Polisi Mwanza yakamata watuhumiwa 53 kwa kujihusisha Biashara ya Danguro kinyume na Sheria

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tarehe 02.06.2023 muda wa 21:40 usiku huko maeneo va Sabasaba. Kata na Wilava va Ilemela limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aitwaye James Chacha, miaka 58, mfanyabiashara, mkazi wa lloganzara akiwa anafanya biashara ya Danguro kwenye nyumba yake na katika Nyumba hiyo walikamatwa watuhumiwa 53 kati yao wanawake 23 na wanaume 30 wakifanya vitendo vya ngono kinyume na maadili.

Mnamo tarehe 02.06.2023 muda wa 08:30 asubuhi Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa eneo la lloganzara karibu na shule ya msingi Tulele @kwa Chacha kuna biashara ya Danguro. Baada ya taarifa hizo kuripotiwa askari walifanya ufuatiliaji ambapo walifika eneo hilo nakufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi ukikamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Tarehe 01.06.2023 muda wa 14:00 mchana huko katika kijiji cha Chema, tarafa ya Kahunda, Wilaya ya Sengerema, kulipatikana taarifa kuwa kuna mtu anatoa mahubiri ya kupotosha jamii kwa kuwataka waumini wake wasiende Hospital kupata huduma ya matibabu pindi wakiugua au kuuguliwa; Badala yake wapelekwe kwenye kanisa lake liitwalo Neno kwaajili ya kuombewa na kupata uponyaji wa magonjwa yanayo wakabili.

Askari Polisi walifika katika kanisa hilo lililopo kijiji cha chema na kufanikiwa kumkamata Herman Magigita, miaka 60, mehungaji wa kanisa la Neno na mkazi wa Mwangika kwa tuhuma za kosa la kufanya shughuli za kanisa bila kuwa na kibali cha usajili kinyume cha sheria na kutoa mahubiri potofu kwa waumini wake.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa wito kwa wakazi wote wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi na kutoa taarifa zaidi za uhalifu na wahalifu wote ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yao, kamwe tusifiche uhalifu kwa namna yoyote ile. Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinafanziwa kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa.

IMG_7497.jpeg
IMG_7498.jpeg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tarehe 02.06.2023 muda wa 21:40 usiku huko maeneo va Sabasaba. Kata na Wilava va Ilemela limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aitwaye James Chacha, miaka 58, mfanyabiashara, mkazi wa lloganzara akiwa anafanya biashara ya Danguro kwenye nyumba yake na katika Nyumba hiyo walikamatwa watuhumiwa 53 kati yao wanawake 23 na wanaume 30 wakifanya vitendo vya ngono kinyume na maadili.
What if hiyo idadi wangekuwa scartered kwenye nyumba zake nne au tano zilizo katika maeneo tofauti?
 
MAADILI YA TAIFA.

SELIKALI, WAZAZI, VIONGOZI WA DINI, WATOTO KUJITAMBUA = 0.

HII NCHI YA HOVYO SANA
 
James Chacha; wakati mwingine ukitaka kufanikiwa kwenye hiyo huduma, jitahidi kuwa karibu na hao jamaa. Wakitaka hela ya kubrashia viatu, wape!! Lakini pia wenzako huwa wanaweka na bar ya kuzugia.

Usisahau wachawi bado wapo!
 
Hivi wale waliotajwa na CAG kuwa wametapanya fedha zetu wamesha kamatwa na polisi? Au ndo imetoka!
 
Polisi bhana hiyo mikoa mkiwazuia hao mtaanza kusikia kesi za ubakaji zimeongezeka inatakiwa mnakataza ila sio kihivyo kama ndio agenda kuu huko daslm wanasema Bandari wamempa kanjubai ninyi mpo busy na nyama choma...
 
Back
Top Bottom