Wananchi wa Tanzania hawataki utawala wa haki na Sheria. Matendo yao ndiyo yanathibitisha. Binafsi sioni umuhimu wa katiba mpya, hii inatosha

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,143
Habari za asubuhi!

Katiba ya Tanzania sio kikwazo cha maendeleo, katiba ya Tanzania sio kikwazo cha haki za binadamu. Yet, mapungufu madogo madogo yapo lakini si makubwa. Nchi zote duniani katiba zao zina mapungufu kulingana na muda. Hivyo nashauri marekebisho kufanyika kidogo kidogo kadri siku zinavyokwenda kulingana na muda uliopo.

Mostly wanaoimba kupigania katiba mpya ni watu wa fursa, ulaji wao siasa, uvaaji wao siasa.

Haya nauliza swali:

Ni kipengele kipi cha katiba ya JMT kikiondolewa au kuongezwa kitaleta maendeleo? Hii katiba iliyopo wananchi ndio wanaongoza kuivunja.

HAKI YA KUISHI
Hii ndio haki kubwa zaidi kuliko haki zote za mwananchi, lakini wananchi wa Tanzania ndio wa kwanza kuivunja kila siku. Kijana ameiba elfu 5 anauwawa. Mtu kaiba kuku anauwawa. Kakata dirisha la mtu usiku anauwawa.
Rushwa kwa watumishi wa umma inachochewa na wananchi wenyewe. Anakwenda kwa mwalimu mkuu Ili amwamishie mtoto wake shule hiyo yeye mwenyewe anaanza kumshawishi mkuu wa shule kuwa pesa ya maji ipo. Hospital vivyo hivyo.

Kila sehemu za umma Mtanzania akienda anajiandaa kutoa rushwa. Nimeona mwenyewe mazingira kadhaa ambayo hayakuwa na ulazima wa kutoa rushwa lakini mtu anakuambia tuchange tutoe pesa tuhudumiwe haraka. Yaani mpaka nikashangaa.

Taratibu zote ziko wazi na free lakini mtu hamwamini anayemuhudumia anamshawishi ampe rushwa.
Hii katiba iko vizuri, tuifuate kwanza hii halafu tuwaze ijayo. Ijulikane kuwa Mimi si mwanachama wa chama chochote, na umri wangu huu wa miaka 36 sijawahi kupiga kura na sifikirii kupiga kura, musije kusema nimetumwa.

Ninajielewa na siwezi kutumika kama pedi, sina njaa, najiweza.
 
Nikikumbuka wale COVID-19 wanavyoendelea kula pesa bungeni licha ya kufukuzwa kwenye chama chao, nakubaliana na wewe hata tukipata katiba mpya haitatusaidia
 
Kipengele kinacholalamikiwa sana ni kile watu wa serikali kuwa wasimamizi wa uchaguzi kinawazuia watu wa vyama vingine kushinda naamini Kwa nchi hii kikiondolewa na wapinzani wakashinda bac watakiondoa na kurudisha kilekile Ili waendelee Kila nnchi
 
Back
Top Bottom