Hoja za Waombaji Ajira za Waalimu

WEKKI

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
477
145
TAMISEMI MSAIDIENI MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KUZUIA MALALAMIKO YA NAFASI ZA AJIRA 21,200 ZILIZOTANGAZWA KADA YA ELIMU NA AFYA

Na. Matuguta Zax

Nampongeza sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili na sasa ameanza mwaka wa tatu kwa kishindo cha kumwaga ajira za kada ya Afya na Elimu 21,200. Kwa kweli mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, katika suala la kutoa ajira nyingi kiasi hiki Mama amethubutu, ameweza na anatosha kabisa tumuunge mkono 2025.

Aidha, naipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwatumikia watanzania kwa kuandaa mfumo mzuri sana wa kupokea maombi ya nafasi za ajira, mfumo mzuri wa kuchakata maombi na hatimaye kuwasambaza vijana hawa wazalendo kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kwa watanzania wenzao. Kwa kweli Kazi kubwa na nzuri mnayoifanya inampa heshima kubwa sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla. Hivyo nathubutu wazi kuwashukuru Mhe Angellah Kairuki Waziri TAMISEMI, Festo Dugange na Deogratius Ndejembi Manaibu Waziri TAMISEMI.

Pamoja na Kazi yenu njema kama timu imara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI bado usemi wa wahenga umeendelea kuthibitika kwamba Mtu hujikuna panapowasha.

Ni ukweli usiopingika kabisa kwamba vijana wanaoomba nafasi za ajira wamekuwa wakilalamikia mapungufu mbalimbali yanayojitokeza katika kuajiri. Siyo vijana pekee yao bali hata wazazi wao na walezi wao wameyalamikia mapungufu hayo ya namna gani vijana wao hupewa ajira hizo na Serikali. Kwa kuthibitisha kuwa vijana wanapitia wakati mgumu hata wabunge wao wamejitahidi kuelezea hisia na masikitiko ya mapungufu ya michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana wanaotuma maombi yao.

Kwa umuhimu wa suala lenyewe, naomba ikumbukwe kuwa mwaka 2021 zilitoka nafasi za ajira 9,675 kada ya Afya na Elimu na mwaka 2022 zilitoka nafasi za kada ya Afya ya Elimu 17,412. Katika michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana waliotuma maombi yao kulikuwa na malalamiko kama haya:-

1. Nafasi za ajira zilizotoka 2021, baadhi ya wahitimu waliomaliza 2021 kupangiwa vituo vya Kazi wakiachwa waliomaliza mwaka 2015, 2016, 2017,2018,2019 na 2020. Kutowatendea haki namna hii vijana ni kuwalazimiaha kujiingiza katika vitendo visivyofaa kama vile umalaya, ushoga na utumiaji wa madawa ya kulevya.

2. Nafasi zilizotoka tena mwaka 2022, baadhi ya wahitimu wa mwaka huo huo 2022 walipangiwa vituo vya Kazi wakiwa na sifa zile zile za rundo la vijana waliomaliza 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020 na 2021 ambao waliachwa wakiwa na vigezo vyote vinavyotakiwa. Kutokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa namna gani wahitimu hawa wazalendo kupewa haki yao wengine walichukua maamuzi magumu ya kujinyonga. Sasa inatosha tuwaonee huruma hawa vijana!

3. Kutokupewa kipaumbele wenye umri mkubwa zaidi kama vile 44, 45 ilihali kijana kama huyu asipopewa nafasi ya kipaumbele maana yake mwaka utakaofuata atakuwa nje ya vigezo. Kwa nini kuupa nguvu huu usemi wa wahenga kwamba aliyeshiba hamjui kabisa mwenye njaa!

4. Vijana wanaojitolea kwenye shule zetu wakihangaika kuwasaidia watoto wetu hawapewi kipaumbele na badala yake wanapewa kipaumbele vijana ambao wanajitolea kwenye mifuko ya wakubwa. Haki ya watoto wa masikini waliosoma kwa Shida wakauza mashamba yote ya urithi ili wapate Elimu lakini bado hata kuajiriwa napo inakuwa ngumu sijui tena wauze nguo zao za urithi ili wapate ajira? Inatosha tuwaonee huruma hawa vijana tuwape haki yao!

USHAURI WANGU TAMISEMI

Mosi, nawaomba msaidieni Rais Samia aliyewaamini kwa Moyo wake wote katika kufanya jambo hili la kuajiri watoto wa wapiga kura wake basi isafishe Serikali yake ya Awamu ya Sita iliyojizolea sifa ya Usikivu kwa kuhakikisha mnawajali watoto wa wapiga kura wake. Bado wananchi wake wanahitaji kumshika mkono Mama Samia na kuvuka naye 2025. Watendaji wa OR-TAMISEMI kataeni kuwa Kikwazo!

Pili, Kwa kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imepewa dhamana ya kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupokea maombi ya nafasi za ajira, kuyachakata na kuwasambaza vijana wa kada ya Afya na Elimu kwenye vituo mbalimbali nchini mapendekezo yangu katika ajira hizi 21,200 na zitakazoendelea kutolewa na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan ni haya:-

1. Mwaka wa kumaliza Chuo upewe kipaumbele. Kwa hiyo kundi la 2015 lianze na baadaye miaka mingine ifuate. M/kiti wa CCM aliahidi kutatua Kero kwa wananchi wake naomba TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais kutekeleza alichokiahidi kwa wapiga kura wake.

2. Umri wa mwombaji upewe kipaumbele. Anzeni kuwapangia vituo kwanza wenye miaka kuanzia 30-45 halafu wengine wafuate. Mwenyekiti wa CCM na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewapa imani kubwa TAMISEMI naomba tumieni hiyo kumsaidia Rais.

3. Wanaojitolea wapewa kipaumbele. Hili ni kundi jingine muhimu linapaswa kuangaliwa. Angalizo, kundi hili linaweza kuwa chanzo cha rushwa na kukosesha haki kwa kundi la kwanza na la pili hapo juu. Uadilifu, uaminifu na hofu ya Mungu ndiyo zinaweza kutetea haki za kundi hili.

4. Idadi ya kwamba mwombaji ameshaomba mara ngapi anakosa nafasi nalo lipewa kipaumbele. Kwa sababu kuna vijana wanaomba ajira hizi kwa mara ya kumi sasa. TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua Kero za wananchi na wapiga kura wake.

Mwisho siyo kwa umuhimu wake, kwa kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewaamini ninyi TAMISEMI kufanya jambo hili la kuwapangia vituo vijana wanaoomba nafasi za ajira 21,200 kada ya Afya na Elimu, basi ilindeni haki ya kila mmoja na mtangulizeni Mwenyezi Mungu katika shughuli hii.
 
Malalamiko hayawez kuisha kwa sababu lazima tu wawepo watakaopata na kundi kubwa litakosa
 
Naunga mkono hili , nakumbuka kuna ajira fulani zilitoka kipindi fulani kabla bashungwa hajachukua nafasi..

Ajira zile zilizingatia maelezo yako na hakukuwa na malalamiko mitandaoni . Nadhani wakifanya vile tena kila kitu kitaenda vizuri kabisa
Hiyo ni bias Mkuu acha watu waombe hata aliyemaliza 2022 Kama anafiti katika qualiffication acha aombe.
 
Hapana mkuu , hebu jaribu kuvaa viatu vya waliomaliza 2015 na 2016 , hawa walifanyiwa uharamia mbaya sana na mwenda zake maana hakutoa ajira mbaka mwaka 2018 au 2019 nadhani ( sina uwakika ).

Sasa unapomchukua huyu wa 2022 nakumuacha wa 2015 , wakati sifa wanalingana hapa unataka kujenga picha gani ? Kati ya hawa wawili ni nani kapendelewa labda ??..

Ifike mahali busara tu itumike maana hata wa 2022 anapoona wa 2015 kapata hata moyo huwa haumuumi maana anajua bado ananafasi ya kuomba tena je huyu wa 2015 unafikiri huwa anajihisi vipi ??...
 
Mkuu hiyo ni bias Kuna Jamaa yupo chuo ana miaka 39 anasoma degree and he never employed anywhere ndo anaitafuta degree yake ya kwanza so huyu Kama akifanikiwa atapata degree yake ya kwanza 2024 mwaka huyu na yeye unataka Apate Ajira mwaka gani?

Naona hoja ya umri inaleta maana lakini sio mwaka wa kumaliza chuo .
 
Uyo jamaa katokea fom6 au diploma.
 
Mkuu hiyo ni bias Kuna Jamaa yupo chuo ana miaka 39 anasoma degree and he never employed anywhere ndo anaitafuta degree yake ya kwanza so huyu Kama akifanikiwa atapata degree yake ya kwanza 2024 mwaka huyu na yeye unataka Apate Ajira mwaka gani?

Naona hoja ya umri inaleta maana lakini sio mwaka wa kumaliza chuo .
Okay , ntakuuliza swali moja mbaka anafika moaka 39 alikuwa wapi ??.

Technically mbaka mtu anakuwa na miaka 39 huku level yake ya elimu ikiwa ni diploma basi hapo it's obvious huyu mtu either alichelewa sanaaaa sanaaa kuanza shule au apa katikati kaunga unga sanaaa .

Sasa hiii ni tatizo lake yeye binafsi lakini on other side kijana ambaye kapambana na kuvuka madaraja yote vizuri na kupata degree yake mapema mwaka 2015 sasa kwanini tuendelee kumuweka mtaani kisa kuna jamaa ambaye aliunga unga elimu yake nakujikuta kamaliza 2022 akiwa na miaka 39 .?? Huoni kama hapa tutakuwa hatutendi haki kwa huyu wa 2015 ?..

Hivyo kigezo cha kumaliza mwaka ni kuzuri zaidi kukizingatia hapa kwa mtazamo wangu .
 
S

Sio kuunga unga Mkuu maisha yapo na up and down nyingi

Then Kama ulimaliza ualimu 2015 mpaka leo kama huna Ajira unabidi kutafta connection ili uingie katika Mfumo easily ukiwasikiliza wana-siasa uta. Buytime Sana.
 
Mkuu hiyo ni bias Kuna Jamaa yupo chuo ana miaka 39 anasoma degree and he never employed anywhere ndo anaitafuta degree yake ya kwanza so huyu Kama akifanikiwa atapata degree yake ya kwanza 2024 mwaka huyu na yeye unataka Apate Ajira mwaka gani?

Naona hoja ya umri inaleta maana lakini sio mwaka wa kumaliza chuo .
Umeongea vizuri sana kiongozi ndio mana me nasisistiza vigezo vya kuzingatia viwe vitatu navyo ni
1.mwaka wa kuhitimu
2. Umri was muombaji
3. Ali ya muombaji yaani mf mlemavu na nk
Vikifuatwa hivi vigezo atakayelalamika atakua na utindio wa ubongo
 
TAMISEMI MSAIDIENI MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KUZUIA MALALAMIKO YA NAFASI ZA AJIRA 21,200 ZILIZOTANGAZWA KADA YA ELIMU NA AFYA

Na. Matuguta Zax

Nampongeza sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili na sasa ameanza mwaka wa tatu kwa kishindo cha kumwaga ajira za kada ya Afya na Elimu 21,200. Kwa kweli mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, katika suala la kutoa ajira nyingi kiasi hiki Mama amethubutu, ameweza na anatosha kabisa tumuunge mkono 2025.

Aidha, naipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwatumikia watanzania kwa kuandaa mfumo mzuri sana wa kupokea maombi ya nafasi za ajira, mfumo mzuri wa kuchakata maombi na hatimaye kuwasambaza vijana hawa wazalendo kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kwa watanzania wenzao. Kwa kweli Kazi kubwa na nzuri mnayoifanya inampa heshima kubwa sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla. Hivyo nathubutu wazi kuwashukuru Mhe Angellah Kairuki Waziri TAMISEMI, Festo Dugange na Deogratius Ndejembi Manaibu Waziri TAMISEMI.

Pamoja na Kazi yenu njema kama timu imara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI bado usemi wa wahenga umeendelea kuthibitika kwamba Mtu hujikuna panapowasha.

Ni ukweli usiopingika kabisa kwamba vijana wanaoomba nafasi za ajira wamekuwa wakilalamikia mapungufu mbalimbali yanayojitokeza katika kuajiri. Siyo vijana pekee yao bali hata wazazi wao na walezi wao wameyalamikia mapungufu hayo ya namna gani vijana wao hupewa ajira hizo na Serikali. Kwa kuthibitisha kuwa vijana wanapitia wakati mgumu hata wabunge wao wamejitahidi kuelezea hisia na masikitiko ya mapungufu ya michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana wanaotuma maombi yao.

Kwa umuhimu wa suala lenyewe, naomba ikumbukwe kuwa mwaka 2021 zilitoka nafasi za ajira 9,675 kada ya Afya na Elimu na mwaka 2022 zilitoka nafasi za kada ya Afya ya Elimu 17,412. Katika michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana waliotuma maombi yao kulikuwa na malalamiko kama haya:-

1. Nafasi za ajira zilizotoka 2021, baadhi ya wahitimu waliomaliza 2021 kupangiwa vituo vya Kazi wakiachwa waliomaliza mwaka 2015, 2016, 2017,2018,2019 na 2020. Kutowatendea haki namna hii vijana ni kuwalazimiaha kujiingiza katika vitendo visivyofaa kama vile umalaya, ushoga na utumiaji wa madawa ya kulevya.

2. Nafasi zilizotoka tena mwaka 2022, baadhi ya wahitimu wa mwaka huo huo 2022 walipangiwa vituo vya Kazi wakiwa na sifa zile zile za rundo la vijana waliomaliza 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020 na 2021 ambao waliachwa wakiwa na vigezo vyote vinavyotakiwa. Kutokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa namna gani wahitimu hawa wazalendo kupewa haki yao wengine walichukua maamuzi magumu ya kujinyonga. Sasa inatosha tuwaonee huruma hawa vijana!

3. Kutokupewa kipaumbele wenye umri mkubwa zaidi kama vile 44, 45 ilihali kijana kama huyu asipopewa nafasi ya kipaumbele maana yake mwaka utakaofuata atakuwa nje ya vigezo. Kwa nini kuupa nguvu huu usemi wa wahenga kwamba aliyeshiba hamjui kabisa mwenye njaa!

4. Vijana wanaojitolea kwenye shule zetu wakihangaika kuwasaidia watoto wetu hawapewi kipaumbele na badala yake wanapewa kipaumbele vijana ambao wanajitolea kwenye mifuko ya wakubwa. Haki ya watoto wa masikini waliosoma kwa Shida wakauza mashamba yote ya urithi ili wapate Elimu lakini bado hata kuajiriwa napo inakuwa ngumu sijui tena wauze nguo zao za urithi ili wapate ajira? Inatosha tuwaonee huruma hawa vijana tuwape haki yao!

USHAURI WANGU TAMISEMI

Mosi, nawaomba msaidieni Rais Samia aliyewaamini kwa Moyo wake wote katika kufanya jambo hili la kuajiri watoto wa wapiga kura wake basi isafishe Serikali yake ya Awamu ya Sita iliyojizolea sifa ya Usikivu kwa kuhakikisha mnawajali watoto wa wapiga kura wake. Bado wananchi wake wanahitaji kumshika mkono Mama Samia na kuvuka naye 2025. Watendaji wa OR-TAMISEMI kataeni kuwa Kikwazo!

Pili, Kwa kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imepewa dhamana ya kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupokea maombi ya nafasi za ajira, kuyachakata na kuwasambaza vijana wa kada ya Afya na Elimu kwenye vituo mbalimbali nchini mapendekezo yangu katika ajira hizi 21,200 na zitakazoendelea kutolewa na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan ni haya:-

1. Mwaka wa kumaliza Chuo upewe kipaumbele. Kwa hiyo kundi la 2015 lianze na baadaye miaka mingine ifuate. M/kiti wa CCM aliahidi kutatua Kero kwa wananchi wake naomba TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais kutekeleza alichokiahidi kwa wapiga kura wake.

2. Umri wa mwombaji upewe kipaumbele. Anzeni kuwapangia vituo kwanza wenye miaka kuanzia 30-45 halafu wengine wafuate. Mwenyekiti wa CCM na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewapa imani kubwa TAMISEMI naomba tumieni hiyo kumsaidia Rais.

3. Wanaojitolea wapewa kipaumbele. Hili ni kundi jingine muhimu linapaswa kuangaliwa. Angalizo, kundi hili linaweza kuwa chanzo cha rushwa na kukosesha haki kwa kundi la kwanza na la pili hapo juu. Uadilifu, uaminifu na hofu ya Mungu ndiyo zinaweza kutetea haki za kundi hili.

4. Idadi ya kwamba mwombaji ameshaomba mara ngapi anakosa nafasi nalo lipewa kipaumbele. Kwa sababu kuna vijana wanaomba ajira hizi kwa mara ya kumi sasa. TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua Kero za wananchi na wapiga kura wake.

Mwisho siyo kwa umuhimu wake, kwa kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewaamini ninyi TAMISEMI kufanya jambo hili la kuwapangia vituo vijana wanaoomba nafasi za ajira 21,200 kada ya Afya na Elimu, basi ilindeni haki ya kila mmoja na mtangulizeni Mwenyezi Mungu katika shughuli hii.
naongeza Tamisemi kama mnasoma huu uzi tunaomba kigezo cha ufahulu mkubwa pia kiwekwe mfano form four one ya 8 , form six one ya 6 chuo gpa ya 4 ili watoto wetu wafundishwe na walimu wenye uelewa

nafasi ni chache watu ni wengii ivyo kigezo kikuu kiwe wale waliofahulu kwa kiwango cha juu nitashangaa mnamuacha wenye one ya form six au mwenye first class diploma au degree mnachukua aliepata division three au pass chuo
 
Kama umesoma vyuo. Vya Tz GPA kubwa sio mtu kuwa smart upstairs ,

Mimi mwalimu wangu aliyenifundisha civics yeye alikuwa sio Mwalimu Bali mwanasheria lakini darasa zima tulipata B za civis just imagine unapata B ya civics miaka kumi iliyopita , kufundisha mtoto ili awe smart ni kipaji na sio GPA kubwa
 
Wewe mtoa uzi ni SAUTI ya Muumba Ivi kweli unaweza kuweka grounds za kushindania ajira kwa kuchanganya pamoja vijana waliomaliza 2015 na wale wa 2022? Ni aibu. Hakuna mtu mwenye akili timamu atalalamika eti kwanini yeye kamaliza 2021 au 2020 hajaajiriwa kaajiriwa wa 2015 au 2016.

Pia niendelee kupaza sauti nikiwa kama mwanachama kabambe wa CCM. Wasiachwe wale waliosoma stashahada ya uzamili ya elimu. (Postgraduate Diploma) Tunaomba alama na Hakika ya Haki ionekane. Wengine wanamoyo wa kazi kuliko hata hao walioenda kusoma kwa maslahi.

Pongezi kwenu Tamisemi na Mhe. Rais kwa usikivu.

Pia kama mnaajiri kufuatana na wage load tunaomba muongeze kwani tangu huko nyuma tulipiga mayowe kwamba maendeleo yaguse watu sio vitu. Si mbaya ikiongezwa kuliko kwenda kwenye hati hewa. Ama kwa wachache.
 
Ko sisi wa 2022 hatuna haki na hizo ajira au
Mnayo ndio mana mmeambiwa muombe
Hla vigezo vya kupata miongoni mwenu viwe
1. Umri wa muhitimu .sababu wapo waliomaliza 2022 teyar wana umri wa miaka 40+ huyu mda c mrefu atafika 45 na kuondoka kwenye vigezo vya kuwa na sifa za kuomba ajira
2. Ali ya muombaji. Hapa tunajua pia wapo wahitimu wa 2022 wana hali mbalbali za kusaidikika mfano ulemavu n.k
3. Mwaka was kuhitimu chuo hapa ndio wengi hiki kigezo kitawatoa nje
Kea hyo mtu mwenye kigezo kimoja au zaidi ya hapo apewe ajira kama auna hata kimoja subir kidogo au kajivunje upate hata kigezo kimoja🤣
 
TAMISEMI MSAIDIENI MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KUZUIA MALALAMIKO YA NAFASI ZA AJIRA 21,200 ZILIZOTANGAZWA KADA YA ELIMU NA AFYA

Na. Matuguta Zax

Nampongeza sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili na sasa ameanza mwaka wa tatu kwa kishindo cha kumwaga ajira za kada ya Afya na Elimu 21,200. Kwa kweli mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, katika suala la kutoa ajira nyingi kiasi hiki Mama amethubutu, ameweza na anatosha kabisa tumuunge mkono 2025.

Aidha, naipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwatumikia watanzania kwa kuandaa mfumo mzuri sana wa kupokea maombi ya nafasi za ajira, mfumo mzuri wa kuchakata maombi na hatimaye kuwasambaza vijana hawa wazalendo kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kwa watanzania wenzao. Kwa kweli Kazi kubwa na nzuri mnayoifanya inampa heshima kubwa sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla. Hivyo nathubutu wazi kuwashukuru Mhe Angellah Kairuki Waziri TAMISEMI, Festo Dugange na Deogratius Ndejembi Manaibu Waziri TAMISEMI.

Pamoja na Kazi yenu njema kama timu imara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI bado usemi wa wahenga umeendelea kuthibitika kwamba Mtu hujikuna panapowasha.

Ni ukweli usiopingika kabisa kwamba vijana wanaoomba nafasi za ajira wamekuwa wakilalamikia mapungufu mbalimbali yanayojitokeza katika kuajiri. Siyo vijana pekee yao bali hata wazazi wao na walezi wao wameyalamikia mapungufu hayo ya namna gani vijana wao hupewa ajira hizo na Serikali. Kwa kuthibitisha kuwa vijana wanapitia wakati mgumu hata wabunge wao wamejitahidi kuelezea hisia na masikitiko ya mapungufu ya michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana wanaotuma maombi yao.

Kwa umuhimu wa suala lenyewe, naomba ikumbukwe kuwa mwaka 2021 zilitoka nafasi za ajira 9,675 kada ya Afya na Elimu na mwaka 2022 zilitoka nafasi za kada ya Afya ya Elimu 17,412. Katika michakato ya ugawaji wa nafasi za ajira kwa vijana waliotuma maombi yao kulikuwa na malalamiko kama haya:-

1. Nafasi za ajira zilizotoka 2021, baadhi ya wahitimu waliomaliza 2021 kupangiwa vituo vya Kazi wakiachwa waliomaliza mwaka 2015, 2016, 2017,2018,2019 na 2020. Kutowatendea haki namna hii vijana ni kuwalazimiaha kujiingiza katika vitendo visivyofaa kama vile umalaya, ushoga na utumiaji wa madawa ya kulevya.

2. Nafasi zilizotoka tena mwaka 2022, baadhi ya wahitimu wa mwaka huo huo 2022 walipangiwa vituo vya Kazi wakiwa na sifa zile zile za rundo la vijana waliomaliza 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020 na 2021 ambao waliachwa wakiwa na vigezo vyote vinavyotakiwa. Kutokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa namna gani wahitimu hawa wazalendo kupewa haki yao wengine walichukua maamuzi magumu ya kujinyonga. Sasa inatosha tuwaonee huruma hawa vijana!

3. Kutokupewa kipaumbele wenye umri mkubwa zaidi kama vile 44, 45 ilihali kijana kama huyu asipopewa nafasi ya kipaumbele maana yake mwaka utakaofuata atakuwa nje ya vigezo. Kwa nini kuupa nguvu huu usemi wa wahenga kwamba aliyeshiba hamjui kabisa mwenye njaa!

4. Vijana wanaojitolea kwenye shule zetu wakihangaika kuwasaidia watoto wetu hawapewi kipaumbele na badala yake wanapewa kipaumbele vijana ambao wanajitolea kwenye mifuko ya wakubwa. Haki ya watoto wa masikini waliosoma kwa Shida wakauza mashamba yote ya urithi ili wapate Elimu lakini bado hata kuajiriwa napo inakuwa ngumu sijui tena wauze nguo zao za urithi ili wapate ajira? Inatosha tuwaonee huruma hawa vijana tuwape haki yao!

USHAURI WANGU TAMISEMI

Mosi, nawaomba msaidieni Rais Samia aliyewaamini kwa Moyo wake wote katika kufanya jambo hili la kuajiri watoto wa wapiga kura wake basi isafishe Serikali yake ya Awamu ya Sita iliyojizolea sifa ya Usikivu kwa kuhakikisha mnawajali watoto wa wapiga kura wake. Bado wananchi wake wanahitaji kumshika mkono Mama Samia na kuvuka naye 2025. Watendaji wa OR-TAMISEMI kataeni kuwa Kikwazo!

Pili, Kwa kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imepewa dhamana ya kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupokea maombi ya nafasi za ajira, kuyachakata na kuwasambaza vijana wa kada ya Afya na Elimu kwenye vituo mbalimbali nchini mapendekezo yangu katika ajira hizi 21,200 na zitakazoendelea kutolewa na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan ni haya:-

1. Mwaka wa kumaliza Chuo upewe kipaumbele. Kwa hiyo kundi la 2015 lianze na baadaye miaka mingine ifuate. M/kiti wa CCM aliahidi kutatua Kero kwa wananchi wake naomba TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais kutekeleza alichokiahidi kwa wapiga kura wake.

2. Umri wa mwombaji upewe kipaumbele. Anzeni kuwapangia vituo kwanza wenye miaka kuanzia 30-45 halafu wengine wafuate. Mwenyekiti wa CCM na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewapa imani kubwa TAMISEMI naomba tumieni hiyo kumsaidia Rais.

3. Wanaojitolea wapewa kipaumbele. Hili ni kundi jingine muhimu linapaswa kuangaliwa. Angalizo, kundi hili linaweza kuwa chanzo cha rushwa na kukosesha haki kwa kundi la kwanza na la pili hapo juu. Uadilifu, uaminifu na hofu ya Mungu ndiyo zinaweza kutetea haki za kundi hili.

4. Idadi ya kwamba mwombaji ameshaomba mara ngapi anakosa nafasi nalo lipewa kipaumbele. Kwa sababu kuna vijana wanaomba ajira hizi kwa mara ya kumi sasa. TAMISEMI tumie njia hii kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua Kero za wananchi na wapiga kura wake.

Mwisho siyo kwa umuhimu wake, kwa kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewaamini ninyi TAMISEMI kufanya jambo hili la kuwapangia vituo vijana wanaoomba nafasi za ajira 21,200 kada ya Afya na Elimu, basi ilindeni haki ya kila mmoja na mtangulizeni Mwenyezi Mungu katika shughuli hii.
Umeandika MENGI sana itoshe kusema,
Ningepita kimya kimya ingekua sio sawa...
Well done 😊

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Wasalaam
Kwa Sasa
+267
 
Back
Top Bottom