Wana jf napenda tu kusema machache.
Chuo kikuu kinafikia hatua ya kuwa chuo bora baada ya mchakato na muda fulani kupita. Kwa chuo kikuu dodoma, ni mapema mno kukiita cha kata au vodafasta. Muda wahitajika kuamua ubora wake. Kuona kuwa ni duni baada ya kulinganisha na vyuo vingine vikongwe nchini kama udsm si sahihi. Ukiangalia historia, hata udsm kilianza kama school tu kabla ya kuwa affiliated na uea. Lakini hatua kwa hatua kimeimarika.
Pia muhimbili (muhas) kilikuwa kidogo sana wakati kinaanza. Maprof walikuwa wa kuhesabu, lakini sasa kimepiga hatua kubwa sana.
Ukija ardhi (aru), nacho mwanzoni hakikuwa na madokta, lakini wakajiwekea malengo kuwa baada ya miaka 10 wawe na madokta wa kutosha na hali imekuwa hivyo. Aru ina maprof na madokta wengi sana.
Vivyo hivyo mzumbe, na vyuo vingine vingi unavyo vifahamu.
Sasa tukija kwa udom, twahitaji muda kuanzaia miaka kumi na kuendelea ili kuwe na ubora unaohitajika kulingana na vigezo vilivyo wekwa na tuc. Huwezi leo leo ukajenga majengo, papo hapo ukawa na walimu wenye phd na maprof. Hayo ni mambo yanayo hitaji muda. Na bila shaka yatakuwepo kwenye mipango yao ya muda mrefu na wa kati. Hatimaye tutakuwa na udom iliyo na sura kama vyuo vingine ambavyo mnadhani ni bora.
Pia labda ushauri kwa udom, katika kipindi hiki cha shida ya walimu, ni bora kuajiri walimu toka nje ya nchi. Hiyo inasaidia sana kupata ujuzi wa watu toka sehemu nyingine ya dunia. Binafsi sipendelei kufundishwa na mwalimu aliyesoma degree ya kwanza tanzania, ya pili tz, phd tz. Nahisi nakosa stadi toka nchi zingine.
Halafu lingine ni kuwazoeza wanafunzi wetu kusoma vitabu. Hilo ni tatizo sana. Wanafunzi wetu wengi hawazoezwi kusoma vitabu. Vitabu vinakufanya hata kama umesoma chuo duni namna gani, unakuwa na stadi, uelewa na ujuzi wa hali ya juu na kujiamini pia. Elimu yetu ya tz inatupa shida sana mara unapokwenda kusoma ulaya na marekani ambako wanafunzi na jamii yao na kwa ujumla ina utamaduni wa kusoma vitabu. Unakuta wenzako wanasoma vitabu mulivyogawiwa kwenye kozi kama wanacheza vile, na mukienda kwenye semina wanakuwa fiti, huku wewe vinakutesa mno kuvisoma.
Hivyo udom ni chuo kichanga sana, chahitaji muda ili kiwe bora. Kufuata mipango waliojiwekea ndiyo msingi wa maendeleo ya chuo hicho.