Kwa wale mnaofuatilia taarifa ya habari, kuna vijana waliokuwa wakizungumza wakiwa wamebanwa na malori baada ya kupata ajali na kuomba msaada kupitia vyombo vya habari.
Majeruhi wawili waliobanwa katika lori la mizigo katika ajali iliyotokea eneo la Maseyu barabara ya Morogoro - Chalinze wamefariki Dunia baada ya kuchelewa kuokolewa kwa zaidi ya masaa 16 kutokana na kukosekana kwa vifaa vya uokoaji.
Jambo la kusikitisha, pamoja na kwamba wamekaa hai kwa muda mrefu lakini vyombo sahihi vya kuwakwamua kutokana na kubanwa na malori vimekosekana hadi wakafa wanaona.
Mungu isaidie Tanzania, watu wanakufa baada ya kuwa hai kwa zaidi masaa 10.
Swali la kujiuliza, vipi kama Lori hilo lingekuwa limembana waziri au mkuu wa mkoa akiwa ndani ya gari lake?.
Bila kuoneana aibu, hapo serikali mmefanya uzembe! R.I.P my fellow poor