Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

Mla Mbivu

Maandishi makubwa ya nini? kama una hoja utaeleweka hata ukitumia font size ya kawaida tu!

Lazima uwe mmoja wa product za chuo cha kata
 
Last edited by a moderator:
Wana jf napenda tu kusema machache.
Chuo kikuu kinafikia hatua ya kuwa chuo bora baada ya mchakato na muda fulani kupita. Kwa chuo kikuu dodoma, ni mapema mno kukiita cha kata au vodafasta. Muda wahitajika kuamua ubora wake. Kuona kuwa ni duni baada ya kulinganisha na vyuo vingine vikongwe nchini kama udsm si sahihi. Ukiangalia historia, hata udsm kilianza kama school tu kabla ya kuwa affiliated na uea. Lakini hatua kwa hatua kimeimarika.

Pia muhimbili (muhas) kilikuwa kidogo sana wakati kinaanza. Maprof walikuwa wa kuhesabu, lakini sasa kimepiga hatua kubwa sana.

Ukija ardhi (aru), nacho mwanzoni hakikuwa na madokta, lakini wakajiwekea malengo kuwa baada ya miaka 10 wawe na madokta wa kutosha na hali imekuwa hivyo. Aru ina maprof na madokta wengi sana.
Vivyo hivyo mzumbe, na vyuo vingine vingi unavyo vifahamu.

Sasa tukija kwa udom, twahitaji muda kuanzaia miaka kumi na kuendelea ili kuwe na ubora unaohitajika kulingana na vigezo vilivyo wekwa na tuc. Huwezi leo leo ukajenga majengo, papo hapo ukawa na walimu wenye phd na maprof. Hayo ni mambo yanayo hitaji muda. Na bila shaka yatakuwepo kwenye mipango yao ya muda mrefu na wa kati. Hatimaye tutakuwa na udom iliyo na sura kama vyuo vingine ambavyo mnadhani ni bora.

Pia labda ushauri kwa udom, katika kipindi hiki cha shida ya walimu, ni bora kuajiri walimu toka nje ya nchi. Hiyo inasaidia sana kupata ujuzi wa watu toka sehemu nyingine ya dunia. Binafsi sipendelei kufundishwa na mwalimu aliyesoma degree ya kwanza tanzania, ya pili tz, phd tz. Nahisi nakosa stadi toka nchi zingine.

Halafu lingine ni kuwazoeza wanafunzi wetu kusoma vitabu. Hilo ni tatizo sana. Wanafunzi wetu wengi hawazoezwi kusoma vitabu. Vitabu vinakufanya hata kama umesoma chuo duni namna gani, unakuwa na stadi, uelewa na ujuzi wa hali ya juu na kujiamini pia. Elimu yetu ya tz inatupa shida sana mara unapokwenda kusoma ulaya na marekani ambako wanafunzi na jamii yao na jamii yao kwa ujumla ina utamaduni wa kusoma vitabu. Unakuta wenzako wanasoma vitabu mulivyogawiwa kwenye kozi kama wanacheza vile, na mukienda kwenye semina wanakuwa fiti, huku wewe vikutesa mno kuvisoma.

Hivyo udom ni chuo kichanga sana, chahitaji muda ili kiwe bora. Kufuata mipango waliojiwekea ndiyo msingi wa maendeleo ya chuo hicho.

Umekuja na hoja nzito, nimeikubali, kilichopo nadhani kinachopelekea watu kusema cha kata ni hawa wanaudom kujinasibu wapo juu kiel;imu na kurejea kwenye majengo badala ya taaluma halisi wanayoipata.
 
hahaaa, kwa taarifa yako sisomi udom,

na sijasoma chuo bongo,

ila nawaponda nyinyi vilaza mnaosoma au mliosoma

vyuo flani flani mnaoponda wenzenu wa udom.

Hakuna kutafuta public sympathy hapa...

This shows that you are a bigger f**l than I thought
 
Mla Mbivu

Kamaliza degree mwaka huu kajiunga na masters mwaka huu na inaonekana kamaliza yupo internet sasa akili matope wakisema chuo cha kata mnakuwa mbog, masters kasoma kwa wiki ngapi huyu kisha yupo internet cafe. aaha kweli ukistaajabu ya musa utaona ya .................
 
Last edited by a moderator:
kweli kabisa, udsm wana tabia ya kuwaona vyuo vingine kuwa yebo yebo, hata mimi mwenyewe nilikuwa nafikiria kuwa udsm ni bora. Lakini kumbe zilikuwa fikra mgando kama za ccm na vyama vya upinzani. Tulizoea chuo kikuu kimoja miaka nenda rudi. Mpaka ikafikia kuwa ukisema nasoma chuo kikuu watu walijua tu ni mlimani - udms. Kwa hiyo ilikuwa chuo kikuu maana yake mlimani - udsm. Lakini sasa vyuo ni vingi. Ukisema nasoma chuo kikuu mpaka wakuulize chuo gani.

Kwa hili la udom naipongeza serikali, maana baada ya miaka kumi hakitakuwa tena kama kilivyo sasa, kitakuwa bora zaidi. Siku zote mwanzo huwa mgumu. Hivyo udom lazima ipite kipindi kigumu.

Kumbe mnakubali kuwa UDOM kwa sasa ni chuo cha kata!!!!!!!

Tulieni wala msiwe na pressure, labda baada ya miaka 5 hali itabadilika ila kwa sasa status ya UDOM ni sawa na chuo cha kata
 
Anayebisha kuwa udom ni chuo cha kata aingie kwenye mtandao asome majina ya wanachuo waliojiunga mwaka huu, asilimia kubwa wanatoka shule za kata. Pia unaweza kuni PM nikutumie orodha ya wanachuo wanaotoka katika mkoa wangu waliotoka shule za kata ulinganishe na wale waliokwenda vyuo vingine. Acheni kubishia ukweli
 
JAMANI MI SIMO..........ILA ETI NIMESIKIA SOCIALOGY inafundishwa na MHINDI....!

SASA NAJIULIZA ANAFUNDISHA SOCIALOGY YA WAPI?.........INDIA AU TZ?

MI SIMO....

Mimi ninapinga sana JF kujiita land of great thinkers... Sasa kama huyo hapo ni kweli great thinkers kweli inaonyesha hata sociology haijui na kitu gani kinasomemeshwa kwenye sociology masikini weee!! hebu niambie mtanzania gani aliyeatoa social theory?kuhusu TZ social theory nyingi sana zimetolea na kama,Karl Max,Herbert Spencer,Emile Durkheim,Ferdinand Tonnies,Robert K.Merton,Max Weber,Georg Simmel,Talcott Persons,Anthony Giddens,Max Horkheimer,Harrison white na wengineo. Sasa hao wote ni watanzania na hawajatoa theory zao kwa kuishi na jamii ya WTz sasa nashangaa sana vyuo vyetu hata kabla ya huyo muhindi vinazitumia theory zao na vitabu vyao...Kitu chengine naomba Viongozi wa JF suala la nani mtu kuwa mwanachama bora liangaliwe tena bora atu awasilishe maombi ikiwe hard copy ya IQ score results...
 
Mkuu kuna tofauti kati ya ISP na internet cafe, Unajua hivi ni vitu vya technologia. ISP ni internet Service Provider kama vile African Online, na wengine wote wanaounganisha wateja/watumiaji wa kawaida/mashirika katika mtandao wa Internet. Siyo kama pale internet Cafe za posta, hila hawa ndio wanaleta huduma ya mtandao katika sehemu za Internet cafes na makampuni mbali mbali. Kwa hilo unaombwa kufuta usemi wako.

Mi nilidhani anafany kwa Billy Gates kumbe hata african online ni ya internet service provider anaye heshimika
 
Mimi ninapinga sana JF kujiita land of great thinkers... Sasa kama huyo hapo ni kweli great thinkers kweli inaonyesha hata sociology haijui na kitu gani kinasomemeshwa kwenye sociology masikini weee!! hebu niambie mtanzania gani aliyeatoa social theory?kuhusu TZ social theory nyingi sana zimetolea na kama,Karl Max,Herbert Spencer,Emile Durkheim,Ferdinand Tonnies,Robert K.Merton,Max Weber,Georg Simmel,Talcott Persons,Anthony Giddens,Max Horkheimer,Harrison white na wengineo. Sasa hao wote ni watanzania na hawajatoa theory zao kwa kuishi na jamii ya WTz sasa nashangaa sana vyuo vyetu hata kabla ya huyo muhindi vinazitumia theory zao na vitabu vyao...Kitu chengine naomba Viongozi wa JF suala la nani mtu kuwa mwanachama bora liangaliwe tena bora atu awasilishe maombi ikiwe hard copy ya IQ score results...

Mi nadhani unapofundisha social theory sometimes inapendeza ukifananisha na mazingira ya jamii husika ukichukulia kwa watanzania wengi hawajapata bahati ya kwenda kuona maisha ya wenzetu.
Nakumbuka miaka ya 2000 mwanzoni kulikuwa na workshop ambayo moja ya watoa mada alitokea canada akashangaa sana eti mpaka leo watu wanasoma vicious cycle, akasema imepitwa na wakati kwa taifa kama Tanzania
 
Wana jf napenda tu kusema machache.
Chuo kikuu kinafikia hatua ya kuwa chuo bora baada ya mchakato na muda fulani kupita. Kwa chuo kikuu dodoma, ni mapema mno kukiita cha kata au vodafasta. Muda wahitajika kuamua ubora wake. Kuona kuwa ni duni baada ya kulinganisha na vyuo vingine vikongwe nchini kama udsm si sahihi. Ukiangalia historia, hata udsm kilianza kama school tu kabla ya kuwa affiliated na uea. Lakini hatua kwa hatua kimeimarika.

Pia muhimbili (muhas) kilikuwa kidogo sana wakati kinaanza. Maprof walikuwa wa kuhesabu, lakini sasa kimepiga hatua kubwa sana.

Ukija ardhi (aru), nacho mwanzoni hakikuwa na madokta, lakini wakajiwekea malengo kuwa baada ya miaka 10 wawe na madokta wa kutosha na hali imekuwa hivyo. Aru ina maprof na madokta wengi sana.
Vivyo hivyo mzumbe, na vyuo vingine vingi unavyo vifahamu.

Sasa tukija kwa udom, twahitaji muda kuanzaia miaka kumi na kuendelea ili kuwe na ubora unaohitajika kulingana na vigezo vilivyo wekwa na tuc. Huwezi leo leo ukajenga majengo, papo hapo ukawa na walimu wenye phd na maprof. Hayo ni mambo yanayo hitaji muda. Na bila shaka yatakuwepo kwenye mipango yao ya muda mrefu na wa kati. Hatimaye tutakuwa na udom iliyo na sura kama vyuo vingine ambavyo mnadhani ni bora.

Pia labda ushauri kwa udom, katika kipindi hiki cha shida ya walimu, ni bora kuajiri walimu toka nje ya nchi. Hiyo inasaidia sana kupata ujuzi wa watu toka sehemu nyingine ya dunia. Binafsi sipendelei kufundishwa na mwalimu aliyesoma degree ya kwanza tanzania, ya pili tz, phd tz. Nahisi nakosa stadi toka nchi zingine.

Halafu lingine ni kuwazoeza wanafunzi wetu kusoma vitabu. Hilo ni tatizo sana. Wanafunzi wetu wengi hawazoezwi kusoma vitabu. Vitabu vinakufanya hata kama umesoma chuo duni namna gani, unakuwa na stadi, uelewa na ujuzi wa hali ya juu na kujiamini pia. Elimu yetu ya tz inatupa shida sana mara unapokwenda kusoma ulaya na marekani ambako wanafunzi na jamii yao na jamii yao kwa ujumla ina utamaduni wa kusoma vitabu. Unakuta wenzako wanasoma vitabu mulivyogawiwa kwenye kozi kama wanacheza vile, na mukienda kwenye semina wanakuwa fiti, huku wewe vikutesa mno kuvisoma.

Hivyo udom ni chuo kichanga sana, chahitaji muda ili kiwe bora. Kufuata mipango waliojiwekea ndiyo msingi wa maendeleo ya chuo hicho.

Mawazo mazuri sana. Big up
 
ok tufanye nini sasa ukiwa ni mmoja wa wapingaelimu ndani ya JF SEMA nini kifanyike ili tuondokane na kauri yako isiyoweza kubalika daimaaa?

mapinduziiii daimaaaaa

Ilikichuikua almost 10 years UDSM kutambulika na kusimama yenyewe hiyo ikiwa na sababu wengi wa graduates walitakiwa kujenga taifa na sio kufundisha na wengi ya malecturers wa kipindi hicho walikuwa wageni.
Leo hii UDSM ni kinashika namba 10 to 13 kwenye grading ya vyuo Afrika ikiongozwa na SA na EGYPTY, nadhani hata wanaojaribu kuharibu sura ya UDSM hawatafuti ukweli wa kimataifa.
Tusubiri kama miaka mitano ili UDOM IWE KAMA HAO MIMI NIMEFUNDISHWA NA WATU WALIOTOKA UDSM KUJA UDOM KAMA DR AME AND BAISI.
Moja ya matatizo ya vyuo visivyotambulika kimataifa ni kwamba huwezi kudahiliwa kwenye vyuo vikubwa kama havard, denver na vinginevyo duniani
Kijikite kwenye kusomesha waalimu na kupelkeka wanachuo kwenye masomo ya vitendo

Kisha chuo kijizuie kujiingiza kwenye siasa.
 
wawili kati ya walimu muhimu sn udom ni kaka mmojaaliwahi kuwa katibu wa serikali ya wanafunzi Tumaini, huyu bwana alisoma Bachelor ya Tourism akamaliza mwaka 2008 na hadi sasa hajasoma masters anasubiri skolashipu. Mwingine ni mdada alisoma kozi kama ya huyo katibu sa serikali ya wanafunzi wa Tumaini, mbaya zaidi Curriculum ya hiyo tourism imekaa kimagumashi sana. UDOM ni chuo cha kata tu

muongeze na mwl.kapinga wa loyola high school mabibo. O level na A level history.Sasa lecturer wa udom. Wakat udom inafunguliwa uyu alihama na wanafunzi wake wa sekondari ya loyola. Yeye anaenda kuwa mwl wao wanaenda kuwa wanafunzi . Kama unabishi muulize Teri gilead aliyegombea urais udom mwaka jana,nae ni mwanafunzi wake na waliama pamoja. Sa si bora wangekaa pale pale loyola na wengne wakakaa Tandaimba, Tumain University alaf wakayaita Udom ila HQ ikawa Dodoma? Mleta mada kusema ukweli si kupinga,kupinga ni kukaa ukweli. Jf si wapinga maendeleo ni wapinga ukweli na hawataki kusikia hata Phd za kwenye Gift pepa kama za mh.MSAFIRI a.k.a traveller!
 
Tatizo ukweli mchungu..kuwa waanzishaji wa kitu sio dhambi..walioanzisha UDOM (wanafunzi) sio dhambi kukubali kuwa chuo bado kichanga..kinachoponza tu ni hawa wanasiasa..hata serikali kuanza kutafuta upenyo wa kukitumia chuo hicho vibaya (eg wanafunzi kuchanga hela kumchukulia fomu mgombea, kufanya maandamano ya kipuuzi kushadidia maamuzi ya kipuuzi ya serikali, n.k)..cha msingi 'Tumieni muda mwingi kujifunza kutoka vyuo vingine, ndipo mtakapotambua "VYUO VIKUU NI SEHEMU AMBAPO MAWAZO HURU NA IMARA YANAPOKOMAZWA'....taratibu tu UDOM nayo siku moja itakuwa chuo imara na kongwe..stop being Arrogants!
 
Mweee thambi thangu mniachie
 
Mimi ninapinga sana JF kujiita land of great thinkers... Sasa kama huyo hapo ni kweli great thinkers kweli inaonyesha hata sociology haijui na kitu gani kinasomemeshwa kwenye sociology masikini weee!! hebu niambie mtanzania gani aliyeatoa social theory?kuhusu TZ social theory nyingi sana zimetolea na kama,Karl Max,Herbert Spencer,Emile Durkheim,Ferdinand Tonnies,Robert K.Merton,Max Weber,Georg Simmel,Talcott Persons,Anthony Giddens,Max Horkheimer,Harrison white na wengineo. Sasa hao wote ni watanzania na hawajatoa theory zao kwa kuishi na jamii ya WTz sasa nashangaa sana vyuo vyetu hata kabla ya huyo muhindi vinazitumia theory zao na vitabu vyao...Kitu chengine naomba Viongozi wa JF suala la nani mtu kuwa mwanachama bora liangaliwe tena bora atu awasilishe maombi ikiwe hard copy ya IQ score results...

kweli kizbao noma unapinga jf kuwa land yaG.thinkers alaf unasign in. We ulitaka ukute akina nani? Unasema Tz hamna socioligist theories?unajua maana ya sociology au ?sociologist uliowataja wanagusa moja kwa moja jamii ya Tz au una maana Tz ina tamaduni za watu uliowataja tu? Usiwe mzembe zunguka ktk maktaba uwajue wasomi wetu,sio kukaa vijiwen ukisimuliwa majina oh karl marx,weber! Du wee noma! Tz ina tamadun zake tofauti na unovodhani! Jf ni jamvi makini mkuu. Usipokubaliana nao haimaanishi status yao inapotea. Unataka tuanze kupimana IQ kuwa kigezo cha kuingia Jf? Una maana ianze kuwa discriminative! Je IQ za wageni wataozidi ata jf mods watapimwa na nani,au unadhan IQ yako ndo best of all? Au basi jf ikupe ajira uanze kuchuja unaowataka wewe! Wapo wengi kama wewe pindi wanapokabwa na hoja wanakimbilia kuuliza aliyekualika ni nani?ajabu! Pia wapo wanaotaka hard kopi za vyeti,IQ n.k vp mtaishia kuangalia hardkopi wakat watu wanajenga hoja. Wake up man,discuss!
 
Sawa mkuu nakubali!
Tatizo ukweli mchungu..kuwa waanzishaji wa kitu sio dhambi..walioanzisha UDOM (wanafunzi) sio dhambi kukubali kuwa chuo bado kichanga..kinachoponza tu ni hawa wanasiasa..hata serikali kuanza kutafuta upenyo wa kukitumia chuo hicho vibaya (eg wanafunzi kuchanga hela kumchukulia fomu mgombea, kufanya maandamano ya kipuuzi kushadidia maamuzi ya kipuuzi ya serikali, n.k)..cha msingi 'Tumieni muda mwingi kujifunza kutoka vyuo vingine, ndipo mtakapotambua "VYUO VIKUU NI SEHEMU AMBAPO MAWAZO HURU NA IMARA YANAPOKOMAZWA'....taratibu tu UDOM nayo siku moja itakuwa chuo imara na kongwe..stop being Arrogants!
 
mkuu kuna tofauti kati ya isp na internet cafe, unajua hivi ni vitu vya technologia. Isp ni internet service provider kama vile african online, na wengine wote wanaounganisha wateja/watumiaji wa kawaida/mashirika katika mtandao wa internet. Siyo kama pale internet cafe za posta, hila hawa ndio wanaleta huduma ya mtandao katika sehemu za internet cafes na makampuni mbali mbali. Kwa hilo unaombwa kufuta usemi wako.
#

mwambie huyo kilaza, imebidi nikae kimya kuliko kumjibu mtu anayeandika asichokijua.

Ahsante mkuu.
 
Hivi nyie mnaokiponda udom mnakunya akili au?
Hamfikirii kuwa kodi zenu mnazokatwa kwenye mishahara
yenu zimechangia kujenga pale?
Badala mjivunie angalau kodi zenu zimefanyia jambo la heri bado linalalamika.
mimi kukatwa kod yangu aimaanish nisie kitu ata km kibovu
kukatwa kod ni tofauti na huduma niliyokatwa kod yangu
NI CHUO CHA KATA FULL STOP.KOD YANGU INATEKETEA,
 
Wewe Jackbauer wacha kutudanganya Katika Chuo ambacho walimu wake wengi hawana sifa ni MUHAS.. kwani hao wanaojiita ma sn lecture wengi wao hawana PhD na hasa kwenye clinical medicine ma Pro ni wachache sana hivi juzi tu watu ndiyo wamepewa huo kuwa ma Ass pro lakini ukiangalia CV zao zinatia kichefu chefu kwani wengi wao publication 0.na walimu wenye master kwa clinical medicine ndiyo wanaotoa lecture na hao hao huwa wanawasimia wanafunzi wa master...na katika basic science wako wenye MD tu basi na wanasomesha je MUHAS pia chuo cha kata..
Na kuhusu jambo jengine ambalo huna hana idea nalo USA in general more 30% ya wananchi wake wana degree ya kwanza na kuendelea. na katika utafiti uliofanyika karibuni mji ambao una degree holder kidogo basi ni 19% ya population ya mji huo.kwa hivyo kijana kabla ya kusema kitu fanya utafiti wako.mimi nimeshafundisha MUHAS..

wewe unaijua MUHAS Kweli?hii ilikuwa MUCHS chini ya UDSM,haikuanzishwa kwa papara kama UDOM,Lecturers wake ni wazee wa zamani waliotoka university ya East Africa.Ukiona M.D kwenye kufundisha ni Tutorial ass.maprofesa wapo na hao unaosema wamepata juzi ni wawili tu.kwa taarifa yako nawafahamu M.D(MUHAS sio MUCHS graduates) walioko UDOM ambao kwa sasa wanasoma masters Bugando ili waje kufundisha watoto wetu hapo UDOM,ingawa watasaidia lakini sidhani kama watadeliver the same as prof premji,mbembati,pallangyo,matuja,karim,lyamuya e .t .c.
Nadhani u-mvivu wa kusoma la sivyo sielewi kwa nini huoni publications za watu wa MUHAS,try to visit pubmed,EA MED JOURNAL n.k ili u-appriciate kazi za kitanzania.inawezekana ulifundisha MUHAS,labda ulikuwa unafundisha midwifery au lab techn. Vitu ambavyo havifundishwi hata na degree holder.mwalimu mzuri wa clinical medicine ni yule aliyepractise thats why kuna walimu wa basic science na clinicals(medicine sio sociology or politics).ukitoa mifano rejea ya kitafiti ni lazima uangalie maeneo yote yaani duniani(worldwide)africa au E.A,sio kutuwekea data za USA Pekee.
you have to be serious when discussing serious issues like education,stop yelling like a stupid politician.
Shule za kata,vyuo vilivoibuka kama uyoga vikiongozwa na UDOM ni kosa jingine ambalo madhara yake yataonekana mda si mrefu.
 
Back
Top Bottom