Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

hakuna la kujivunia!elimu sio majengo.
Tatizo letu tanzania tunataka kila mtu awe na 'white coller job'
vocational training ni muhimu kwa watoto wetu,haiwezekani na haitatokea watanzania wote tukawa na akili za kufika university hata tukiweka udom kila kata.lazima kuwe na wasomi werevu(wachache) na watu wenye elimu ya msingi level ya vocational training/fom 6 ya ukweli.wasomi hawa wapewe jukumu la kuiletea maendeleo nchi kwa kutumia vipaji vyao vya kiakili.hata marekani,uk na kenya hakuna degree holders weengi kama tunavyohisi.nadhani ingekua jambo la msingi kuviboresha vyuo kama udsm,sua,mzumbe,ifm,dit... Kuliko kukurupuka na hiki chuo cha kata.
Najua ntawaumiza sana wale wanaopata marks za tia maji tia maji but i ll never hesitate kueleza ukweli unapohitajika.

mwana acha chuki wewe, wewe ulikuwa unaona poa

dodoma isiwe na chuo eti viboreshwe vilivyopo?

Sema kama umefanya utafiti na ukaona utofauti uliopo

especially ki-academic kati ya udom na hivyo vyuo ulivyotaja hapo juu,

tuambie vyuo hivyo vimeizidi udom katika nyanja zipi kielimu, au unaropoka tu.

Acha chuki za kishamba.
 
Hivi nyie mnaokiponda udom mnakunya akili au?
Hamfikirii kuwa kodi zenu mnazokatwa kwenye mishahara
yenu zimechangia kujenga pale?
Badala mjivunie angalau kodi zenu zimefanyia jambo la heri bado linalalamika.


Punguza ukali wa maneno!
Walipa kodi fweza zetu nyingi wanakula mafisadi kiasi kidogo sana kinafanya maendeleo kama hayo.
Kwa sasa wakati kinamapungufu mbali mbali kitaitwa hivyo kwa 'utani' tu, ila kikiisha jiimarisha jina hilo litapotea lenyewe. Maana kuna watu wengine humu wamekasirika mishipa ya hasira imewasimama utafikiri hawajui kama hilo ni jina la utani, hakuna mahali popote 'official document' inayo kitaja kuwa UDOM ni Chuo Kikuu Cha Kata!

Ila Kale ka-fueza alikopewa Mh. JK toka Middle East kenyewe hukasemi! Masharti yake je?
 
Hakuna mtu mwenye degree na anafundisha UDOM, wapo watu wanadegree na wanafanya masterz pale udom chuo huwa kinawatumia km maseminar leader,mimi nafanya degree udom, malecture wangu wawil ni ma dr, na wawil ni maprofesa na wengine wana masterz tena kutoka vyuo vikubwa vinavyotambulika dunian.

Kama insu wa malecturz hebu jiulize chuo kikuu cha ardhi wapo kwenye mgomo na moja kati ya madai yao ni walimu hawatoshi..ili nitatizo la vyuo ving tz.,na kwanao ijua udom tatizo sio kubwa km watu ambao wanashindwa kutumia akil zao na wanatumia akil za wenzao wanavyofikiria.
 
Kama mzumbe, udsm au sua kuna watu wa aina hiyo sio sababu ya udom kuwa hivyo pia. Huwezi kuiba kwa sababu jirani yako ni mwizi wewe vipi bwana?
Kumbe umeliona hilo?? Na dogo nimemuuliza ishu nyingi sana kuhusu UDOM, na hata nilipoenda, kwenye graduation yake.

Nilipata taarifa kadhaa, kwa kifupi kuponda kwenu kumepitiliza.

Tatizo langu ni kwamba watu mnaidiss UDOM kinoma na ndio maana nasema wanaodiss namna hiyo ni mataahira na wana chuki, kama unataka kitu kirekebishwe kuna namna ya kufikisha ujumbe kistaarabu, na sio kuita chuo cha kata, juzi madogo wamegoma.

Na kuna thread iliwekwa hapa, badala ya kuwapa pole na kuwatia moyo, wapuuzi wanaanza kuwaponda eti si mnajidai CCM, kwani mmeambiwa chuo kizima chenye wanafunzi zaidi ya 20,000 wote ni CCM.

M
i bado namchukulia mtu anayeponda UDOM bila fact za ukweli ni taahira.

Pondeni na vyuo vingine basi, sio kila mtu udom udom, ya ifm mnayajua??
 
Mla Mbivu

this is UDOM-CCM school of thoughts:

Matusi, kejeli, kukanusha ukweli, kuhisi unaonewa na hatimae kutafuta public sympathy.

Huu ni uthibitisho mwingine kuwa hiki ni chuo cha kata na hamna lolote wanalopata vijana wetu pale.

Kwi kwi kwi!!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana wewe kweli Mla Mbivu. Sisi wenzio hatuamini kwenye mbivu tusijepata mbovu kwa kuvumilia sana
 
Last edited by a moderator:
pole sana wewe kweli mla mbivu. Sisi wenzio hatuamini kwenye mbivu tusijepata mbovu kwa kuvumilia sana

wa wapi wewe??

Nani kakuambia ili ule mbivu lazima uvumilie,

naona unatoka nje ya mada,

unasoma / umesoma chuo gani wewe??

Au hujasoma kabisa.
 
Hivi nyie mnaokiponda udom mnakunya akili au?
Hamfikirii kuwa kodi zenu mnazokatwa kwenye mishahara
yenu zimechangia kujenga pale?
Badala mjivunie angalau kodi zenu zimefanyia jambo la heri bado linalalamika.[

tujivunie nini? kodi zipi? wakati ni mafao yetu yaliyoko PPF,NSSF,BIMA YA AFYA,LAPF na matokeo yake wanaostaff wanapata mafao madogo bz fedha zimekopwa na serikali ya mafisa . hakuna kitu wewe udom au unaangalia majengo? chuo si majengo chuo ni elimu inayotolewa pale?
mfano angalia mzumbe hawana majengo kama udom lakini elimu inayotolewa pale si ya kitoto.
mnakazania kujenga majengo alafu wanafunzi wanamaliza masomo hakuna elimu ya vitendo? wanafundishwa na degree holder? utapata nini hapo? sasa kuna tofauti gani na walimu wa vod fast wale form 6 ambao leo wanafundisha sekondari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ndo mana tunasema udom ni chuo cha kata
 
this is udom-ccm school of thoughts.
Matusi,kejeli,kukanusha ukweli,kuhisi unaonewa na hatimae kutafuta public sympath.
Huu ni uthibitisho mwingine kuwa hiki ni chuo cha kata na hamna lolote wanalopata vijana wetu pale.
Kwi kwi kwi!!

hahaaa, kwa taarifa yako sisomi udom,

na sijasoma chuo bongo,

ila nawaponda nyinyi vilaza mnaosoma au mliosoma

vyuo flani flani mnaoponda wenzenu wa udom.

Hakuna kutafuta public sympathy hapa...
 
nadhani mkuu ungejaribu kufuatilia cv za walimu waliopo pale kwanza then ndio uongee
kwani usemacho kinautofauti mkubwa sana,pili umefika wakati tutoe kutu tulizonazo ktk vichwa vyetu kwani malanyingi tunatumia maji ktk kufikilia na sio bongo

mapinduziiii daimaaaaa

Of course kukiita chuo cha kata kimelinganishwa tu na na shule zetu za kata na sababu kubwa ni kwamba hakina waalimu wenye uzoefu, kama ni maprof wako wachache na faculty zingine hakuna kabisa. Na kama ni hao lecturers wengi wao ndio wamemaliza shule.Lingine kukosa mafunzo kwa vitendo na maabara zisizo well equipped. Hivyo kwa maelezo hayo mafupi, kitabakia na hadhi ya kuitwa chuo cha kata hadi hapo kitakapotoa elimu yenye hadi ya chuo kikuu.
 
Kwa nyakati tofauti serikali inakiri kuna uhaba wa wasomi ikiwemo ngazi ya bachelor/masters.
Haingii akilini leo hii kuambiwa UDOM kuna lecturers wa kutosha. au ndio wale feki waliotokea kenya? Tuache siasa kwenye mambo ya msingi kama elimu.mwakani unaweza ukasikia UDOM yatoa madaktari,manesi,wafamasia n.k hivi kwa kasi hii tutapona kweli?
 
this is UDOM-CCM school of thoughts.
Matusi,kejeli,kukanusha ukweli,kuhisi unaonewa na hatimae kutafuta public sympath.
Huu ni uthibitisho mwingine kuwa hiki ni chuo cha kata na hamna lolote wanalopata vijana wetu pale.
Kwi kwi kwi!![/Q


UDOM KUNA MAJENGO TU LAKINI HAKUNA ELIMU BORA PALE INAYOTOLEWA MKATAE MKUBALIII. CHUO KIMEAZISHWA KISIASA KWA LENGO LA KUPATA KURA ZA WANANCHI LAKINI CHUO HAKIJAWA TAYARI KUTOA WASOME AMBAO WATASAIDIA KULETA MAPINDUZI KWA TAIFA HILI.
MFANO MIMI NI MMOJA WA WAAJIRI NA TUMETANGAZA KAZI JUZI JUZI TU NA WALIOPITA KWA USAILI NI WATU 5 KATI YA HOA TOKA UDOM NI 2 LAKINI KWENYE USAILI HAKUNA KITU YANI HAWAJUI CHOCHOTE UKWELI TULIIUMIA SANA MANA NI KAMA WAMEPOTEZA MUDA WAO TU KUSOMA LAKINI WALICHOAMBULIWA 00000000000000000000000000000. NA WATASUMBUKA SANA KATIKA AJIRA

UDOM -CCM.
 
Mkuu,
Kwanza labda niulize ni katika mfumo wa Chuo Kikuu gani duniani hakina Tutorial Assistants ambao wanafundishwa ili nao watakapohitimu waje kuwa maprofesa?

Ni taasisi ngapi za umma na binafsi zilizolalamika ubora wa graduates wa UDOM? Miezi 6 imepita tangu wengi wao waajiriwe

Wanafunzi zaidi 21,000/= waliopo UDOM sasa wangekuwa wapi baada ya kukosa nafasi UDSM, IFM, SUA, MZUMBE au MUCCOBS? Kama si kuongeza idadi ya vibaka na wavuta unga mitaani?

Tujifunze kuwa na shukrani.

Heri ya kuwa na vibaka kuliko kuwa na wasomi feki ambao badae ukimbilia kwenye siasa na kuwa wezi wa kura tu ambayo ni aina hatari ya vibaka (rejea uchaguzi uliopita).

Tutorial assistant siyo tatitizo, tatizo ni kuwa yeye ndiye anakuwa 'senior' wa somo husika. Hiyo haipo chuo chochote duniani.

Kuhusu waajiri kulalamika mimi sijafanya utafiti na miezi sita probation inakuwa haijaisha so sina cha kusema.
 
Me pia huwa nashangaa iweje watu waseme udom ni chuo cha kata! Kiukwl chuo hiki cku zinavyokwenda kitakuwa bora sana,ni kwl vyuo vingi Tanzania (c udom pekee) kuna upungu mkubwa wa wahadhiri,ili kutatua tatizo hili udom huwaendeleza kielimu waliowaajiri. mwaka juzi nikiwa udsm nilimsikia prof. Tibaijuka(waziri wa makazi alishawi fundisha udsm) wakati wa wiki ya kigoda cha mwalimu akisema hata udsm ilipoanza haikuwa na waadhiri wenye sifa,watu wengi wakasomeshwa nje walau mambo yakabadilika..vivyo vivyo udom itakuwa nzuri its just the matter of tym..cha muhimu wazalendo msome kwa bidii mkiwa undergraduate ili muweze kupata gpa inayohitajika (3.8 and above) ili mkihitajika muweze kuajiriwa,wengi wagraduate mitaani hawana gpa hiyo thus y kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri nchi nzima.

UDSM ilianza kama university college ya East Africa,ingawa uhaba wa walimu ulikuako huwezi kulinganisha na UDOM.ni chuo kilichoibuka kama 'mzuka' na inachukua idadi kubwa ya wanafunzi kuliko uwezo wake kwa sasa.hakuna ubishi kilianzishwa ili serikali ipate cha kusema during election campaign na sio nia dhati ya kuikomboa tanzania kielimu.

In Tz politics is everything!
 
UDSM ilianza kama university college ya East Africa,ingawa uhaba wa walimu ulikuako huwezi kulinganisha na UDOM.ni chuo kilichoibuka kama 'mzuka' na inachukua idadi kubwa ya wanafunzi kuliko uwezo wake kwa sasa.hakuna ubishi kilianzishwa ili serikali ipate cha kusema during election campaign na sio nia dhati ya kuikomboa tanzania kielimu.

In Tz politics is everything!

Na SUA, MUHIMBILI NA ARDHI ZIMEIBUKA KAMA MATAWI YA UDSM. MZUMBE Ilianza kwa kulea watu wake ndipo ikawa university. Sasa hichi chuo uyoga cha UDOM wakubali ukweli kwamba elimu yao itakuwa mbaya. Ikumbukwe pia hivyo vyuo vingine elimu siyo nzuri sasa kitu kilicho chini yao si hatari?
 
hahaaa, kwa taarifa yako sisomi udom,

na sijasoma chuo bongo,

ila nawaponda nyinyi vilaza mnaosoma au mliosoma

vyuo flani flani mnaoponda wenzenu wa udom.

Hakuna kutafuta public sympathy hapa...

kazi kweli kweli!do yo know the meaning of 'school of thoughts' haina maana mpaka usome UDOM ndo uwe na school of thoughts ya UDOM.
Thats why Tz hatuendelei,yani wewe umesoma ughaibuni halafu unajidhalilisha namna hii?natumaini hujasomeshwa na kodi zetu la sivyo uturejeshee fidia.
 
Punguza ukali wa maneno!
Walipa kodi fweza zetu nyingi wanakula mafisadi kiasi kidogo sana kinafanya maendeleo kama hayo.
Kwa sasa wakati kinamapungufu mbali mbali kitaitwa hivyo kwa 'utani' tu, ila kikiisha jiimarisha jina hilo litapotea lenyewe. Maana kuna watu wengine humu wamekasirika mishipa ya hasira imewasimama utafikiri hawajui kama hilo ni jina la utani, hakuna mahali popote 'official document' inayo kitaja kuwa UDOM ni Chuo Kikuu Cha Kata!

Ila Kale ka-fueza alikopewa Mh. JK toka Middle East kenyewe hukasemi! Masharti yake je?

sio hivyo anko sam. Magreat thinkers wengine nashndwa kuwaelewa.
Bora watu waende pale wapate data kamili ndio waje kumwaga upupu hapa.
Kuna watu walikosa nafasi pale hawana qualification. Kuna wengine walikuwa na multiple admission ila wakaenda udom.
Hivi tunataka watu wote wasome udsm tu au?
Mnajishaua kusema walimu sijui nini... Nani asiyejua kuwa uhaba na ubora wa walimu ni vyuo na shule karibia zote tz.
Hata huo uzuri wa majengo yao pia mnaponda! Jamani mnataka wasome chini ya miti ndio msifie au?
Vijana wa dom msihofu wala nini!
 
kazi kweli kweli!do yo know the meaning of 'school of thoughts' haina maana mpaka usome udom ndo uwe na school of thoughts ya udom.
Thats why tz hatuendelei,yani wewe umesoma ughaibuni halafu unajidhalilisha namna hii?natumaini hujasomeshwa na kodi zetu la sivyo uturejeshee fidia.

Acha kelele wewe kwanza hufai kuwa Jack Bauer, inabidi tukuite Charles Logan.
Kukufahamisha kuwa usi-connect post yangu na mimi kusoma UDOM ni kujidhalilisha?
Hizo school of thought zipo kibao kwenye management, economics, philosophy etc. Nilikuelewa vyema, but aim ni kukufahamisha mimi ni Mtanzania na sijasoma huko UDSM, UDOM wala MZUMBE, na so far sijaona tofauti yoyote kati ya graduates wa vyuo vya Kitanzania.
 
wa wapi wewe??

Nani kakuambia ili ule mbivu lazima uvumilie,

naona unatoka nje ya mada,

unasoma / umesoma chuo gani wewe??

Au hujasoma kabisa.
Inategemeana na defintion yako ya kusoma. Nimesoma mpaka awali lakini sijui kushambulia personality wala sina jazba kama wewe. Hoja ndio jambo la msingi vinginevyo sio lazima kujibu kila kitu. Unadhani tukianza kuulizana viwango vya elimu humu yupo amabye hajasoma? au umevamia tu mada?
 
Back
Top Bottom