Ajali Morogoro: Gari la abiria lagonga lori kwa nyuma, wawili wafariki dunia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro eneo la Oilcom Nanenane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Fortunatus Muslimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu kuwa Said Abdallah ambaye alikuwa dereva wa gari hilo pamoja na Ramadhan Muya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 hadi 35 ambaye alikuwa ni kondakta wa gari hilo.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa chanzo ni mwendokasi.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni siku chache tangu watu 22 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ahmeed baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likisafirishwa kwenda nje ya nchi lenye namba za IT 2816 katika eneo la Melela Kibaoni Barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

Chanzo: Global Publishers

Pia Soma...
Morogoro: Watu 22 Wamefariki dunia kwenye ajali ya Basi la Ahmed linalofanya safari kati ya Tanga-Mbeya. Limegongana na Lori
 
Pale napo barabara ni nyembamba sana isee double road inatakiwa ianzie Mikese mpk Mzumbe.
 
Nyingine hii, imetokea jana maeneo ya Mikese hukohuko Morogoro, ikihusisha basi la Libanika Tours
Screenshot_20220320-153709_Gallery.jpg
 
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro eneo la Oilcom Nanenane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Fortunatus Muslimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu kuwa Said Abdallah ambaye alikuwa dereva wa gari hilo pamoja na Ramadhan Muya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 hadi 35 ambaye alikuwa ni kondakta wa gari hilo.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa chanzo ni mwendokasi.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni siku chache tangu watu 22 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ahmeed baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likisafirishwa kwenda nje ya nchi lenye namba za IT 2816 katika eneo la Melela Kibaoni Barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

Chanzo: Global Publishers

Pia Soma...
Morogoro: Watu 22 Wamefariki dunia kwenye ajali ya Basi la Ahmed linalofanya safari kati ya Tanga-Mbeya. Limegongana na Lori
Hii barabara ya Morogoro daily hailali njaa
 
Back
Top Bottom