivyo nilivyopatana na yule shemeji yangu. cha msingi kwa wale wenzangu ni kujitambua uko wapi kwa sababu gani. na daima kumbuka 'YATIMA HADEKI'
 
Kuna hawa wajita mayoweee wakija kwako wanakuja 10 au 7 ongeza na family yako, wasukuma nao akikutembelea ujue wanajibeba wengiii na hawajali hata kama una chumba kimoja na sebule
Tena ukiwa karibu na hospital yaan mjini ndugu wanaopata mimba kazi yao kuja wajifungue kwako mwingine anaweza kuja na mimba ya miez 5 anakaa mpaka ajifungue
Mi nishaona familia ambayo ni wakali wageni hua hawaji sana
Umetusema aisee, anyway ila kiukweli ukikaa mjini especially kama mmoja either mume au mke wazazi wake wote ni kutoka kijijini na bahati mbaya huyo partner wako ndio katokamo alafu wadogo zake wote wameishia darasa la 3A hapo tegemea wageni tu kila siku vinginevyo ni kujitahidi kutoa support wakiwa huko huko maana maisha yetu watz kama wewe hujapata extended family basi wazazi wako walikuwa wanaishi maisha extended family. Kwa ujumla hii hali ipo karibu kote especially kama unakaa katika mkoa ambao mmoja wa wanandoa anatoka hapo.
 
nmelelewa kwenye extenda family tangu naanza shule. mwanzoni wakati bado mdogo it was hard kwa kweli, nilikuwa najiona mtoto ninaestahili matunzo ya mama bila kutambua niko kwa watu. thank God kadiri umri ulivyoenda ndivyo nilivyopatana na yule shemeji yangu. cha msingi kwa wale wenzangu ni kujitambua uko wapi kwa sababu gani. na daima kumbuka 'YATIMA HADEKI'

Hivyo ndivyo inatakiwa maana wengine huwa tunaishi nao kwenye hizi familia na ukiangalia ni dogo tu alafu amefanya blunder yaani ukimkoromea tu kama ilivyo kawaida yetu wabantu kumkoromea dogo anakuona kama unamnyanyasa wakati the same kama ukimkoromea mdogo wako wa damu kwa level ile ile anachukulia poa. Kikubwa ukikaa kwa mtu kuna baadhi ya vitu hutakiwi kujilinganisha na mtoto wa anaekuweka mjini
 
Back
Top Bottom