Wamisri wa kale walikuwa weusi(Africans)

Watu kibao duniani wametawaliwa na wameonyosha Juhudi kuwa hata kama wameitwa majina yote mabaya ila wanaweza kujikwamua mfano china na india..

Sisi huku afrika tumekalia kulilia tulitawaliwa wakati nchi zetu zina miaka zaidi ya 60 zikiwa na uwezo wa kujiamulia mambo yake ila viongozi na wananchi tunaangushana.

My point ni kwamba tusiwalaumu wazungu kwa hali yetu wakati na sisi tuna nguvu na akili na hakuna mtu atakayekuja kutuendeleza tusipoamua wenyewe na vile tukubali kuwa pamoja na ubaya wa wazungu hayo mambo kama research za kuthibitisha kuwa kwenye hayo maprimadi waliwahi kuwepo watu weusi na wenyewe wamechangia
Miaka 60 ya kujiamulia mambo?nani amekwambia?
Mambo yanaamuliwa Washington DC ,London au Brussels.
Kama hauamini tafuta kitabu kinaitwa Confessions of economic hitman cha John Perkins(kama sijakosea author) uone mambo yanavyoendeshwa.
That's why Oginga Odinga alisema "Not yet Uhuru".

Hakuna mzungu aliefanya tafiti egypt na kusema ni wamisri walikua weusi.Hawataki kuamini weusi walistaarabika miaka karibia 3000 kabla yao,hizo tafiti zimefanywa na wazawa waliojitolea maisha uao kutafuta historia ya kweli..Kama ilivyo kwa historia ya uhuru wa Tanganyika inaanzia kwa Nyerere na kuishia kwa Nyerere jambo ambalo sio kweli.
 
Watu kibao duniani wametawaliwa na wameonyosha Juhudi kuwa hata kama wameitwa majina yote mabaya ila wanaweza kujikwamua mfano china na india..

Sisi huku afrika tumekalia kulilia tulitawaliwa wakati nchi zetu zina miaka zaidi ya 60 zikiwa na uwezo wa kujiamulia mambo yake ila viongozi na wananchi tunaangushana.

My point ni kwamba tusiwalaumu wazungu kwa hali yetu wakati na sisi tuna nguvu na akili na hakuna mtu atakayekuja kutuendeleza tusipoamua wenyewe na vile tukubali kuwa pamoja na ubaya wa wazungu hayo mambo kama research za kuthibitisha kuwa kwenye hayo maprimadi waliwahi kuwepo watu weusi na wenyewe wamechangia
Uhuru tulionao ni wa bendera tu ndugu yangu,the whiteman still calls all the gademu shots
 
Unaposema sio "pure Africans" nimekumbuka tafiti mmoja ilijaribu kusema watutsi si wabantu na wewe naona ni mmoja wapo. Hivi mwafrika halisi ni yupi? maana inaonyesha tayari una vigezo vyako vya juu ya nani ni mwafrika halisi.
Ndiyo watutsi sio wabantu
 
Naona baadhi ya wachangiaji wanasema Israel ilikuwa ya watu weusi jambo ambalo sio kweli pia Yesu kuwa mweusi. Yote haya ni kutokana na fikra finyu, kukosa vitu vya kujivunia hususan maendeleo ya dunia kwa hivyo watafiti wanajaribu na wameweza kwa kiasi fulani naweza sema kuaminisha watu kwamba historia iliyopo ni ya uongo.
Kwa kipindi kirefu sasa duniani katika uvumbuzi au ugunduzi watu weusi wamekuwa nyuma au wachache katika maswala mbalimbali ya sayansi na maendeleo kwa ujumla. Na moja ya sababu kubwa ya kuwa hivyo "wamekuwa" wakidai ni kutokana na ukoloni na kwa namna moja au nyingine waweza kubaliana nao lakini ukweli ni kwamba historia ya Israel,Egypt sio ya mtu mweusi. Uwepo wao (weusi) sio kigezo cha kudai na kusema wao ndio walikuwa watawala na kwamba wameporwa historia yao.
Thibitisha sasaa!!
 
Mkuu, anaongea ukweli kabisa, watu walikuwa wanakuja Africa kusoma na kujifunza kila kitu kwa sababu Africa ilikuwa imeendelea kupita eneo lolote Duniani. Wagiriki wote maarufu walikuza africa kujifunza elimu ya juu, Hata Musa alieandika vitabu vitano vya kwanza vya biblia elimu yake yote aliipata kutoka Misri. Wale Wamisri wazamani walitokea ndani ya Africa, nchi zote zilizokuwa karibu na river Nile. Nchi Kama Tanzania, Sudan, Ethiopia, Uganda, etc. Civilization ilikuja kutoka nchi hizi na kwenda chini.

Pia Africa ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanzisha (Monotheist religion) Mungu Mmoja ambayo baadaye Judaism, Christianity and Islam will copy. Na kuirudisha tena kwa waafrica na kuwaambia angalia dini nzuri mpya. Leo apya Africa we are tunapigana kwa ajiri ya dini, kwa sababu hatujui historia yetu na tumedanganywa kwa muda mrefu sana.

Unaweza kusoma mwenyewe habari za Osiris, Isis na Horus. Unaweza kusoma zaidi kwenye vitabu vya Dr Cheick Anta Diop (The African origin of Civilization: Myth or Reality?) na Theopile Obenga. (Ancient Egypt and Black Africa: A student's Handbook for the Study of Ancient Egypt in Philosophy, Linguistics and Gender Relations).

Tatizo leo hatusomi historia yetu ya ukweli iliyoandikwa na Waafrica. Pia tv, newspapers, kubwa zinazomilikiwa na wazungu mara nyingi sana hazisemi ukweli kuhusu historia kwa sababu hawapendi ukweli ufahamike.
Sasa watu kama nyie mnaojua si mjitahidi muandike hata vitabu??,, au muwe na vipindi katika runinga na redio?,, wajue wengi zaidi,, mwishoni kabisa yaingie hadi kwenye mitaala yetu?
 
Historia ni jambo refutable hivyo basi yaweza kuwa ni kweli. Ila mimi mara nyingi huwa nachukizwa na jinsi hizi tafiti zinapo mchambua au kumuelezea mtu mweusi. Mfano jambo la pua kuwa nene au fupi au uweusi kupitiliza, kwangu mimi hizi sio sifa za mtu mweusi hata kidogo.
boss angalia hii documentary utagndua kwann moja ya feature ya mwafrika ni pua nene!
 
Sasa watu kama nyie mnaojua si mjitahidi muandike hata vitabu??,, au muwe na vipindi katika runinga na redio?,, wajue wengi zaidi,, mwishoni kabisa yaingie hadi kwenye mitaala yetu?
Vitabu vipo vimeandikwa na wataalamu wa mambo ya misri ya kale(Egyptologist) wa Kiafrica tangu miaka ya 1950,ni wewe tu hutaki kufwatilia sababu umekomaa na mainstream mass media unasoma harry potter na da vinci code.
Redioni sio kila mwenye wazo anaenda Kusema,lazjma misimamo uako iendane na wamililiki wa chombo hicho.Huwezi ona Tanzania Daima linaandika ufisadi wa mbowe au ITV kurusha makala ya kumponda Mengi n.k Wengi wa wamiliki wa vyombo vya habari ndio hao hao wanaoeneza uongo wa uduni wa mwafrika.
 
Af nshaona nawewe huna busara ya kujibu mtu,, kwani hivyo vitabu vipo vya kiswahili??,, mimi nlichokuwa nalenga ni elimu kama hii kuwafikia watu wote kwa njia ya urahisi,, wewe unaanza lawama za kuniambia nasoma mavitabu ya harry potter na da vinci kama vile una uhakika,, sasa kama huvyo vitabu vipo tangu 1950 kwa nin bado ni vya wachache??,, utajibu waafrika hawapendi kusoma,, wakati kuna vitabu kama biblia vimezekana kusomwa na idadi kubwa ya waafrika,, ni swala la uhamasishaji tu,, usiogope ogope na wewe!
 
"Misri ilikua ni Afrika kwa maandishi yake,utamaduni wake na namna yake ya kufikiri" .Hivi ndivyo anavyohitimisha mtaalamu wa masuala ya kale ya Misri(Egyptologist) raia wa Ufaransa Jean Vercoutter na mpinzani wa Cheikh Anta Diop katika mkutano wa Cairo juu ya utambulisho wa Wamisri wa kale.

Mkutano wa Cairo ulifanyika Mwaka 1974,UNESCO taasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuamua masuala kama hayo,ilikubali kua Cheikh Anta Diop na Theopile Obenga wako sahihi kua Misri ya kale ilikua ni ustaarabu(Civilazation) wa kiafrika katika nyanja zote,hii ilitokea baada ya malumbano makali kati ya Egyptologist wawili wa Kiafrika na wenzao wawili.

USHAHIDI

Tofauti na mtu atakavyoelekezwa kuamini,Misri ilikaliwa na watu waliokua wanahamia kutoka Kusini kwenda Kaskazini na watu weusi walioitwa Anu. Hawa ni watu waliotokea Kusini mwa Afrika na maeneo ya maziwa makuu ambao walilowea kwanza ilipo kwa sasa Sudan na Kusini mwa Misri.Ni Watu jamii ya Anu polepole ndio waliofuata bonde la mto Nile na kuitia Kaskazini yote mpaka Delta katika himaya yao.
Ustaarabu wa Misri una mizizi yake kutokea Kusini mwa Afrika na eneo la maziwa makuu sababu eneo hili ndio binadamu wa kwanza walizaliwa na ndio bakibaki(traces) za ustaarabu wote wa binadamu unaweza kuonekana( rejea mambo ya Oldupai Gorge) na hii ndio sababu kwa nini eneo hili Wamisri wa kale waliliita Ta Ntjer maana yake ardhi takatifu au ardhi ya Mungu.

Na kwa urithi huu uliopatikana katikati mwa Afrika kwa miaka 170,000 uliowezesha Anu kuijenga Misri kutokea kusini kwenda kaskazini.Hisabati, Kuandika, Kilimo, Usanifu Majengo, dini nakadhalika vyote vilianzia Afrika na Sudan na vilikuzwa zaidi na Wamisri.

Mafarao wa kwanza walitawala upande wa kusini kwa maelfu ya miaka,ilikua ni Msudani alieitwa Nare Mari ndie aliyemaliza kuiteka Delta ya mto Nile na Kuunda Falme ya Misri(Dynasty) iliyoungana mnamo mwaka 3300 BC.

Jina la Misri na Wamisri

Jina walilojipa na jina walilolipa bara lao pasi na shaka linaonyesha waziwazi asili(race) yao. walitumia jina(mzizi) Kam/Kem ikiwa na maana iliyopakwa makaa(coal coated) kwahiyo walikua ni weusi.Ambao ni sawa na Kemi/Kembou/Kheum/Kala ikimaanisha coal(makaa), iliyounguzwa , nyeusi katika Lugha nyingi za Kiafrika.

Michoro na Sanamu zote za Farao zinaonyesha waziwazi hawa ni watu weusi,kuanzia utawala wa kwanza(first dynasty) mpaka uvamizi wa Wagiriki.
Narmer-1st-Dynasty.jpg

Ingawa wamejaribu kuziharibu pua zao ila tazama walivyo na midomo mipana.
images

-Ushahidi mwingine ni kipimo cha vina saba na majaribio katika ngozi kwa kuangalia uwingi wa melanin.
-Familia sawa ya Lugha ,tamaduni sawa na dini sawa na waafrika wengine kwingineko.
Egyptologist wote wa Ulaya walishindwa kuonyesha uwiano kati ya Kimisri na lugha za Endo European ambazo ni ''semitic'' kama Arabic na Hebrew,Ni Cheikh Anta Diop katika miaka ya 50 aliyegundua usawa kati ya Wolof(Lugha yake) na Kimisri
-Mfumo wa familia ulioegemea upande wa mama(matriachy),jinsi mazishi yanavyofanywa na mpangilio wa ufalme,kila kitu katika tamaduni za Misri kinafanana na tamaduni za kusini mwa jangwa la Sahara. Dini ya Misri ambayo imeandikwa sana na inaendelea kuandikwa ni sawa na ile inayofanywa na watu weusi. Misri haikuamini katika Mungu zaidi ya mmoja(polytheistic) na wana sayansi wote wanajua hii na wakapandikiza propaganda kua Misri iliamini katika Miungu ili wainyime Afrika heshima yao kua wao ndio wa kwanza kuabudu katika Mungu mmoja.

Ushahidi mwingine ni kutoka kwa Wasomi wa Ulaya wenyewe mfano Wagiriki wa kale kabisa wanaoheshimika kuja Afrika wanasema Wamisri waliokutana nao ni weusi

Herodotus,anajulikana kama baba wa historia anaandika hakika kabisa Colchians(watu walioishi kando ya Black Sea) wana asili ya Misri(are of Egyptian race) kwa sababu walikua na ngozi nyeusi na nywele frizzy.

Aristotle,penginepo mwenye ushawishi mkuu katika ufikiri wa Kimagharibi anasema wale weusi sana ni waoga,hii ni kwa Wamisri na Waethiopia.

Aeschylus,mwana mashahiri akielezea meli ya Wamisri ikiondoka, i notice the crew with its black members bringing out the white tunics.

hata wakati wa utawwala wa Rumi,miaka 250 kabla ya uvamizi wa waarabu bila kujalisha uwepo wa ngozi nyeupe Misri kwa miaka 600 Ammian Marcellin, rafiki wa mtawala wa Rumi Julius anasema watu wa Misri kwa wingi wao ni wekundu(brown) au weusi.

Kama Wamisri walikua weusi,watu weupe wanatoka wapi?

Ustaarabu wa Misri ulianza miaka 27,000 iliyopita,miaka 19,000 kabla ya kuonekana kwa mtu mweupe.Uvamizi wa kwanza mkubwa wa weupe ulikua ni ule wa mwaka 663 BC wa Assyrians
Baada ya hapa Misri ikaanza kuyumba.ikavamiwa tena na Persia na Wagiriki waliomaliza tawala zote za Misri wakaja Warumi na Mwisho kabisa Waarabu walioingia Misri kama sehemu ya Uvamizi wa Kiislam karibia miaka 1000 baada ya utawala wa mwisho wa wazawa.
Waarabu walivyoingia Misri wazawa walikua wamekimbilia pande nyingine za Afrika kati yao wapo Sonike wa Mali,Akan wa Ghana,Yoruba wa Nigeria, Bassa wa Cameroon na hata Zulu na Xhosa wa Afrika Kusini. Weusi waliobakia Misri walizaliana na wavamizi ambao hiki kizazi kinaitwa Copt.
hii inaelezea kwa nini hawa Copts ni weupe lakini wanaongea BLACK TONGUE .Waarabu hawana lolote kuhusu ustaarabu wa Misri na wako makini kutosema ili wakusanye pesa ya utalii Misri.

Kama Misri ilikua ya weusi,kwa nini weusi hawana akili?

Hili ni swali maarufu sana linaloulizwa na Waafrika waliomeza propaganda ya kua mtu mweusi ni inferior.Lazima ufahamu kua baada ya uvamizi wa wageni Misri iliyumba sana, ila kutoa Misri,Afrika kwingineko ustaarabu ulizaliwa.
Mpaka mwanzo wa biashara ya utumwa ya wazungu,Afrika ilikua imetapakaa Falme nyingi maridadi na ilikua bara tajiri kuliko yote. Hujawahi kujiuliza kwa nini Mansa Musa ambae aliishi karne ya 14 ndie mtu tajiri kuliko wote kuwahi kutokea?(Meet Mansa Musa I of Mali – the richest human being in all history)Ni utumwa na ukoloni ndio umewafanya waafrika wajione wako nyuma. Na haieleweki kwanini tunaambiwa udhaifu wetu ni wa asili tumeweza kujenga ustaarabu ambao ulikuja kuambukiza dunia nzima.
Hii habari ni ngumu kumwingia mtu mweusi sababu haijasemwa na maneno takatifu ya wazungu.

Nimejaribu kutafsiri kutoka
The ancient Egyptians were Black
kama Unawajua asili ya Nubians ndio utajua kua hata Mkwawa alikua Mnubi na afrika nzima ilikua nchi ya Black,hata algeria,Moroco kote kulikua na tamazight wanajulikana kwa kiswahili wa Beriberi wote walikua weusi
 
Very good son of the soil. The Africans and Africa must fight to reclaim what is rightfully African. The whites for a long time have demonized Africa to deny them their rich heritage. Their propaganda succeeded but it is no longer a hidden fact that Africa is the origin of civilization. It is thus encouraging to see people like you coming forth to educate and evangelize the true African history. Changes will not happen overnight but we must relentlessly propagate this to all. African can never be inferior to the whites nut in fact superior. For example it is only blacks that can habitats any weather without harmful effects to their skin. Take a white man to Sahara desert and see what happens to his skin. It is even evident that the great men of the bible were blacks but whites have been fighting so hard to make it look like they were whites. Africa must stand up now against this adulteration and reclaim our rightful place in history. Hongera Sana.
 
Vizuri sana mkuu lakini tutumie na lugha zetu tuachane na hizi za hawa tunaowalaumu kwa kutufikisha hapa tulipo.....
 
Each one,teach one.
 
Ni kweli Afrika inatakiwa idai yote yaliyo yake (rightful ours) lakini hebu tujiulize hao weupe walioko Misri watakwenda wapi!. Hii ni sawa na Afrika kusini. Ila kwa Misri ni zaidi kwani Wabantu hawapo kabisa na kama wapi ni wachache mno kuweza kuanza kupigania ardhi yao.

Uingiliaji wowote kutoka mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la sahara utingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia au kusababisha vita kubwa na yaweza kuwa vita ya dunia kwani nchi za kiarabu na nchi za kimagharibi zina manufaa/zinanufaika zaidi na Misri ilvyo sasa.
 
Point ni kudai our precious HERITAGE kama ikiwa kudai ardhi itabidi kudai sio Misri oekee,bali hata pia north Africa yote na what they call middle east.
 
Ni kweli Afrika inatakiwa idai yote yaliyo yake (rightful ours) lakini hebu tujiulize hao weupe walioko Misri watakwenda wapi!. Hii ni sawa na Afrika kusini. Ila kwa Misri ni zaidi kwani Wabantu hawapo kabisa na kama wapi ni wachache mno kuweza kuanza kupigania ardhi yao.

Uingiliaji wowote kutoka mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la sahara utingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia au kusababisha vita kubwa na yaweza kuwa vita ya dunia kwani nchi za kiarabu na nchi za kimagharibi zina manufaa/zinanufaika zaidi na Misri ilvyo sasa.
It's not about claiming Egypt as a country but reclaiming our rich heritage from disinformation by whites by putting things straight through correct education to the masses.
 
Vizuri sana mkuu lakini tutumie na lugha zetu tuachane na hizi za hawa tunaowalaumu kwa kutufikisha hapa tulipo.....
Asante Mkuu. Nitajitahidi ingawa ndio hivyo walishatufanya hata kujieleza kwa lugha yetu Ni shida.
 
Mi nafikiri bila hata juhudi zao hao tusingejua hiyo Egypt iliwahi kuwa chini ya watu weusi maana hata hizo research huwa hatuzitilii maanani ..
Na shida zote za mtu mweusi aende akahangaike kwenye mapiramidi huko kutaka kujua asili yake aache kupambana na malaria na magonjwa kibao huku yanayomsubiri

Mkuu, unabidi uelewee kama watu wote wana historia yao, Weusi, white, Arabs and asians. Ukiwaliza waarabu historia yao watavyambia kwa miata mingi elfu nne tanao, Ukiwauliza wazungu historia yao, watakwambia historia yao kwa miaka ya millions. Ukiwauliza waafrica historia yao, wengi hawajui kitu chochote kabla ukoloni na utumwa.

Kwa hiyo mtu mweusi leo sio kama anataka kuchukua misri au kuchukua mapiramidi. Mtu mweusi anataka kuchukua historia yake. Kama watu wengine wote duniani wanaipenda na wanaijua historia yao. Kwanini weusi wasijue na wasiepende historia yao.

Kama waafrica watajua historia yao vizuri, watoto wetu watafundishwa vizuri historia yao na watakuwa kuwa wanapenda historia yao na rangi yao kama watu wengine duniani wanavyopenda yangi zao na historia yao.

Kumbuka kwamba sisi wote wanadamu maisha yetu yametengenezwa zaidi kwa historia yetu; elimu tuliyopewa, dini zetu, watu tunaongea nao kila situ, sehemu tunayo ishi, kazi zetu na vitu kama hizi.

Lakini kitu kikubwa ni historia, wazazi wetu wanavyotuambia, elimu tuliyofundishwa. kama unaweza kuwaambia wazazi kufundisha watoto wetu historia yao ya kweli, walimu kufundisha elimu ya ukweli, dini kusema ukweli, kwa miaka mifupi utakuwa na watoto wanaofikiria kama watoto wazungu na waarabu, kama kwamba watoto wetu wanaweza kufanya kila kitu chochote kama mtu yoyote duniani anavyoweza kufanya.

Nakuuliza swali, kwa nini unafikiria wazungu wanafikilia wanaweza kufanya kitu chochote?
 
Back
Top Bottom