Jeshi la Polisi kuchunguza Askari anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,168
Kamishna Hamad alitaja sababu tatu za kutokukubaliana na tendo hilo ndani ya polisi; kinyume cha sheria, maadili na linalomwondolea ukakamavu askari.

Kutokana na mkasa huo, Kamishna Hamad aliyeonekana kukereka nalo, aliiambia Nipashe kwamba ofisi yake ina mpango maalum wa kuwasaka askari wake wote wenye hulka na kujihusisha na matendo ya aina hiyo.

"Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kadhia hiyo ikiwamo kufanyiwa kipimo askari huyo ili kujiridhisha kama kweli anafanya kitendo hicho... ingawa tumeona video katika mitandao ya kijamii lakini hatuwezi kusema moja kwa moja kama ni kweli au sio kweli," alifafanua.

Alisisitiza kwamba, kanuni na mwenendo wa kisheria za jeshi hilo haziruhusu mapenzi ya jinsia moja, na madai hayo yakithibitika, atafikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na hatua nyinginezo.

Kamishna Hamad alisema askari anapokuwa shoga, hukosa uaminifu na ukakamavu katika jukumu lake la msingi la kulinda raia na mali zao.

"Hatufai na atashindwa kufanya kazi za polisi, na hata heshima kwa jamii haitakuwapo. Kama unamtuma askari polisi wa aina hii akamkamate mhalifu, akifika huko anaweza hata akaguswa (...). Sasa heshima iko wapi kwa Jeshi la Polisi?" alilalamika katika kauli ya kukereka.

Aliendelea: "Huu si utamaduni wa Jeshi la Polisi na wala hakutumwa hivyo. Matendo ya mtu binafsi lazima yatafautishwe na taasisi.

"Hata hizo picha zinazosambaa hazionyeshi kuwa amevaa sare za polisi au kufanya kitendo hicho kwenye kituo cha polisi, hivyo isitafsiriwe kuwa Jeshi la Polisi ndio limefanya."


Akizungumzia mikakati ya jeshi hilo katika kukomesha ushoga ndani ya Polisi Zanzibar, Kamishna Hamad aliwataka askari wote wenye mwenendo wa aina hiyo, wajisalimishe kwenye uongozi ili warekebishwe waendane na utamaduni wa jeshi hilo.

"Lengo sio kuwafukuza kazi, bali ni kuwarekebisha, kwa sababu huwezi kujua anafanya vitendo hivyo kwa sababu gani. Inawezekana alishafanyiwa kitendo hicho tokea utotoni na hawezi kujitetea na anaendelea kujizuru," alifafanua.

Kuhusu namna ya kuwatambua wenye tabia hiyo, alisema taratibu za polisi wakati wa kuajiri hazihusishi utambuzi wa tabia za ushoga kwa mwajiriwa bali hupimwa afya zao kwa ujumla.

Pia alisema Jeshi la Polisi lina taratibu na sheria zake ambazo zimeainisha makosa yote ambayo askari wa jeshi hilo hapaswi kufanya pamoja na hukumu zake endapo atafanya makosa hayo.

"Humu ndani ya kitabu hiki (sheria za polisi) kuna utaratibu mzima wa jeshi umewekwa. Kwa hivyo, askari anayefanya makosa ambayo yameainishwa humu ikiwamo hayo ya kufanya mapenzi ya jinsia moja, kuna mahakama za kijeshi na hukumu zimewekwa," alisema


Chanzo: Nipashe

---

Kwa jinsi alivyoifedhehesha Jamhuri leo asubuhi mlitakiwa mtupe ukweli

Pia soma
- Video chafu ya askari wa kiume akiingiliwa inaleta picha gani?
 
Aisee afande kaleft group...kweli utamu auna siri
20211128_193658.jpg
 
Kwa ufahamu wangu hapo kinachofanyiwa kazi ni ile video clip kwanza kama sio editing na vitu kama hivyo. Ikishabainika kuwa ni video halisi ndio sasa taratibu zingine za kisheria zitaendelea.

Moja ya changamoto itakayofanya wachelewe zaidi ni chanzo cha video husika hapo kuna watu au chain ya watu itaingia, na hao watajikuta wana hatia chini ya Sheria ya Makosa ya kimtandao, kusambaza picha chafu

Wakiwahi Mahakamani iwe ya kijeshi au kiraia wataaibika na hilo wanalijua. Anaweza kuikataa mwanzo mwisho hiyo video hadi watakapothibitisha kuwa hiyo video sio bandia ni halisi. Na hapo ndio hadi kifaa kilichotumika kurekodi kitahitajika. (Pagumu hapo)

Changamoto nyingine ni huu mtego Polisi na Ofisi ya DPP wanabidi kuwa makini sana, hili swala linaweza likatuingiza kwenye mtego kama Kenya sababu yanaweza kuibuka masuala ya haki za binadamu, kesi hii itasimama ikisubiri maamuzi ya Mahakama Kuu, ambayo sasa akipata wakili mzuri Ibara ya 13(5) ya Katiba ni ngumu kumeza.

Inaweza ikatengeneza sheria ya hovyo zaidi.

Hapa chakufanyikani kumalizana naye kimya kimya kwa makosa tofauti na hili swala la ushoga ili hata asiporidhikaakaenda Mahakamani asipate au asipenyeze swala la ushoga kujadiliwa na Mahakama Kuu.

Ushoga kujadiliwa na Mahakama Kuu ni hatarikwa afya ya taifa, tufahamu kuwa sheria zetu zipo 50/50 kwenye hili swala itategemea presha ya nje, hoja za utetezi, hojaza upingaji na msimamo wa Mahakama juu ya sheria na haki za binadamu.

Ifahamike Jajianaweza kuwa anapinga vikali sana haya mambo ya ushoga lakini akatoa maamuzi/tafsiri ya sheria tofauti kabisa na msimamo wake binafsi kwakuwa hapo atakuwa ni Jaji na sio yeye binafsi.

Hil jambo ni mtego sana, tukikurupuka itatu cost
 
Muigizaji maarufu jijini Dar es Salaam ameitaka Serikali ya mama Samia na Dk Mwinyi kufanya kila wawezalo na kumchukulia hatua Kali Askari aliyechafua hali ya hewa na video yake chafu.

Amber Rutty ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na tv mitandao Leo ijumaa. Amber Rutty amedai hii tabia ya watu kuvujisha picha mbaya mitandaoni inaharibu kizazi na Ni hatari kwa watoto wetu, na ameomba Sheria kali kuchukuliwa ili iwe funzo kwa watu wengine wwnye tabia mbaya Kama hizo.

Kwa hili naungana kabisa na dada Amber.
 
Back
Top Bottom