Wamisri wa kale walikuwa weusi(Africans)

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,370
3,956
"Misri ilikua ni Afrika kwa maandishi yake,utamaduni wake na namna yake ya kufikiri" .Hivi ndivyo anavyohitimisha mtaalamu wa masuala ya kale ya Misri(Egyptologist) raia wa Ufaransa Jean Vercoutter na mpinzani wa Cheikh Anta Diop katika mkutano wa Cairo juu ya utambulisho wa Wamisri wa kale.

Mkutano wa Cairo ulifanyika Mwaka 1974,UNESCO taasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuamua masuala kama hayo,ilikubali kua Cheikh Anta Diop na Theopile Obenga wako sahihi kua Misri ya kale ilikua ni ustaarabu(Civilazation) wa kiafrika katika nyanja zote,hii ilitokea baada ya malumbano makali kati ya Egyptologist wawili wa Kiafrika na wenzao wawili.

USHAHIDI

Tofauti na mtu atakavyoelekezwa kuamini,Misri ilikaliwa na watu waliokua wanahamia kutoka Kusini kwenda Kaskazini na watu weusi walioitwa Anu. Hawa ni watu waliotokea Kusini mwa Afrika na maeneo ya maziwa makuu ambao walilowea kwanza ilipo kwa sasa Sudan na Kusini mwa Misri.Ni Watu jamii ya Anu polepole ndio waliofuata bonde la mto Nile na kuitia Kaskazini yote mpaka Delta katika himaya yao.
Ustaarabu wa Misri una mizizi yake kutokea Kusini mwa Afrika na eneo la maziwa makuu sababu eneo hili ndio binadamu wa kwanza walizaliwa na ndio bakibaki(traces) za ustaarabu wote wa binadamu unaweza kuonekana( rejea mambo ya Oldupai Gorge) na hii ndio sababu kwa nini eneo hili Wamisri wa kale waliliita Ta Ntjer maana yake ardhi takatifu au ardhi ya Mungu.

Na kwa urithi huu uliopatikana katikati mwa Afrika kwa miaka 170,000 uliowezesha Anu kuijenga Misri kutokea kusini kwenda kaskazini.Hisabati, Kuandika, Kilimo, Usanifu Majengo, dini nakadhalika vyote vilianzia Afrika na Sudan na vilikuzwa zaidi na Wamisri.

Mafarao wa kwanza walitawala upande wa kusini kwa maelfu ya miaka,ilikua ni Msudani alieitwa Nare Mari ndie aliyemaliza kuiteka Delta ya mto Nile na Kuunda Falme ya Misri(Dynasty) iliyoungana mnamo mwaka 3300 BC.

Jina la Misri na Wamisri

Jina walilojipa na jina walilolipa bara lao pasi na shaka linaonyesha waziwazi asili(race) yao. walitumia jina(mzizi) Kam/Kem ikiwa na maana iliyopakwa makaa(coal coated) kwahiyo walikua ni weusi.Ambao ni sawa na Kemi/Kembou/Kheum/Kala ikimaanisha coal(makaa), iliyounguzwa , nyeusi katika Lugha nyingi za Kiafrika.

Michoro na Sanamu zote za Farao zinaonyesha waziwazi hawa ni watu weusi,kuanzia utawala wa kwanza(first dynasty) mpaka uvamizi wa Wagiriki.
Narmer-1st-Dynasty.jpg

Ingawa wamejaribu kuziharibu pua zao ila tazama walivyo na midomo mipana.
images

-Ushahidi mwingine ni kipimo cha vina saba na majaribio katika ngozi kwa kuangalia uwingi wa melanin.
-Familia sawa ya Lugha ,tamaduni sawa na dini sawa na waafrika wengine kwingineko.
Egyptologist wote wa Ulaya walishindwa kuonyesha uwiano kati ya Kimisri na lugha za Endo European ambazo ni ''semitic'' kama Arabic na Hebrew,Ni Cheikh Anta Diop katika miaka ya 50 aliyegundua usawa kati ya Wolof(Lugha yake) na Kimisri
-Mfumo wa familia ulioegemea upande wa mama(matriachy),jinsi mazishi yanavyofanywa na mpangilio wa ufalme,kila kitu katika tamaduni za Misri kinafanana na tamaduni za kusini mwa jangwa la Sahara. Dini ya Misri ambayo imeandikwa sana na inaendelea kuandikwa ni sawa na ile inayofanywa na watu weusi. Misri haikuamini katika Mungu zaidi ya mmoja(polytheistic) na wana sayansi wote wanajua hii na wakapandikiza propaganda kua Misri iliamini katika Miungu ili wainyime Afrika heshima yao kua wao ndio wa kwanza kuabudu katika Mungu mmoja.

Ushahidi mwingine ni kutoka kwa Wasomi wa Ulaya wenyewe mfano Wagiriki wa kale kabisa wanaoheshimika kuja Afrika wanasema Wamisri waliokutana nao ni weusi

Herodotus,anajulikana kama baba wa historia anaandika hakika kabisa Colchians(watu walioishi kando ya Black Sea) wana asili ya Misri(are of Egyptian race) kwa sababu walikua na ngozi nyeusi na nywele frizzy.

Aristotle,penginepo mwenye ushawishi mkuu katika ufikiri wa Kimagharibi anasema wale weusi sana ni waoga,hii ni kwa Wamisri na Waethiopia.

Aeschylus,mwana mashahiri akielezea meli ya Wamisri ikiondoka, i notice the crew with its black members bringing out the white tunics.

hata wakati wa utawwala wa Rumi,miaka 250 kabla ya uvamizi wa waarabu bila kujalisha uwepo wa ngozi nyeupe Misri kwa miaka 600 Ammian Marcellin, rafiki wa mtawala wa Rumi Julius anasema watu wa Misri kwa wingi wao ni wekundu(brown) au weusi.

Kama Wamisri walikua weusi,watu weupe wanatoka wapi?

Ustaarabu wa Misri ulianza miaka 27,000 iliyopita,miaka 19,000 kabla ya kuonekana kwa mtu mweupe.Uvamizi wa kwanza mkubwa wa weupe ulikua ni ule wa mwaka 663 BC wa Assyrians
Baada ya hapa Misri ikaanza kuyumba.ikavamiwa tena na Persia na Wagiriki waliomaliza tawala zote za Misri wakaja Warumi na Mwisho kabisa Waarabu walioingia Misri kama sehemu ya Uvamizi wa Kiislam karibia miaka 1000 baada ya utawala wa mwisho wa wazawa.
Waarabu walivyoingia Misri wazawa walikua wamekimbilia pande nyingine za Afrika kati yao wapo Sonike wa Mali,Akan wa Ghana,Yoruba wa Nigeria, Bassa wa Cameroon na hata Zulu na Xhosa wa Afrika Kusini. Weusi waliobakia Misri walizaliana na wavamizi ambao hiki kizazi kinaitwa Copt.
hii inaelezea kwa nini hawa Copts ni weupe lakini wanaongea BLACK TONGUE .Waarabu hawana lolote kuhusu ustaarabu wa Misri na wako makini kutosema ili wakusanye pesa ya utalii Misri.

Kama Misri ilikua ya weusi,kwa nini weusi hawana akili?

Hili ni swali maarufu sana linaloulizwa na Waafrika waliomeza propaganda ya kua mtu mweusi ni inferior.Lazima ufahamu kua baada ya uvamizi wa wageni Misri iliyumba sana, ila kutoa Misri,Afrika kwingineko ustaarabu ulizaliwa.
Mpaka mwanzo wa biashara ya utumwa ya wazungu,Afrika ilikua imetapakaa Falme nyingi maridadi na ilikua bara tajiri kuliko yote. Hujawahi kujiuliza kwa nini Mansa Musa ambae aliishi karne ya 14 ndie mtu tajiri kuliko wote kuwahi kutokea?(Meet Mansa Musa I of Mali – the richest human being in all history)Ni utumwa na ukoloni ndio umewafanya waafrika wajione wako nyuma. Na haieleweki kwanini tunaambiwa udhaifu wetu ni wa asili tumeweza kujenga ustaarabu ambao ulikuja kuambukiza dunia nzima.
Hii habari ni ngumu kumwingia mtu mweusi sababu haijasemwa na maneno takatifu ya wazungu.

Nimejaribu kutafsiri kutoka
The ancient Egyptians were Black
 
Good...nimeipenda saana hii.
Natamani Apollo,Eiyer & co...wapitie hapa ili wajazie nyama.

.....thanks and God bless you and all Africans.
Mkuu nimeisoma hii na nakubali kwamba Wamisri wa kale kabisa walikuwa ni weusi kama sisi huku kusini mwa jangwa la Sahara,lakini siyo hivyo tu bali hata nchi zingine ambako kuna weupe wengi....

Suala la Misri linaonekana kuwa gumu kwasababu lina mambo mengi sana ambayo yameunganishwa na kutengeneza uongo mkuu kuhusu asili na historia ya mtu mweusi....

Kuna vita kubwa inafanywa kuhakikisha mtu mweusi anabaki kwenye lindi na giza kwasababu wanajua ubora wa mtu mweusi.Wanajua kuwa binadamu wa kwanza kustaarabika alikuwa mweusi.Binadamu wa kwanza alikuwa mweusi.Kwa wale wa kwenye dini ni kwamba mitume na manabii wote walikuwa weusi....

Mtu mweusi ni binadamu bora kabisa kupata kuwepo duniani na hawa ndiyo "wateule" walioko duniani.Ujinga na njama za kinyama zilizotokea miaka 2000 iliyopita zimemfanya mtu mweusi awe hapa alipo leo....

Kama leo wakikubali kuwa Misri ilikuwa na watu weusi itabidi wabadili mambo mengi sana.Hawatakubali kwasababu binadamu aliyewahi kuwepo duniani,binadamu aliyebadili historia ya dunia,binadamu ambaye aliishi na kufanya mengi alikuwa mweusi,kitendo cha kusema Misri ilikuwa na wesusi hapo kabla inakuwa kama wanakubali binadamu huyo alikuwa mweusi na balaa la jambo hili wanalijua kabisa.....

Kamwe hawatakubali hasara watakayoipata kwa kukubali jambo hili maana kuna uhusiano mkubwa sana kati ya Waisraeli na Wamsiri wa kale...

Hata eneo lote la "Mashariki ya kati" lilikuwa ni sehemu ya Afrika na palikuwa panajulikana kaka "north west Afrika" na siyo mashariki ya kati kwakuwa hakuna kitu mashariki ya kati duniani na eneo hilo lilikuwa linakaliwa na watu weusi wote na weupe walikuja baadaye sana.....

Haya mambo yana mengi sana....
 
Tatizo tunashindwa kuelewa ipi ni STORY na ipi ni HISTORY.....ndo mana pengine tunajuwa Egyptians ni Arabians......
Egypt ni neno la Kigiriki,Hiyo Egypt wenyewe aboriginals waliita Kem/Kemet.
Wagiriki waliingia Misri wakati falme imeangushwa zamani na watu wake kutawanyika Afrika yote.
 
Egypt ni neno la Kigiriki,Hiyo Egypt wenyewe aboriginals waliita Kem/Kemet.
Wagiriki waliingia Misri wakati falme imeangushwa zamani na watu wake kutawanyika Afrika yote.
hyo falme iliangushwa na nani...tuanzie hapo
 
Mkuu nimeisoma hii na nakubali kwamba Wamisri wa kale kabisa walikuwa ni weusi kama sisi huku kusini mwa jangwa la Sahara,lakini siyo hivyo tu bali hata nchi zingine ambako kuna weupe wengi....

Suala la Misri linaonekana kuwa gumu kwasababu lina mambo mengi sana ambayo yameunganishwa na kutengeneza uongo mkuu kuhusu asili na historia ya mtu mweusi....

Kuna vita kubwa inafanywa kuhakikisha mtu mweusi anabaki kwenye lindi na giza kwasababu wanajua ubora wa mtu mweusi.Wanajua kuwa binadamu wa kwanza kustaarabika alikuwa mweusi.Binadamu wa kwanza alikuwa mweusi.Kwa wale wa kwenye dini ni kwamba mitume na manabii wote walikuwa weusi....

Mtu mweusi ni binadamu bora kabisa kupata kuwepo duniani na hawa ndiyo "wateule" walioko duniani.Ujinga na njama za kinyama zilizotokea miaka 2000 iliyopita zimemfanya mtu mweusi awe hapa alipo leo....

Kama leo wakikubali kuwa Misri ilikuwa na watu weusi itabidi wabadili mambo mengi sana.Hawatakubali kwasababu binadamu aliyewahi kuwepo duniani,binadamu aliyebadili historia ya dunia,binadamu ambaye aliishi na kufanya mengi alikuwa mweusi,kitendo cha kusema Misri ilikuwa na wesusi hapo kabla inakuwa kama wanakubali binadamu huyo alikuwa mweusi na balaa la jambo hili wanalijua kabisa.....

Kamwe hawatakubali hasara watakayoipata kwa kukubali jambo hili maana kuna uhusiano mkubwa sana kati ya Waisraeli na Wamsiri wa kale...

Hata eneo lote la "Mashariki ya kati" lilikuwa ni sehemu ya Afrika na palikuwa panajulikana kaka "north west Afrika" na siyo mashariki ya kati kwakuwa hakuna kitu mashariki ya kati duniani na eneo hilo lilikuwa linakaliwa na watu weusi wote na weupe walikuja baadaye sana.....

Haya mambo yana mengi sana....
Kamwe hawataweza kukubali kua ancient Egyptians walikua weusi,wameshakubali kua Egyptian civilazation ndio mzizi wa civilization zote duniani..

Hawatakubali kubadilika sababu wameshasema na mpaka kuwaaminisha weusi kua wao ndio jamii dhaifu kupata kutokea.Wakikubali kua weusi ni number 1 civilazation in the world wataonekana wao ndio dhaifu kiuhalisia.

Hata hao akina Aristotle ambaye ni baba wa philosophy ya magharibi alikuja kujifunza Alexandria Misri.
 
Na hata hiyo walioita New World iligogunduliwa na Columbus,mtu mweusi alikua ashafika huko kitambo tu.Hivi mtu atasema asili ya wahindi weusi ni wapi??
 
"Good Way Is That You Suspect, Follow Your Insincts".... moja kati ya nukuu zangu nanazozipenda na zinaniongoza katika mambo mengi sana. binafsi nishawahi jiuliza, hivi ni kweli sisi waafrika (weusi) hatujastaarabika? hivi ni kweli bila wazungu tungeendelea kuishi maisha pori yale? je ni kweli mtu mweupe ana akili nyingi kuliko mweusi? na je ni nini chanza cha mweusi kuzidiwa maarifa na mweupe? halafu pia nikajiuliza... mbona matendo anayofanya mtu mweusi yana staha kuliko ya mtu mweupe? swali la mwisho likawa, ingekuwa kama mtu mweusi ndo angetawala kila kitu ulimwenguni!?... Jibu nililohisi, HUENDA KUNA HIYANA WATU WEUPE WALIWAHI KUWAFANYIA MABABU ZETU, HAPO KALE! leo ndo napata mwanga, kweli njia nzuri ni ile unayoihisi.
 
hyo falme iliangushwa na nani...tuanzie hapo

Hujasoma thread mkuu ila nakutafunia sasa umeze mwenyewe......

''Ustaarabu wa Misri ulianza miaka 27,000 iliyopita,miaka 19,000 kabla ya kuonekana kwa mtu mweupe.Uvamizi wa kwanza mkubwa wa weupe ulikua ni ule wa mwaka 663 BC wa Assyrians
Baada ya hapa Misri ikaanza kuyumba.ikavamiwa tena na Persia na Wagiriki waliomaliza tawala zote za Misri wakaja Warumi na Mwisho kabisa Waarabu walioingia Misri kama sehemu ya Uvamizi wa Kiislam karibia miaka 1000 baada ya utawala wa mwisho wa wazawa.''
 
nashukuru kwa kunitafunia....ndo nameza mkuu.....
 
Kamwe hawataweza kukubali kua ancient Egyptians walikua weusi,wameshakubali kua Egyptian civilazation ndio mzizi wa civilization zote duniani..

Hawatakubali kubadilika sababu wameshasema na mpaka kuwaaminisha weusi kua wao ndio jamii dhaifu kupata kutokea.Wakikubali kua weusi ni number 1 civilazation in the world wataonekana wao ndio dhaifu kiuhalisia.

Hata hao akina Aristotle ambaye ni baba wa philosophy ya magharibi alikuja kujifunza Alexandria Misri.
Hata Pythagoras elimu yake ni ile ile tu....

Kimsingi ukweli wa eneo linaloitwa "mashariki ya kati" ni kitendawili kwa wale wasiopenda kujua ukweli..

Mambo mengi wameficha maksudi kabisa.Misri utamaduni wake ulikuwa ule ule na ndiyo maana wakaazi wengi wa mashariki ya kati waliishi Misri na hakukuwa na tofauti na pia lugha yao ilikuwa moja...

Ukweli ni kwamba mtu mweusi ndiyo mhimili wa yote ambayo leo yanaitwa ustaarabu,yeye ndiye mwanzilishi.Weupe wanachukia sana pale ambapo ukweli huu unavyoendelea kusemwa lakini hakuna namna wao watulie tu....
 
Ukweli ni kama moshi hata ukiufunika utapenya tuu mkuu..time will tell
 
Asante kwa mada hii, umeniongezea kwa yale ninayoendelea kutaka kuyajua kwa mwaka huu wa 2017. Naomba wale wanaohitaji kufahamu zaidi watafute mihadhara ya akina Hon. Minister, Louis Farrakan, Dr. Ben Jacanann, Dr. Sartimer, Dr. Khalid Mohammed, Dr. Martin Luther, Dr. Malcon na wengine wengi. Ukienda 'youtube' utawasikia.

Kwa ufupi historia ya mtu mweusi imepotoshwa kiasi kwamba watu weusi wa sasa hawajui na hawatojua historia yao na uthamani wa mtu mweusi hususan mchango wao katika maendeleo ya sayansi ya sasa. Sio hivyo, kuna suala la 'ni nani hasa wana wa Israeli waliotamkwa kwenye vitabu vitakatifu???? ukiweza kusoma vitabu vitakatifu hususan Biblia iko wazi kuhusu hili lakini jinsi linavyohubiriwa na watu weupe ni kuficha ukweli.

Hata ukitumia common sense kuhusu Taifa la sasa la Israel utagundua waisrael wa leo sio wale waliotajwa kwenye biblia. Hivi iweje katikati ya Ufaransa na Ubeligiji liwepo Taifa la watu weusi wakati nchi zote zilizopo jirani zina watu weupe (Itakuwa miujiza) ni sawa na Israel, iweje pale middle east liwepo taifa moja tu la watu weupe wakati mataifa yaliyozunguka yana clored people???

Jambo zuri ni kwamba kwa sasa duniani kote kuna mjadala mkali sana kuhusu 'who are the real children of Israel'. Ukifuatilia mjadala huu ambapo reference nyingi zinatoka kwenye biblia na historia ya watu weusi na hasa wapi binadamu wa kwanza aliishi, basi utagundua mtu mweusi ndiyo anakuwa 'center' ya mjadala. Tuendelee kujifunza ili tujifahamu pamoja na uwezo mchango wa mtu mweusi katika historia ya maendeleo ya dunia ya sasa.
 
Historia ni jambo refutable hivyo basi yaweza kuwa ni kweli. Ila mimi mara nyingi huwa nachukizwa na jinsi hizi tafiti zinapo mchambua au kumuelezea mtu mweusi. Mfano jambo la pua kuwa nene au fupi au uweusi kupitiliza, kwangu mimi hizi sio sifa za mtu mweusi hata kidogo.
 
Hata Pythagoras elimu yake ni ile ile tu....

Kimsingi ukweli wa eneo linaloitwa "mashariki ya kati" ni kitendawili kwa wale wasiopenda kujua ukweli..

Mambo mengi wameficha maksudi kabisa.Misri utamaduni wake ulikuwa ule ule na ndiyo maana wakaazi wengi wa mashariki ya kati waliishi Misri na hakukuwa na tofauti na pia lugha yao ilikuwa moja...

Ukweli ni kwamba mtu mweusi ndiyo mhimili wa yote ambayo leo yanaitwa ustaarabu,yeye ndiye mwanzilishi.Weupe wanachukia sana pale ambapo ukweli huu unavyoendelea kusemwa lakini hakuna namna wao watulie tu....

Mama yangu ni mmoja wa waumini wa doctrine ya inferiority wa mtu mweusi,anasema mtu mweusi kokote aliko ni shida na umaskini na matatizo yaleyale yaliyopo Africa.

Utaulizwa hizi habari unazitolea wapi?Mbona darasani hazifundiswi?
Hata Pythagoras elimu yake ni ile ile tu....

Kimsingi ukweli wa eneo linaloitwa "mashariki ya kati" ni kitendawili kwa wale wasiopenda kujua ukweli..

Mambo mengi wameficha maksudi kabisa.Misri utamaduni wake ulikuwa ule ule na ndiyo maana wakaazi wengi wa mashariki ya kati waliishi Misri na hakukuwa na tofauti na pia lugha yao ilikuwa moja...

Ukweli ni kwamba mtu mweusi ndiyo mhimili wa yote ambayo leo yanaitwa ustaarabu,yeye ndiye mwanzilishi.Weupe wanachukia sana pale ambapo ukweli huu unavyoendelea kusemwa lakini hakuna namna wao watulie tu....
 
Historia ni jambo refutable hivyo basi yaweza kuwa ni kweli. Ila mimi mara nyingi huwa nachukizwa na jinsi hizi tafiti zinapo mchambua au kumuelezea mtu mweusi. Mfano jambo la pua kuwa nene au fupi au uweusi kupitiliza, kwangu mimi hizi sio sifa za mtu mweusi hata kidogo.
Ingawa unahisi kusema pua pana au midomo mnene ni offensive sawa,samahani lakini ukweli ndi huo.

Kwa mtazamo wako sifa za mtu mweusi ni zipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom