Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,272
- 2,037
Nimekuwa nikiuliza mara kwa mara kwanini wananchi tunaishi kwa shida sana huku viongozi wakiishi maisha ya raha?
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana na Muumba wetu kwa kutupa raslimali karibu kila wilaya. Tuna mabonde mazuri kwa kilimo, milima, maziwa yenye kila aina ya samaki, mbuga za wanyama zenye aina zote za wanyama, madini mbalimbali ambayo hayapatikani popote duniani zaidi ya Tanzania.
Watalii wanamiminika, bahari tunayo, lakini vyote hivi wanafaidika ni viongozi na wabunge. Yote haya ni ubovu wa Katiba, Katiba aliyoiandaa Hayati Nyerere na viongozi wenzake 20 wakiongozwa na Mzee Msekwa na Mzee Thabiti Kombo wakati wa utawala wake bila kuwashirikisha wananchi. Viongozi waliopo madarakani wanatumia ubovu wa Katiba iliyopo kujipatia faida wao na familia zao, ndio sababu ya wao kukataa kuwapatia wananchi Katiba waitakayo, Katiba ambayo wananchi watashiriki kuandaa na kutoa maoni yao na mapendekezo yao. Viongozi waliopo hawataki Katiba mpya, kwani kutokana na wananchi kutofaidika na Katiba iliyopo, wananchi wameamua kudai Katiba mpya, Katiba ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wote na sio viongozi tu.
Ukweli Hayati Nyerere na viongozi 20 walioshiriki kuandaa Katiba iliyopo, hamkutendea haki wananchi.