Mkuu najua unakipenda sana chuo chako,lakini ukweli unabaki pale pale UDOM ni sombasomba ya wanafunzi wa aina mbalimbali aliofaulu sana,wastani na kidogo.Wengi wanaojiunga na chuo hicho ni waliokosa UDSM,SUA,MZUMBE,ARDHI UNIVERSITY,MUHIMBILI UNIVERSITY.Najua utabisha sana lakini true will prevail.Jingine ni kuwa uanzishwaji wa UDOM ulikuwa ni wa kisiasa zaidi badala ya kufuata misingi ya kawaida ya uanzishwa wa Vyuo vikuu.Kwa mfano uwezi kutaka kutoa PHD wakati chuo hakina PHD holders wa kutosha na wenye uzoefu unaohitajika.kinachohalibu zaidi ni pale wanasiasa wanapojipanga kuakikisha ifikapo 2015 chuo kiwe na wanafunzi 50000 bila kujali miundombinu ya chuo.Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anasoma shahada ya uzamili na akafanikiwa kumaliza course work mwaka 2009,lakini cha kushangaza ni kuwa kwa bahati mbaya mbaka leo hii hajapata mwalimu wa kumsimamia disertation yake ili aweze kukamilisha masomo yake.Maana yake ni kuwa chuo kilidahili wanafunzi wa shahada ya uzamili bila ya kujali miundombinu yake.Hii ni aibu kubwa kwa Chuo!!
Haya yote si kweli. Kwa taarifa yako nina ndugu yangu toka nitoke, mfanyakazi wa UDSM anasoma Masters UDOM. Huyu naye ni kilaza? UDSM inamlipia kila kitu. Pale bwana kuna walimu wenye PhD toka Urusi, India, Kenya, Ulaya na Nigeria na Watanzania waliotoka vyuo vingine. Wanao pia wanafunzi wa PhD. Ami yangu na dada zake wawili wamemaliza mwaka jana UDOM mmoja yupo VodaCom, wawili wameajiriwa Arusha kwenye mashirika binafsi. Acheni chuki zisizo na maana. Hata hivyo UDOM ni chuo kichanga sana lazima kitakuwa na changamoto nyingi.