Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Nalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Jeshi la Polisi kumwita mtuhumiwa ofisini kwao nakumkalisha chini Kisha kumpiga picha nakuzisambaza. Hii siyo sahihi kabisa, sidhani kama watoto wao wanapotuhumiwa au watoto wa viongozi wanapokengeuka tunawafanyia hivi.
Lakini jambo la pili huyu mtoto ni mhanga wa ukatili unaofanywa na wanaume na watu wenye fedha, badala tutafute waliomrubuni tunakwenda kumdhalilisha na kumwaribia future yake. Hii siyo kazi ya Serikali. Mhanga wa matukio ya kialifu analindwa Duniani kote, udhalilishaji wa mtuhumiwa ni kinyume kabisa na Haki za binadamu.
Tulitegemea Jeshi liwe mfano wa kukemea picha zisizofaa wao ndio wanasambaza. Matokeo yake watoto wengi ambao wajapevuka kama alivyo mtuhumiwa wanaweza kutafuta umaarufu kwa kufanya matendo haya nakutegemea dola isambaze taarifa zao wafahamike Duniani.
Sijawahi kuona polisi Zanzibar wakipiga picha watu wanaotuhumiwa kuishi kinyume na maadili na kuzisambaza, aaskari bara mnafundishwa wapi ukatili na ya policing?Wapi nafasi ya dawati la jinsia?