Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

Tutajieni vyuo mlivyosoma nyie. Kwa maneno yenu mmeanza kukubaliana na ukweli

Wewe nenda kwenye internet na angalia rank ya vyuo vya Tz Duniani kama nilivyosema hapo ni uongo au not vyuo tulivyosoma sisi haitokusaidia.lengoni kujua jinsi gani elimu katika nchi yetu iko ndogo kiasi gani na tujadili nini kifanywe ili itatuliwe.kwani wengi wetu tuko kwenye ndotoni kwa kuzania ya kuwa tuko juu kielimu kama watu wanavyojisifia kwa sababu ukisha kujiona uko top unakuwa huna chance ya ku improve...sasa we need reality check ya kujua sisi tupo wapi?
 
Inawezakuwa hivyo kwani kufahamu kitu ni relative...Pro Aboud Hasomeshi tena..Na kitu kimoja niangalizie sehemu moja tu ya zangu niliyounga mkono UDOM kutoa. mimi nilizungumzia MUHAS baada ya kukitolea mfano wewe ya kuwa kinastahili. mimi maeleze yanu yote hapo MUHAS na UDOM ya wale wale tu na ukienda katika Private University zote Tz hali inatisha kuliko hivyo vya serikali.kusema ukweli Tz hatuna qualifyied lectures wa kutosha na hilo linajulika.huwezi kusema kwa sasa ilivyo nchi yetu tu enrol university 2500 tu. kamailivyokuwa kabla ya 2001.mwisho ninasema kama UDOM ni chuo cha kata basi hivyo vilivyobakia ni mkumbo mmoja kama mtu ana 5 ni Fna 10 ni F vilevile.

naona sasa unaachana na scientific facts na unaamua kusiriba tu.toa vigezo vya hiyo grading uliofanya.napata wasiwasi hata kwenye hiyo research unayofanya utaacha majibu halisi na kubandika hisia zako.
 
Wewe nenda kwenye internet na angalia rank ya vyuo vya Tz Duniani kama nilivyosema hapo ni uongo au not vyuo tulivyosoma sisi haitokusaidia.lengoni kujua jinsi gani elimu katika nchi yetu iko ndogo kiasi gani na tujadili nini kifanywe ili itatuliwe.kwani wengi wetu tuko kwenye ndotoni kwa kuzania ya kuwa tuko juu kielimu kama watu wanavyojisifia kwa sababu ukisha kujiona uko top unakuwa huna chance ya ku improve...sasa we need reality check ya kujua sisi tupo wapi?

Ndicho tunachofanya hapa tukiwa na uhakika wahusika wenye bajeti wanasoma na kufanyia kazi bila kusubiri migomo mingine. Kwamba elimu yetu iko hoi kila mtu anajua lakini tunapotoa changamoto hapa tusiitwe wapinga maendeleo wa JF. Kama ni kusifia wapo walioajiriwa kwa kazi hiyo kina Cosmas Mwaisobwa wa HESLB, kina Salva Rweyemamu, Premji Kibanga, Gazeti la Uhuru, kina Prof Kikula, Mukandala na wengine. hatuwezi kuogopa kumwambia mfalme kwamba hajavaa nguo kwa sababu hapendi kuambiwa ukweli.
 
Jamani lets face it, UDOM needs to do better than what is doing now. Ukweli ni kwamba..kwa upande wangu...kitendo cha UDOM kugawa PhD kwa Kikwete wakati hawajawahi kutoa PhD ya kiukweli kwa mwanafunzi aliyeisomea pale..inaonyehsa ni jinsi gani hiki chuo kilivyo na na ufupi wa kufikiria. Ndo maana watu wanakidharau. Sijui ufundishaji wake..but I trust Prof. Kikula is a good professor. Otherwise..UDOM itaendelea kuitwa chuo cha kata mpaka waprove otherwise.

Na wanafunzi wake waanze kubehave responsbily siyo kutoa waraka wa kuissupport CCM simply because they want to be seen by the powers that be.
 
Mliosoma vyuo bora pitieni hapa chini halafu mtutajie vyuo mlivyosoma huko ughaibuni
QS World University Rankings Results 2010 | Top Universities
Hiyo link uliyotoa hapo juu inaweza kuwa usivione vyuo vya tz hao ni waingereza wamejipendelea lakini angalia link hii hapa utaona top university in africa na rank yao duniani hapa kipo UDSM tu.
Ranking Web of World universities: Top Africa.
na Link hii hapa nyengien top university katika sub sahara africa.vipo UDSM,SUA,Open university,IFM,MUHAS na KCMC na usiwache kuangalia rank zao duniani.
Ranking Web of World universities: Top Sub-Saharan Africa
Sasa mtu ataamuwa mwenyewe wapi ilipo elimu yetu..
 
ushauri wa bure kwa wanaosoma UDOM,haina haja ya kujipendekeza wala ku-prove anything to JAMII FORUMS,u just do what is best for ur university,and when there is something to be proud of,TZ n the world will be ready to cheer,nakushauri u quit JF if u r from UDOM,hawa jama watazidi kukukatsha tamaa,they 'll never understand u
 
UDOM ni chuo kikuu cha kata. Ni kimbilio la wanafunzi vilaza (kama ilivyo watoto vilaza wa sekondari wanavyokimbilia sekondari za kata). Ubora wa chuo sio majengo. Uzuri wa mkakasi...

Ninamfahamu mwalimu mmoja wa vodafasta amepata nafasi ya kuchukua digrii. Huyu lazima ataimba sifa za chama chetu kile kile Che Che Mi.

Pia hata waalimu wengi wao ni bogus tu.

Udom deserves this title Chuo cha kata.
 
sio hivyo anko sam. Magreat thinkers wengine nashndwa kuwaelewa.
Bora watu waende pale wapate data kamili ndio waje kumwaga upupu hapa.
Kuna watu walikosa nafasi pale hawana qualification. Kuna wengine walikuwa na multiple admission ila wakaenda udom.
Hivi tunataka watu wote wasome udsm tu au?
Mnajishaua kusema walimu sijui nini... Nani asiyejua kuwa uhaba na ubora wa walimu ni vyuo na shule karibia zote tz.
Hata huo uzuri wa majengo yao pia mnaponda! Jamani mnataka wasome chini ya miti ndio msifie au?
Vijana wa dom msihofu wala nini!

Hapo umenena, maana hata huko Duniani tunako amini kuna elimu bora, vile vile kuna vyuo vya hadhi tofauti tofauti lakini bado kuna maendeleo kuliko sisi. Huu ni ufinyu wa mawazo tu watu bado wamekariri UDSM ndo chuo bora kuliko vingine, mbona kinatoa pia MAFISADI? Watu wasiona waadilifu WEZI wa PESA za UMMA wala hawawazi kuleta maendeleo nchini, wao wanawaza KUIBA tu kwa namna yeyote ile!

Mfano; Mzee wa Vijisenti amesomea hapo UDSM lakini kama taifa tunaweza kujivunia nini kutoka kwake? Amekwisha lifanyia nini taifa hili mpaka tuseme hii ndo product bora ya Mlimani? WIZI mtupu! Mifano ni mingi kwa kuangalia product za Mlimani.Heri wameanzisha UDOM labda product zake zinaweza kuwa na graduate wazalendo wengi zaidi kuliko nguli wezi zaidi toka Mlimani.
 
Mtazamo wangu kwa vyuo vya tanzania:

1. Ifm, cbe, mwl. Nyerere, social works, kiu:

hivi ni vyuo vya kijiji

(havijafikia kata)

2. Udom, st. Johns, st. Augustine, muslim morogoro:
hivi ni vyuo vya kata

3. Tumaini, mzumbe, iaa, mist:

hivi ni vyuo vya tarafa

4. Udsm, muhas, ardhi,sua:

hivi ni vyuo vya wilaya

kwa kifupi bado hata hivyo tunavyoviona vina unafuu bado ni bomu, elimu ya bongo iko chini ndio maana chuo cha kwanza tanzania duniani hakipo hata 1000 bora.

ha ha ha! Nimependa mchanganuo wako. Vipi vyuo ulivyoviacha?
Havijaingia hata level ya ukijiji nin?
 
Mwaka jana nilipokuja Tanzania nilitembelea vyuo vitatu, Sekuco, Stefano Moshi Memoria University and UDOM. Ukweli ni kwamba hivi vyuo bado havina hadhi ya kuwapa wanafunzi changamoto.

Chuo kikuu ni sehemu ambayo mwanafunzi anapewa uwezo kwa kufikiria nje ya boxi, na walimu wenye ubora wa juu ndio chombo pekee ambacho kinaweza kuchangia hili. Pale Sekuco niliona baadhi ya graduate wanafundisha graduate wenzao, hii ni hatari. Mwanafunzi wa masters anaweza kufundisha kama tuu ana experience ya kutosha katika kazi. Mimi ni masters degree na nina wadau wenzangu ambao wana 20 years experience ya management basi wanatoa lecture kwenye university kubwa. Lakini ni sababu ya experience zao, and nothing more. Vingenevyo wangekuwa MaTA's tuu.
 
Me pia huwa nashangaa iweje watu waseme udom ni chuo cha kata! Kiukwl chuo hiki cku zinavyokwenda kitakuwa bora sana,ni kwl vyuo vingi Tanzania (c udom pekee) kuna upungu mkubwa wa wahadhiri,ili kutatua tatizo hili udom huwaendeleza kielimu waliowaajiri. mwaka juzi nikiwa udsm nilimsikia prof. Tibaijuka(waziri wa makazi alishawi fundisha udsm) wakati wa wiki ya kigoda cha mwalimu akisema hata udsm ilipoanza haikuwa na waadhiri wenye sifa,watu wengi wakasomeshwa nje walau mambo yakabadilika..vivyo vivyo udom itakuwa nzuri its just the matter of tym..cha muhimu wazalendo msome kwa bidii mkiwa undergraduate ili muweze kupata gpa inayohitajika (3.8 and above) ili mkihitajika muweze kuajiriwa,wengi wagraduate mitaani hawana gpa hiyo thus y kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri nchi nzima.

Hiyo GPA 3.8 ndo ina nini?Yaani mtu akimaliza na hiyo GPA ndo anakuwa mwalimu mzuri ama?Mimi kwanza hata huwa sielewi kwanini huwa wanang'ang'ania hiyo GPA.Inapofika suala la kutayarisha wahadhiri wa baadae nafikiri inabidi waende beyond 3.8 GPA...hiyo GPA inaweza kuwa moja ya criteria ila inabidi waende zaidi ya hapo.Maana unakuta watu wana hizo GPA na hata kuji-express hawawezi ni upuuzi mtupu wapo wapo tu...nafikiri ni muhimu kuangalia na qualities nyingine zaidi ya hiyo GPA tu!
 
Kwa mara nyingine nasema

wanaoponda UDOM na Mataahira na inabidi wakapimwe akili,

wanapelekwa na hisia na chuki na wivu vimewatawala,

nimejaribu kufanya utafiti nikaona wote wanaoponda UDOM

ni vilaza especially wanaotoka katika vyuo flani flani

ambavyo kwa sasa vinaonekana kufunikwa na UDOM,

mdogo wangu amemaliza UDOM kwenye college ya I.T mwaka huu,

na alipata multiple admission moja ya UDSM engineering,

ila akaamua kwenda UDOM kusoma I.S na miaka yote aliyosoma pale

alifanya field na sasa anafanya kazi kwenye kampuni flani kubwa

hapa dsm inayotoa huduma za Internet (ISP),

na yuko nondo zaidi hata ya dogo wangu mwingine aliyemaliza

UDSM Computer Science mwaka jana.

Kwa kifupi ukiona mtu mwenye Bachelor kakabidhiwa course afundishe

labda anafundisha watu wa Diploma au Certificate,

lakini hakuna m2 mwenye Bachelor anayesimamia somo lolote UDOM,

zaidi ya kusimamia semina.

Narudia tena nyie mnaoponda UDOM bila kufahamu ukweli

ni wanafiki, mataahira, wapumbavu na wazandiki

msiopenda maendeleo ya elimu katika nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki UDOM.
Ndugu yangu mtu anaekataa mlimani kwenda UDOM nitamshangaa sana, wengi ni wale waoga, unajua chuo kama UDSM hakina mchezo, u need to be really smart to survive, watu wanakwenda Dodoma wanajua ni mteremko lakini si kwa sababu ya ubora wa chuo, huwezi kufananisha UDOM na UDSM otherwise ur not ok upstairs
 
Mkuu kuna tofauti kati ya ISP na internet cafe, Unajua hivi ni vitu vya technologia. ISP ni internet Service Provider kama vile African Online, na wengine wote wanaounganisha wateja/watumiaji wa kawaida/mashirika katika mtandao wa Internet. Siyo kama pale internet Cafe za posta, hila hawa ndio wanaleta huduma ya mtandao katika sehemu za Internet cafes na makampuni mbali mbali. Kwa hilo unaombwa kufuta usemi wako.

Kama kazi ya ISP ni provide interned service....unaitofautishaje na internet cafe?

Je kufanya kazi kwenye ISP unayosemea inahitaji degree ya IT?

Wangapi wamesoma high schools na colleges akapata IT certificate na wanafanya kazi hii?

Mimi nadhani ujaribu kudadavua hoja yako.

Hata hivyo haibadilishi UDOM kuwa chuo cha kata

1. shule ya kata ni kimbilio la waliokosa matumaini au nafasi sehemu zingine...UDOM ilipoanza sio wanafunzi tuu bali hata waalimu toka vyuo mbalimbali mf SUA, UDSM na MU walikimbilia huko sasa wanalia....wao wenyewe wanasema CHUO NI YEBOYEBO.

2. Mtoto wa shule ya kata hana hela nyingi (ametoka familia maskini) chochote anachopata anaridhika...ikiwemo kufika f4 na kupata 0....UDOM ilijidhihirisha baada ya yule mwanafunzi wa UDOM kuenda kugombea ubunge kwa Nkono alafu akapewa hela akachomoa jina na kwa kuwa uewewa wake sio mkubwa basi alienda na simu ya msg zile kwenye office za chadema. Nadhani mtu wa MU/UDS/SUA au vingine angeitupa simu mbali kabisa.

3. Shule ya kata wananafunzi hawana madawati, vitabu etc, wakiahidiwa hata visivyotekelezeka kama alivyoahidi internet na laptom JK kule kibosho wanafunzi wa shule ya kata waridhika....UDOM wameitisha mgomo, mawaziri wameenda palekinyemela..wamewaahidi watatekeleza wakarudi madarasani...where,,,,this is imposible in a true university

ninatamani kuendelea...lakini lol......give me break...UDOM WILL ALWYS BE SHULE YA KATA hadi hapo watakapojipambanua vinginevyo!
 
Guys be proud with this a.k.a otherwise you will be burning with anger!

Jina ni jina halitoki wala halitaisha, furahieni, sisi wahandisi huwa tunawaita wasiowahandisi MANGWIN and they are proud of this

msipokubaliana na hili na swa na kusema you are not among scholars, vyuo vingi duniani vina aka, na UDOM must be one of them

study hard, prove to people that you are not chuo cha kata, work hard and do soemthing differently from other graduates.

mkipiga kelele eti tunaitwa chuo cha kata is childish and you will never erase this, ni swa na jina la utani la mtu, ukitania akikasirika ndio unataniwa zaidi ni nature ndivyo tulivyo

have a nice study at chuo cha kata
 
UDOM ni chuo kikuu cha kata. Ni kimbilio la wanafunzi vilaza (kama ilivyo watoto vilaza wa sekondari wanavyokimbilia sekondari za kata). Ubora wa chuo sio majengo. Uzuri wa mkakasi...

Ninamfahamu mwalimu mmoja wa vodafasta amepata nafasi ya kuchukua digrii. Huyu lazima ataimba sifa za chama chetu kile kile Che Che Mi.

Pia hata waalimu wengi wao ni bogus tu.

Udom deserves this title Chuo cha kata.
Upeo wenu mdogo ndio uanonyesha kuwa UDOM ni chuo cha kata,mfano nikikuuliza wewe niambie features gani zinazo determine ubora wa chuo?
 
Ni chuo pekee ambacho adi walimu wa shule ya msingi nao ni ma lectures, sasa ni kwa nini kisiwe chuo cha kata
Kama UDSM ndio iantoa product za namna hii sishangai kwanini mnakiita chuo cha Dodoma cha kata
 
kuna watu ni bora wakae kimya sababu hawajui walisemalo kwani unaweza vipi kufananisha UDOM na vyuo vingine Tanzania! Ata kwenye ulimwengu wa vyuo vikuu bado akijajulikana tumeshaanza kikiponda sisi wenyewe ivi kweli tutafika ktk kuendesha gurudumu la maendeleo
Mi napongeza CDM kwani hiyo ndio ilikuwa sera yao kujenga UDOM basi kwa serikali ya CCM ikaitekeleza basi tusirudishane nyuma tujenge taifa letu.
 
1. Watu wengi wanatambua kuwa kumekuwa na ulazimishaji wa mambo ili tu mradi chuo hiki kianzishe course nyingi hata zile ambazo hakijawa na uwezo nazo. Wanataka kufundisha kila kitu eti Udaktari,uhandisi, sayansi ya komputa,jamii,ngoma za kienyeji, elimu, kichina, kisukuma,kizaramo,kikwere etc. Hiki kitu hakiwezekani madhara yake ni kuwa na wahitimu wabovu tu. Mimi nawajua walimu kutoka vyuo vikuu vingine wameajiriwa kama wanataaluma fulani lakini kwa historia wao ni wanataaluma wa taaluma tofauti na waliyoajiriwa UDOM, hivyo kwa mtindo huo msitarajie matokeo mazuri.
2. Chuo kina vikozi vidogovidogo ambavyo ni kama somo moja tu kwenye vyuo vingine, vyanini hivi?
3. Serikali inafanya makusudi ya kukipendelea UDOM na kuuwa vyuo vingine kwa kuwapa masilahi mazuri zaidi wahadhiri wa UDOM, hivyo kuhamia chuo hicho hata katika taaluma ambazo si zao au kuwa viongozi tu badala ya kufundisha.

4. Mimi natabiri Chuo hiki mkwere akiachia ngazi kitabaki magofu tu na ndipo mtadhibitisha kuwa ni cha Kata au ni CHOO KIKUU CHA DODOMA maaana hakuna serikali itakayoweza kuendeleza haya mambo ya kulazimishalazimisha ili tu tuwe na wahitimu 40,000 wa Vodafasta wakati soko la ajira halijaboreshwa kuwachukua.NO OBJECTIVITY HERE, Bora fedha nyingi zingewekezwa katika kukuza ajira rasimi zaidi huku tukiongeza idadi ya wahitimu taratibu.
 
Back
Top Bottom