Waliobanwa katika ajali wafariki

Waliobanwa katika ajali wafariki

Mkuu, hatua tutachukua ila kwa hili la ajali hii tuna kila sababu ya kusikitika na kulalamika.
Mkuu Copper heshima mbele,ufisadi nyuma. Tumeshalalamika na kusikitika kwa maafa na ajali ngapi mkuu!?? Je malalamiko yetu na masikitiko yamesaidiaje kutatua na kupata ufumbuzi wa huu UZEMBE unaosababisha kupoteza maisha Watanzania wenzetu!!?? Maana Leo kwao hao wenzetu,kesho yaweza kuwa kwetu kukumbwa na hayo maafa.
Tafakari MTANZANIA mwenzangu na CHUKUA HATUA.
 
ni simanzi kuona watu wanaangamia kwa vifo vyenye kuumiza namna hii, hivi angebanwa mwanaasha ingekuwaje , Mapolisi misifa si wangeinua gari kwa meno
 
Wamenikera waandishi kuhoji mtu aliye katika hali ile...badala ya kuhakikisha mtu anapata huduma ya damu au drip na hewa ya kutosha wewe unampelekea mic??
hizo ambulance leo wikiend zimepaki kwenye mabaa au hazina mafuta..hakika huko tuendako nchi itakuwa na sheria vipande vipande kama somalia
Inkoskaz
Hivi kweli tuna jeshi la usalama barabarani? Huko wa IGP Mwema, yuko wapi Afande Mpinga....kwanini haya yanatokea kama vile hakuna serikali? Jana nimeshuhudia kwenye ITV taarifa ya habari saa 2 usiku walikuwepo askari polisi wakirandaranda eneo lile kumbe hawakuwa na msaada wowote hata kutoa taarifa ktk kitengo cha maafa ili kurescue wale watu. Watz watz watz mimi binafsi siamini kama tuko salama! Tafakari.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Copper heshima mbele,ufisadi nyuma. Tumeshalalamika na kusikitika kwa maafa na ajali ngapi mkuu!?? Je malalamiko yetu na masikitiko yamesaidiaje kutatua na kupata ufumbuzi wa huu UZEMBE unaosababisha kupoteza maisha Watanzania wenzetu!!?? Maana Leo kwao hao wenzetu,kesho yaweza kuwa kwetu kukumbwa na hayo maafa.
Tafakari MTANZANIA mwenzangu na CHUKUA HATUA.

Mkuu Bora69, kwa specific tukio tufanyeje? Ni ukweli ulio wazi zaidi 85% ya ajali zinasababishwa na uzembe, ila jana watu wamebanwa katika ajali na hapakuwa ja jitihada za maana za kuwanasua hadi wamekufa hapo ndio ninaposikitika. Ingekuwa ni mtu wa hadhi fulani jitihada zote zingefanyika ila kwa kuwa ni wanyonge ndio hivyo tena.
 
Mwenyezi Mungu nisamehe kwa haya niyasemayo ni ubinadamu naomba niandike kama binadamu na kiumbe chako.

Mwenyezi Mungu nauliza hii serikali ya awamu hii imekuja kutufundisha nini au unatupitisha jangwani? hivi ni haki kuanzia afisa mtendaji wa eneo la tukio hadi mkuu wa mkoa @#$%^&*()_(*&^%$ zao hawakuona au kuambiwa watu wanateseka kwa zaidi ya masaaa 10 kwa maumivu wamekalisha ------ yao ofisini wanatumbua hela zetu na vingora mabarabarani kweli?????????????????

Hivi afisa usalama na kamanda wa mkoa MOD tafadhari hawa watu ni ------- nashindwa niandikeje nieleweke kwa hisia na maumivu niliyonayo kwa waliyowakuta wananchi wenzangu.

Jifikirie wewe hata ukibanwa na mlango maumivu yake then jiweke wewe ndo umebanwa na vyuma, mwenyezi Mungu kama unaweza naomba mafuriko yaanzie magogoni plz sir GOD inaumaaaaaaaaaaaaaaaa

Ni uzembe wa serikali hii dhaifu¥€¤§*€@mayo..
 
BONGOLALAImeniuma sana kusikia wale majeruhi wamekufa wakijiona huku wakiomba msaada. Nasema imeniuma na kukata tamaa na kitengo cha maafa chini ya waziri mkuu. Nimewasikia mwenyewe jana wakihojiwa na mtangazaji wa ITV huku wakiomba kunasuliwa bila msaada. Majeruhi wale wapo pale zaidi ya masaa 16 na bado hakuna msaada mpaka wanakufa kweli CCM na serikali ina kazi kweli 2015 na bado wanasema watatawala hata miaka 50 ijayo!
Nakwambia hawa watu ni sh&@zy kabisa,wao wamekalia kufikiria kutengeneza video za ugaidi na ujinga wa propaganda mambo ya msingi yanayo husu raia hawana habari kabisa. Hili jambo hata lingetokea Kongo kwenye vita msaada wa serikali ungeonekana. Hivi kweli viongozi hawa tulionao wanapata wapi ujasiri wa kusimama mbele yetu na kubwabwaja maneno eti serikali sikivu ya chama cha Mapinduzi inawajali watanzania? Ni kuwa wametuona ni mafala sana sie kwa vile ndugu zetu wanakufa na sie tuna wachekea.Ndio maana bado yako majitu yanashinda humu JF kutetea uozo huu bila hata aibu kisa pesa ya lunch kwa damu za ndugu zao wanaokufa kwa mateso ya aina hii. Ahh,acha ninyamaze ila sasa tuamke na kusema basi!
 
Last edited by a moderator:
Saa 16 hata kama waokoaji wangekuwa wanatoka Canada wangeshafika. Tunayo serikali ya kung'oa kucha sio ya kuokoa watu wake.
 
Kidumu chama cha mapinduzi!! Natumai 2015 ndugu zao hawatafanya makosa
 
it real pains. I saw them yesterday!! Rest kwa amani mabrodaz
 
ukweli ni kwamba jambo hili ni lakusikitisha sana ingawa kila mtu kapangiwa wakati wake wa kufa ila si kwa uzembe kama huu uliofanywa na wahusika.

kama watu walitoka mpaka kwenda kuchukua habari and wamekuwa hapo kwa zaidi ya masaa 10 hebu wahusika fikirieni kama watu hawa wangekuwa ni watu toka kwenye familia zenu, kama mke, mtoto, mama au baba yako kweli ungeweza kuzembea kiasi hiki cha watu kushindwa kupata msaada for more than saa 10 mpaka wanakufa.

Ila siwezi kushangaa kwani inaonyesha nguvu zote za uokozi tulipeleka pale kwenye gorofa na kule arusha kwenye mgodi that way mlishindwa kwenda kuokoa watu hao walionasa kwenye gari kwa kuwa hapakuwa na posho na wala hapakuwa na mualiko kwenda kula na mzee wa kaya kama mngeokoa maisha ya watanzania hao.

Ukweli nchi yangu tanzanzania inanisikitisha sana kuona inaburuzwa bila ridhaa yake na watu wachache wenye matamanio yao ya kuila bila huruma wala kujali kuhusu kizazi chake kwa kuwa wenye haki ya kupatia huduma za haraka si watoto wa tanzania ila ni wale wanyonyaji wa tanzania.

Kwa kuwa shwala la uwajibikaji halipo kwenye katiba ya nchi hii, ni vema kuona wenzetu walitumia njia gani kuweka matatizo haya kando, ifike wakati nasi tufanye kama Misri ili kuondoa hawa madhalimu madarakani na si waondoke tuu bali wakamatwe na washitakiwe kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania na kwa kuua kwa kukusudia na wahukumiwe kunyongwa.

Ni hayo tuu
 
Waokoaji walivimbiwa pilau la Ikulu....wao huwa wanasubiri mfe....na bora hawakuja...wangekata miguu,kichwa n.k..hukuona pale posta kwenye ghorofa!!!?
 
serikali ya ccm itaendelea kuongoza hivi hivi mkiona na tutaendelea kufa hivi hivi kwa ushenzi wa serikali ya ccm
 
Dah, katika hali kama ile kweli waandishi wa habari wamefika pale wakapiga picha na kuzirusha hewani, basi? Haki ya nani watz tumechoka, kuanzia rais hadi raia wa kawaida.

Tunawapigia kelele CCM na Kikwete kwenye hili wakati waandishi wa habari na raia wengine wa kawaida waliwahi kufika eneo la tukio. Wameshindwa kweli kufanya jitihada zozote kusaidia uokoaji? Kazi yao tu ilikuwa kupiga picha na kuwafanya tamasha katika vyombo vya habari hao vijana wawili wanavyogugumia kwa maumivu makali?

Ingekuwa nchi zingine raia wa kawaida waliowahi kufika eneo la tukio wangefanya maarifa yote kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanafanya kitu pale. Suala la kulaumu serikali halisaidii chochote katika hali kama ile.

Unamwona kabisa mtu amebanwa kabisa kwenye vyuma we kazi yako ni kunyosha mikono na kuchukua picha tu? Kweli?

Serikali inaakisi raia wenyewe tulivyo. Mijamaa imefika pale imepiga picha na kuzipeleka studio, basi.
 
Maskini inasikitisha sana, ila Mungu amewapumzisha wangekua walemavu wangeteseka sana hapa dunian, najua inauma kwa familia ila Mungu amewapumzisha, Tanzania Yetu inatuangusha kila cku. Rest in peace ndugu zetu.
 
Tusishangae wenzetu wakaunda tume hii mijitu mijinga sana.
 
Inasikitisha kwakweli. Na lazima hii taarifa walikua wanaijua lakini wakaipuuzia. Wale watu walikua na faida gani kwao? Au labda walihisi watatoka kwa miujiza. Kweli hii ni too much. Rest in peace
 
Tatizo tumekuwa mazuzu hadi kila kitu tunategemea serikali. Tungewa na ubinadamu hao watu tungewaokoa bila kusubiri serikali ilete vifaa vyake. Ila kwa sababu kila kinachotokea tunaona serikali ndio inahusika basi sishangai kuona hao watu wamekufa bila msaada. Nina uhakika huo muda wa masaa 16 yamepita malori na matrekta ambayo yangeweza kutoa msaada kwa kiasi kikubwa, ila uokoaji ni kazi ya serikali ndio maana tumewaacha wenzetu wafe na kukimbilia kulalamika huku Jf.
 
Back
Top Bottom